Napinga Makao Makuu ya nchi kuhamia Dodoma

fmesanga

Member
Oct 2, 2007
14
3
Inasikitisha kwamba serikali bado ina ndoto za kufanya Dodoma iwe mji mkuu wa Tanzania kiutawala. Kusudi Dodoma iwe makao makuu inabidi serikali itumie hela nyingi kujenga majumba ya wizara mbalimbali, nyumba za watendaji, miundombinu n.k. Hiyo yote itagharimu hela nyingi ili kufanikisha azma ya kuhamia Dodoma.

Lakini kwa nini makao makuu ya serikali yahamie Dodoma? Kwani huko kuhamia kutaongeza ufanisi wa utendaji kazi serikalini? Si rahisi. Ukweli ni kwamba serikali itaongeza gharma za kujiendesha na kuongeza ufisadi kwa kiwango kikubwa tu.

Hili zoezi la kuhamia Dodoma lilianzishwa mwaka 1973, na mpaka leo ni wizara moja tu (TAMISEMI) ndiyo ipo Dodoma. Na hata hivyo watendaji wake wa juu muda mwingi wapo Dar es Salaam wakihudhuria vikao mbalimbali, wakiongezea serikali gharama - nauli, posho, mafuta ya magari, n.k..

Kwa sabau serikali tayari imeisha poteza pesa katika huu mradi wa kuhamia ni vema iachane nao, kusudi iokoe pesa zingine ambazo zitafanya shuguli zingine za kimaendeleo, k.m. ujenzi wa barabara, zahati, mashule, nyumba za walimu, n.k. Watanzania tuachane na tabia za kutumia au kuishi kupita uwezo wetu. Dhana kwamba Dodoma ikiwa katikati ya nchi huduma na maendeleo vitapatikana kwa urahisi na bei nafuu haina punje ya ukweli wowote.

Nchi nyingi tu duniani miji yao mikuu ya kiutawala au kiuchumi haiko katikati ya nchi hizo. Mifano michache itatosha kuonyesha upotofu wa dhana hii ya kuhamia Dodoma: Washington na New York ya Marekani, Moscow ya Urusi, Beijing Uchina, n.k. Tuachane na tabia ya kuteng'eneza ulaji kwa mafisadi.

Kuhamishia makao makuu Dodoma ni dhambi. Ni dhambi kwa sababu watanzania wengi wanapoteza haki zao za kupata huduma stahili toka serikalini, na wanaendelea kuteseka huku wachache wakiendelea kutafuna hela za walipakodi kwa visingizio vya kuhamia Dodoma.

Watanzania wote tupendao nchi yetu tukatae huu ufujaji wa pesa zetu.
 
Wanajamvi,

Nakiri siasa si fani yangu lakini naomba kuleta hoja hii zaidi kama mwanachi mwenye uchungu na si mchambuzi wa mambo ya kisiasa.

Binafsi natambua dhamira ya dhati ya muda mrefu ya serikali yetu na vilevile nina(sympathize) na wakazi wa makao makuu ambao wangependa kuona ndoto zao zinatimia.

Inaweza kuonekana udhaifu kwa Chama Cha Mapinduzi kuukubali ukweli kwamba swala la Dodoma halitekelezeki tena. Lakini inaweza kuwa ni jambo jema na la kizalendo kuliokoa taifa letu katika hasara kubwa kwa miaka mingi ijayo.

Kwa kuangalia nyuma na tunakokwenda naona kwamba:-

1) Serikali imetumia gharama nyingi na kwa muda mrefu kujaribu kuhamisha makao makuu bila mafanikio. (Bajeti ya CDA, wizara kuhama na kurudi, Vipindi vya bajeti bungeni n.k)

2) Hakuna dalili ya baadhi ya wizara na idara kuhama siku za karibuni na uwekezaji ulio na unaoendelea kufanyika Dar ni mkubwa sana.

3) Mashirika ya wahisani, balozi mbali mbali na wadau wengine ambao serikali inahitaji kuwa karibu nao hawana dhamira ya kuhama.

4) Itachukua miaka mingi na uwekezaji wa hali ya juu kuupa mji wa Dodoma hadhi ya kimaisha itakayowavutia watumishi wa serikali kuu na idara zake kutoka Dar na kwenda kuishi Dodoma.

