Napinga Makao Makuu ya nchi kuhamia Dodoma

Napinga Makao Makuu ya nchi kuhamia Dodoma

Kama hayo matakwa ya Rais wa kwanza ni mazito kiasi hicho, ilikuwaje hadi leo hiyo Dodoma si makao makuu?
Hadi leo lini? Unapofanya plan sio kwamba ndio unatekeleza wakati huo.
Sasa hivi ndio wakati mwafaka wa kufanya hivyo.
Kila jambo na wakati wake na majira mwafaka. Acha utoto basi. Jitahidi kuwa GT.
 
1. kama Dar kumeimarika kiuchumi inamaana kila kitu kiwepo Dar?... je hauoni madhara msongamano wa vitu dar, madhara kuanzia kwenye afya, uchumi n.k

2. Nakubaliana na sababu yako ya Gharama

3. Kufanya Dodoma makao makuu kutaendeleza sio Dodoma tuu bali kupeleka maendeleo na mikoa mingine ya karibu kama singida na Tabora

3. Dodoma ni centre ya Tanzania.. hivyo kuna Geographical advantage ya serikali kuweka makao makui pale kushinda Dar..

Kwa miaka yote hii ambapo Dar 'ilikuwa kama ndio capital city', miji ya Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe, Rufiji, etc ambayo ipo karibu na dar imeendelea kiasi gani? Mbona watu wanajibana pale pale Dar? Hapa suala ni upangiliaji. Kama watu wataruhusiwa kujianzishia vijimakazi vyao, Dodoma nayo itakuwa squatter kama Dar na hayo 'maendeleo' hayatafika Singida, achilia mbali Tabora.
 
Hadi leo lini? Unapofanya plan sio kwamba ndio unatekeleza wakati huo.
Sasa hivi ndio wakati mwafaka wa kufanya hivyo.
Kila jambo na wakati wake na majira mwafaka. Acha utoto basi. Jitahidi kuwa GT.
U-GT haulazimishwi na ukubwa haulazimishwi kama unavyotaka kufanya wewe. Be objective and think freely. Acha kukariri mambo. Kwa sentensi yako hiyo nimegundua ninajadiliana na under age, immature physically and intellectually perhaps.
 
Kabla ya kuandi ni vizuri ukafanya reseach japo kidogo. Usiwe mzembe kiasi hicho.

Makao makuu ya Tanzania ni Dodoma. Dar es Salaam ni mji wa kibiashara.
Sababu ulizozitoa ni za kitoto sana.

Na shughuli za Serikali zikihamia Dodoma utafanya jiji la Dar es salaam biashara ziende haraka. Halafu kumbuka dodoma ni katikati ya nchi kwa hiyo watu wanaweza kufikia ofsi kuu za serikali kirahisi.

Fanya uchunguzi kwanza ujue Rais wa kwanza baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwanini alitaka makao makuu yawe dodoma.

Mawazo ya 1975 ndiyo unataka ya apply now 2016 .....

in this era you can run the government inside a kiosk electronically

Puke .....
 
Mawazo ya 1975 ndiyo unataka ya apply now 2016 .....

in this era you can run the government inside a kiosk electronically

Puke .....
Acha utoto na ujinga. Unajua electron wewe? Au unajishaua.
 
Mh. Rais wa jamhuri ya Muungano wa TZ amesema atafanya jitihada makao makuu ya nchi yahamie Dodoma. mimi kwa hili nakataa kwa sababu zifuatazo!
1. Dar imeshajiimarisha na kujijenga vizuri kama makao makuu ya nchi. ina hadhi ya kuwa CAPITAL CITY
2. Kuhamia Dom kutasababisha tuyumbe kiuchumi kwani pesa nyingi zitatumika kujenga majengo ya ofic za umma na miundombinu kwa ujumla.
3. Hamna uwanja wa ndege wa kimataifa wala bandari kama Dar.
4. gharama za maisha na huduma zitakuwa juu sn. mizigo mingi ya Dom itashukia kwanza Dar kisha ndo isafirishwe. kumbuka Dom itakuwa na watu wengi.
5. Hivi Dodoma kuna nini hata tukung'ang'anie?

