Napinga Makao Makuu ya nchi kuhamia Dodoma

Napinga Makao Makuu ya nchi kuhamia Dodoma

Kuna miji kama Manyoni kukua na kupanuka kutokana na kuwa karibu na mji mkuu.Biashara zitaongezeka.Hii ni faida.
Miji mingi itakuwa hususani morogoro na miji mingi iliyopo njiani kuelekea Dodoma .
 
Dar imewahi kua capital city lini mkuu?
Sio huyu tu bro kuna watu wengi sana wana fikra kama za huyu na hii ni kwasababu kila kizur kinaanzia Dar, hebu kwa mfano niambie sababu za kujenga viwanja viwili vikubwa na vizur eneo moja, shamba la bb ingeboreshwa vzur na ule wa Wachina ukajengwa Dom tungeweza host hata michuano ya kimataifa maana tungekuwa na kiwanja kizur Dar, Mwanza, Dom na Arusha nacho wangekiboresha hayo ndio maendeleo
 
Kwa maoni yangu nadhani tunaweza kuuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu. Japo tunahitaji mapango endelevu ya kuimarisha miundo mbinu kwa takribani miaka 20 hivi... Tukikurupuka itatugharimu sana..
 
Kuamia Dodoma inawezekana. Kwa dharura serikali inaweza kuamia kwenye majumbani yaliyojengwa na NSSF mkoani Dodoma na serikali itakuwa inarejesha taratibu deni la maghorofa hayo. Majengo hayo yanaweza kubadilishwa kidogo ili yakidhi haja ya kuwa ofisi za serikali. Pia UDOM kuna majengo yapo wazi na hawajapata Watumiaji,nayo yanaweza kukidhi hadhi ya kuwa ofisini za serikali kwa maboresho kidogo. Awali niliwahi kushauri wabunge wawe wapangaji wa majumbani ya NSSF hapo Dodoma wakanikatalia, sasa serikali msilete kisingizio cha kukosa majengo wakati haya yapo. Ni yule mwenye vitega uchumi vyake Dar es Salaam wakati anafanya kazi serikali anayeweza kuwa na fikra za kuona jambo la kuamia Dodoma ni dhambi.
 
Kwenda Dodoma ni lazima, sio ombi, Dar inahtaji kupumua.

Limji kileshindikana hata kupimwa watu wanajijengea watakavyo.

Wanajilock na kushindwa kufika makwao kisa hamna road
 
Kule Darban South Africa na Mombasa Kenya kuna Bahari kuna Bahari na serikali hawapo huko na Johannesburg na Nairob ni majiji makubwa hayapo karibu na Bahari .
Ongezea na Cairo hakuna bahar ila haitakuja hii Dar yetu na bahar yake iifikie na ndio mji mkuu wa Misri
 
Dah.... Hili la uhakiki wa vyeti sasa naunga mkono kwa 100%[emoji4] [emoji4]
 
Ongezea na Cairo hakuna bahar ila haitakuja hii Dar yetu na bahar yake iifikie na ndio mji mkuu wa Misri

Ukweli mtupu,
Hao wanakomaa serikali ibakie Dar shauri yao, ningeshauri wajiandae kisaikolojia
 
T2020DOM. Someni namba hiyo na muielewe vizuri
 
Thamani ya Dodoma imebadilika toka JPM atangaze neema
 
Wewe hamna kitu kabisa...ulichoandika Pumba tupu aisee...think beyond the reality
Huyu mleta mada bado kinda sana kwenye historia ya dunia na miji mijuu yake..

Pili ni mvivu wa kufanya tafiti na kujua why Dodoma and not Dar es salaam..

Tatu anaongozwa na ushabiki badala ya uhalisia..

Tumsameheni bure maana hajui alichokiandika..
 
Kuna miji kama Manyoni kukua na kupanuka kutokana na kuwa karibu na mji mkuu.Biashara zitaongezeka.Hii ni faida.
 
Inasikitisha kwamba serikali bado ina ndoto za kufanya Dodoma iwe mji mkuu wa Tanzania kiutawala. Kusudi Dodoma iwe makao makuu inabidi serikali itumie hela nyingi kujenga majumba ya wizara mbalimbali, nyumba za watendaji, miundombinu n.k. Hiyo yote itagharimu hela nyingi ili kufanikisha azma ya kuhamia Dodoma.

Lakini kwa nini makao makuu ya serikali yahamie Dodoma? Kwani huko kuhamia kutaongeza ufanisi wa utendaji kazi serikalini? Si rahisi. Ukweli ni kwamba serikali itaongeza gharma za kujiendesha na kuongeza ufisadi kwa kiwango kikubwa tu.

Hili zoezi la kuhamia Dodoma lilianzishwa mwaka 1973, na mpaka leo ni wizara moja tu (TAMISEMI) ndiyo ipo Dodoma. Na hata hivyo watendaji wake wa juu muda mwingi wapo Dar es Salaam wakihudhuria vikao mbalimbali, wakiongezea serikali gharama - nauli, posho, mafuta ya magari, n.k..

Kwa sabau serikali tayari imeisha poteza pesa katika huu mradi wa kuhamia ni vema iachane nao, kusudi iokoe pesa zingine ambazo zitafanya shuguli zingine za kimaendeleo, k.m. ujenzi wa barabara, zahati, mashule, nyumba za walimu, n.k. Watanzania tuachane na tabia za kutumia au kuishi kupita uwezo wetu. Dhana kwamba Dodoma ikiwa katikati ya nchi huduma na maendeleo vitapatikana kwa urahisi na bei nafuu haina punje ya ukweli wowote.

Nchi nyingi tu duniani miji yao mikuu ya kiutawala au kiuchumi haiko katikati ya nchi hizo. Mifano michache itatosha kuonyesha upotofu wa dhana hii ya kuhamia Dodoma: Washington na New York ya Marekani, Moscow ya Urusi, Beijing Uchina, n.k. Tuachane na tabia ya kuteng'eneza ulaji kwa mafisadi.

Kuhamishia makao makuu Dodoma ni dhambi. Ni dhambi kwa sababu watanzania wengi wanapoteza haki zao za kupata huduma stahili toka serikalini, na wanaendelea kuteseka huku wachache wakiendelea kutafuna hela za walipakodi kwa visingizio vya kuhamia Dodoma.

Watanzania wote tupendao nchi yetu tukatae huu ufujaji wa pesa zetu.
Mheshimiwa acha hoja za kitoto. Kuhamishia makao makuu dodoma ni muhimu. Angalia Nigeria walihamisha toka Lagos kwenda Abuja lkn hiyo haikuondoa hadhi ya Lagos kuwa jiji kubwa la kibiashara kuliko yote. Tumwache Rais atimize dhamira siyo tunapinga kila kitu. Wafanyakazi wasiotaka kwenda Dom wanahaki ya kuacha kama hawapendi
 
Back
Top Bottom