5) Pamoja na kuwa na barabara nzuri kwa sasa, na kuwa katikati ya nchi, bado hatuna mfumo wa miundo mbinu unaoiwezesha Dodoma kufikika kirahisi toka pande zote za nchi.

6) Kugawa viwanja na kutenga bilioni 30 sidhani kama inatosha kubadili muelekeo wa tatizo hili sugu.

WAKATI SASA UFIKE TUUKUBALI UKWELI...hili halitekelezeki ndugu zangu!.

Hatuhitaji manabii kutufunulia hili, tumejifunza vya kutosha katika hili.
 
Mh. Rais wa jamhuri ya Muungano wa TZ amesema atafanya jitihada makao makuu ya nchi yahamie Dodoma. mimi kwa hili nakataa kwa sababu zifuatazo!

1. Dar imeshajiimarisha na kujijenga vizuri kama makao makuu ya nchi, ina hadhi ya kuwa CAPITAL CITY

2. Kuhamia Dom kutasababisha tuyumbe kiuchumi kwani pesa nyingi zitatumika kujenga majengo ya ofic za umma na miundombinu kwa ujumla.

3. Hamna uwanja wa ndege wa kimataifa wala bandari kama Dar.

4. Gharama za maisha na huduma zitakuwa juu sn. mizigo mingi ya Dom itashukia kwanza Dar kisha ndo isafirishwe. kumbuka Dom itakuwa na watu wengi.

5. Hivi Dodoma kuna nini hata tukung'ang'anie?
 
Kabla ya kuandi ni vizuri ukafanya reseach japo kidogo. Usiwe mzembe kiasi hicho.

Makao makuu ya Tanzania ni Dodoma. Dar es Salaam ni mji wa kibiashara.
Sababu ulizozitoa ni za kitoto sana.

Na shughuli za Serikali zikihamia Dodoma utafanya jiji la Dar es salaam biashara ziende haraka. Halafu kumbuka dodoma ni katikati ya nchi kwa hiyo watu wanaweza kufikia ofsi kuu za serikali kirahisi.

Fanya uchunguzi kwanza ujue Rais wa kwanza baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwanini alitaka makao makuu yawe dodoma.
 
Kuna siku nilimsikia Makufuli kwenye hotuba ya Wazee wa Dar(CCM) Kuwa Dar ndio Tanzania hivyo ni lazima ipewe kipaumbele.

Ila kuamia Dodoma ni Jambo zuri wasiwasi wangu ni Tamko maana yeye si wa kwanza kusema hivyo.
 
1. kama Dar kumeimarika kiuchumi inamaana kila kitu kiwepo Dar?... je hauoni madhara msongamano wa vitu dar, madhara kuanzia kwenye afya, uchumi n.k

2. Nakubaliana na sababu yako ya Gharama

3. Kufanya Dodoma makao makuu kutaendeleza sio Dodoma tuu bali kupeleka maendeleo na mikoa mingine ya karibu kama singida na Tabora

3. Dodoma ni centre ya Tanzania.. hivyo kuna Geographical advantage ya serikali kuweka makao makui pale kushinda Dar..
 
Akili yako inafanya kazi?

Hiyo ni njia mojawapo ya mendeleo hujui Tanzania bado tunahitaji miji ilijijenga hivyo kupeleka serikali dom kutafanya tuwe na miji mingi.

Na foleni DAr unajua tunapoteza hela kiasi gani ?

Unajua watu wangapi wanakufa kwa ajili ya overpopulation Dar?

Gharama za watu kutoka mikoani kwenda Dar unaijua kulinganisha na Dodoma ambapo ni rahisi kufikika?

Akili yangu ya miaka 17 imewaza hivyo wewe akili yako ya miaka mingapi imewaza hayo?
 
Uwanja wa ndege ushaanza kutengenezwa, watu wanahamishwa maeneo ya karibu kupisha ujenzi na kupanua eneo

Nb: Dodoma ni makao makuu ya chama na serikali,serikali kuwa Dar, sasa mbona kama Dodoma ni makao makuu hewa??
 