Wewe hamna kitu kabisa...ulichoandika Pumba tupu aisee...think beyond the reality
 
Kabla ya kuandi ni vizuri ukafanya reseach japo kidogo. Usiwe mzembe kiasi hicho.

Makao makuu ya Tanzania ni Dodoma. Dar es Salaam ni mji wa kibiashara.
Sababu ulizozitoa ni za kitoto sana.

Na shughuli za Serikali zikihamia Dodoma utafanya jiji la Dar es salaam biashara ziende haraka. Halafu kumbuka dodoma ni katikati ya nchi kwa hiyo watu wanaweza kufikia ofsi kuu za serikali kirahisi.

Fanya uchunguzi kwanza ujue Rais wa kwanza baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwanini alitaka makao makuu yawe dodoma.
Sababu nyingi ni outdated na kwa dunia ya sasa hazi-apply
 
Dodoma kuko vizuri tu..Baadhi ya ofisi za serikali zipo tayari. Dodoma inakua kwa kasi sana,imepangika vizuri. Serikali kuendelea kubaki Dar ni tatizo,foleni kila siku zinaongezeka kwa sababu watu wengi wapo huko. Serikaki ikihamia Dom ni kweli mwanzoni lazima gharama ziwepo lakini baada ya kuhamia serikali itajiendesha kwa gharama ndogo. Dar inatakiwa ibakie kuwa ni mji wa kibiashara tu. Najua kuna wanaopinga kwa sababu wamezoea kuishi Dar mabadiliko kama haya lazima kuna waty wataumia. Magufuli akikamilisha hili lakuhamisha serikali nitamsifu sana.
 
Bila kujali sababu za kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, uamuzi wa kufanya hivyo ulifanyika mwaka 1973 (miaka 43 iliyopita!) wakati ambapo Nigeria walikuwa hata hawajafikiria kuhamishia serikali Abuja. Baada ya Nigeria kuamua kuhamishia serikali Abuja, walituma wataalamu wake CDA ili kujifunza na kupata uzoefu wa maandalizi ya kuhamisha makao makuu ya serikali. Waliporudi nyumbani wakatumia kikamilifu uzoefu walioupata Tanzania na Abuja ukawa mji mkuu wa Nigeria rasmi December 1991 baada ya wizara zote na ofisi za ubalozi kuhamia huko. Tatizo kubwa hapa kwetu ni kukosekana nia na utashi wa kuhamia Dodoma. Wanasiasa kama Magufuli wanatoa kauli ya "kuhamia Dodoma" kwa lengo tu na kupata umaarufu wa papo kwa papo na wanakumbuka tu suala la kuhamia Dodoma wanapokuwa Dodoma!
 
U-GT haulazimishwi na ukubwa haulazimishwi kama unavyotaka kufanya wewe. Be objective and think freely. Acha kukariri mambo. Kwa sentensi yako hiyo nimegundua ninajadiliana na under age, immature physically and intellectually perhaps.
Also age means nothing too, kwanini usijibu hoja yake unaanza kumshambulia, kama uliona amekosea si ungemrekebisha?
Nyie wazee huwa mnatuaminisha kuwa mmejaa busara kumbe haiko hivyo wakati wote,,.
What I know hoja hujibiwa kwa hoja, and not insult,
Insult ni kwa wasiojiamini.
 
Also age means nothing too, kwanini usijibu hoja yake unaanza kumshambulia, kama uliona amekosea si ungemrekebisha?
Nyie wazee huwa mnatuaminisha kuwa mmejaa busara kumbe haiko hivyo wakati wote,,.
What I know hoja hujibiwa kwa hoja, and not insult,
Insult ni kwa wasiojiamini.
Haujasoma comment yake niliyojibu ndiyo maana unadhani sijajibu hoja yake. yeye amesema NIACHE UTOTO, wewe unaona hiyo ni kauli sawa? Ina maana yeye ameniita mtoto, which means yeye ndiyo mkubwa/mzee (na si vinginevyo kama unavyosema wewe)
 
Usimwamini Mwanasiasa
Kama angetaka hamia huko asingewekeza sana hapa
Au ule uwanja ungejengwa international
 
Kwa uelewa wangu huu mdogo Tangu nikiwa mtoto nimekuwa nikilifikiria siku moja atokee kiongozi anaejiamini ahamishie serikali dodoma , kama haiwezekani basi kila kilichopo Dodoma kurudi dar na iamuliwe rasmi kama makao makuu ya nchi ni dar na sio Dodoma tena
Hatuwezi kuwa na serikali imejigawa nusu Dodoma nusu dar,
Viongozi wanakaa dar, hata mbunge wangu anakaa dar,hiyo haijakaa sawa,
Thanks God Magu ametamka,
Na ameahidi kuhamia chamwino, naamini matamko ya mh.Magufuli sio kama ya watawala waliopita,
Hoja za Gharama sioni kama ni za msingi sana maana awamu zilizopita watu wamefuja pesa zetu na hatukufanya lolote zaidi ya kuumia na kulalamika tu humu, this time ngoja tuumie kwa hizi gharama but angalau tuwe na cha kukionesha in next 10 years,
Kwa mbali naona Dodoma inayopendeza, na yenye mpangilio mzuri mithiri ya Abuja ..
Nigeria waliweza na sisi lazima tuweze

My president go ahead, ukisikiliza hawa watu utajijuta 2020 hii hapa na hujafanya LA maana,
And I am so sure baada ya miaka 10 watu mtarudi hapa kumpongeza magufuli kwa hii hatua,
God bless Tanzania
 
Inasikitisha kwamba serikali bado ina ndoto za kufanya Dodoma iwe mji mkuu wa Tanzania kiutawala. Kusudi Dodoma iwe makao makuu inabidi serikali itumie hela nyingi kujenga majumba ya wizara mbalimbali, nyumba za watendaji, miundombinu n.k. Hiyo yote itagharimu hela nyingi ili kufanikisha azma ya kuhamia Dodoma.

Lakini kwa nini makao makuu ya serikali yahamie Dodoma? Kwani huko kuhamia kutaongeza ufanisi wa utendaji kazi serikalini? Si rahisi. Ukweli ni kwamba serikali itaongeza gharma za kujiendesha na kuongeza ufisadi kwa kiwango kikubwa tu.

Hili zoezi la kuhamia Dodoma lilianzishwa mwaka 1973, na mpaka leo ni wizara moja tu (TAMISEMI) ndiyo ipo Dodoma. Na hata hivyo watendaji wake wa juu muda mwingi wapo Dar es Salaam wakihudhuria vikao mbalimbali, wakiongezea serikali gharama - nauli, posho, mafuta ya magari, n.k..

Kwa sabau serikali tayari imeisha poteza pesa katika huu mradi wa kuhamia ni vema iachane nao, kusudi iokoe pesa zingine ambazo zitafanya shuguli zingine za kimaendeleo, k.m. ujenzi wa barabara, zahati, mashule, nyumba za walimu, n.k. Watanzania tuachane na tabia za kutumia au kuishi kupita uwezo wetu. Dhana kwamba Dodoma ikiwa katikati ya nchi huduma na maendeleo vitapatikana kwa urahisi na bei nafuu haina punje ya ukweli wowote.

Nchi nyingi tu duniani miji yao mikuu ya kiutawala au kiuchumi haiko katikati ya nchi hizo. Mifano michache itatosha kuonyesha upotofu wa dhana hii ya kuhamia Dodoma: Washington na New York ya Marekani, Moscow ya Urusi, Beijing Uchina, n.k. Tuachane na tabia ya kuteng'eneza ulaji kwa mafisadi.

Kuhamishia makao makuu Dodoma ni dhambi. Ni dhambi kwa sababu watanzania wengi wanapoteza haki zao za kupata huduma stahili toka serikalini, na wanaendelea kuteseka huku wachache wakiendelea kutafuna hela za walipakodi kwa visingizio vya kuhamia Dodoma.

Watanzania wote tupendao nchi yetu tukatae huu ufujaji wa pesa zetu.
Hata ukatae wakati rais ameshasema itasidia nini ama unatafuta kiki na wewe uonekane IPO
 
Kuna miji kama Manyoni kukua na kupanuka kutokana na kuwa karibu na mji mkuu.Biashara zitaongezeka.Hii ni faida.
 
Back
Top Bottom