Huu mwandiko wa mvulana, umetoa sababu za kitoto mno, yaan nimejihisi ninasoma mapendekezo ya mwanangu sonia mwenye miaka 10
 
Mh. Rais wa jamhuri ya Muungano wa TZ amesema atafanya jitihada makao makuu ya nchi yahamie Dodoma. mimi kwa hili nakataa kwa sababu zifuatazo!
1. Dar imeshajiimarisha na kujijenga vizuri kama makao makuu ya nchi. ina hadhi ya kuwa CAPITAL CITY
2. Kuhamia Dom kutasababisha tuyumbe kiuchumi kwani pesa nyingi zitatumika kujenga majengo ya ofic za umma na miundombinu kwa ujumla.
3. Hamna uwanja wa ndege wa kimataifa wala bandari kama Dar.
4. gharama za maisha na huduma zitakuwa juu sn. mizigo mingi ya Dom itashukia kwanza Dar kisha ndo isafirishwe. kumbuka Dom itakuwa na watu wengi.
5. Hivi Dodoma kuna nini hata tukung'ang'anie?

Nakushauri kafanye tathmini ya miji mikuu mingine duniani kisha uone kama huhitaji kubadili fikra...

Kwa ufupi tuu.. Dar imeshapanuka to the extent of a breaking point.. tunachofanya Dar sasa hivi ni kuvunja mijengo ya zamani na kujenga mapya on the same spot.. sasa kwanini tusihamie dodoma mkuu??

Mfano mizuri Pretoria na Jo'berg, NY na DC, Beijing na Shangai,
 
Kabla ya kuandi ni vizuri ukafanya reseach japo kidogo. Usiwe mzembe kiasi hicho.

Makao makuu ya Tanzania ni Dodoma. Dar es Salaam ni mji wa kibiashara.
Sababu ulizozitoa ni za kitoto sana.

Na shughuli za Serikali zikihamia Dodoma utafanya jiji la Dar es salaam biashara ziende haraka. Halafu kumbuka dodoma ni katikati ya nchi kwa hiyo watu wanaweza kufikia ofsi kuu za serikali kirahisi.

Fanya uchunguzi kwanza ujue Rais wa kwanza baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwanini alitaka makao makuu yawe dodoma.
Kama hayo matakwa ya Rais wa kwanza ni mazito kiasi hicho, ilikuwaje hadi leo hiyo Dodoma si makao makuu?
 
Nakushauri kafanye tathmini ya miji mikuu mingine duniani kisha uone kama huhitaji kubadili fikra...

Kwa ufupi tuu.. Dar imeshapanuka to the extent of a breaking point.. tunachofanya Dar sasa hivi ni kuvunja mijengo ya zamani na kujenga mapya on the same spot.. sasa kwanini tusihamie dodoma mkuu??

Mfano mizuri Pretoria na Jo'berg, NY na DC, Beijing na Shangai,
Unataka kusema kwamba ili kukuza mji fulani solution ni kuhamishia makao makuu ya nchi huko? Kwani Dodoma imeshindikana nini kuendelea katika hali yake ya sasa? na vipi kuhusu Mbeya, Tabora, Songea, Musoma..zenyewe zitaendeleaje?

Kama ni suala la kupanuka kwa jiji la Dar near breaking point, kwa nini attention isihamishiwe katika kuendeleza miji yenye nafasi kibiashara?
 
Mbona Kenya haikufanya Mombasa kuwa capital city? Nchi haitakiwi kuendelea upande mmoja so nahisi waliopita walichelewa tuu
 
Akili yako inafanya kazi?
Hiyo ni njia mojawapo ya mendeleo hujui Tanzania bado tunahitaji miji ilijijenga hivyo kupeleka serikali dom kutafanya tuwe na miji mingi.

Na foleni DAr unajua tunapoteza hela kiasi gani ?

Unajua watu wangapi wanakufa kwa ajili ya overpopulation Dar?

Gharama za watu kutoka mikoani kwenda Dar unaijua kulinganisha na Dodoma ambapo ni rahisi kufikika?

Akili yangu ya miaka 17 imewaza hivyo wewe akili yako ya miaka mingapi imewaza hayo?
Kweli hiyo ni akili ya miaka 17 au pungufu ya hapo. Nakubaliana na wewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom