Napinga Makao Makuu ya nchi kuhamia Dodoma

Napinga Makao Makuu ya nchi kuhamia Dodoma

Mh. Rais wa jamhuri ya Muungano wa TZ amesema atafanya jitihada makao makuu ya nchi yahamie Dodoma. mimi kwa hili nakataa kwa sababu zifuatazo!

1. Dar imeshajiimarisha na kujijenga vizuri kama makao makuu ya nchi, ina hadhi ya kuwa CAPITAL CITY

2. Kuhamia Dom kutasababisha tuyumbe kiuchumi kwani pesa nyingi zitatumika kujenga majengo ya ofic za umma na miundombinu kwa ujumla.

3. Hamna uwanja wa ndege wa kimataifa wala bandari kama Dar.

4. Gharama za maisha na huduma zitakuwa juu sn. mizigo mingi ya Dom itashukia kwanza Dar kisha ndo isafirishwe. kumbuka Dom itakuwa na watu wengi.

5. Hivi Dodoma kuna nini hata tukung'ang'anie?
Kuhusu swala la uwanja wa ndege upo unaojengwa makotopora uwanja mkubwa sana wanasema utakuwa wa pili africa kwa ukubwa na ujenzi ulianza 2010
 
Dodoma kuko vizuri tu..Baadhi ya ofisi za serikali zipo tayari. Dodoma inakua kwa kasi sana,imepangika vizuri. Serikali kuendelea kubaki Dar ni tatizo,foleni kila siku zinaongezeka kwa sababu watu wengi wapo huko. Serikaki ikihamia Dom ni kweli mwanzoni lazima gharama ziwepo lakini baada ya kuhamia serikali itajiendesha kwa gharama ndogo. Dar inatakiwa ibakie kuwa ni mji wa kibiashara tu. Najua kuna wanaopinga kwa sababu wamezoea kuishi Dar mabadiliko kama haya lazima kuna waty wataumia. Magufuli akikamilisha hili lakuhamisha serikali nitamsifu sana.
Na akiliweza hili lililowashinda watangulizi wake itakuwa regacy yake kubwa mno
 
Unataka kusema kwamba ili kukuza mji fulani solution ni kuhamishia makao makuu ya nchi huko? Kwani Dodoma imeshindikana nini kuendelea katika hali yake ya sasa? na vipi kuhusu Mbeya, Tabora, Songea, Musoma..zenyewe zitaendeleaje?

Kama ni suala la kupanuka kwa jiji la Dar near breaking point, kwa nini attention isihamishiwe katika kuendeleza miji yenye nafasi kibiashara?
Mji mkuu sijui mkoa mkuu wa Tanzania ni wapi/upi?
 
angefanya kimya kimya kwa kutamka pale suala hilo litamzeesha mapema sana na hivi watu wana imani naye sio kama yule mkwere msanii akifeli hilo litamuhathiri kisaikolojia,kuhamisha serikali sio kama kuhamisha kitanda toka chumba hiki kwenda chumba kile,nchi ina vimeo vingi sana ataacha lipi akamate lipi kwa miaka minne iliyobaki,fly over na daraja la coco beach vinamsubiri,viwanda sijui nini sijui
Ni kweli ana mambo lukuki kichwani lakini na hili ya kuhamia Dodoma ni muhimu sana..Kila miaka mitano inakua na mambo mengi sana kiasi kwamba asipoamua saivi yatamshinda kama yalivyowashinda watangulizi wake. Mkuu tukubaliane tu kwamba ni muhimu na priority kwa serikali kuhamia Dodoma na hakuna haja ya kuwa na visingizio hapo. Tumuunge mkono Raisi angalau kwenye hili
 
Ni kweli ana mambo lukuki kichwani lakini na hili ya kuhamia Dodoma ni muhimu sana..Kila miaka mitano inakua na mambo mengi sana kiasi kwamba asipoamua saivi yatamshinda kama yalivyowashinda watangulizi wake. Mkuu tukubaliane tu kwamba ni muhimu na priority kwa serikali kuhamia Dodoma na hakuna haja ya kuwa na visingizio hapo. Tumuunge mkono Raisi angalau kwenye hili
nakubaliana na wewe mkuu ila muda wa miaka minne serikali yote kuwa dodoma sijui ,hata mi ningependa ihamie kule kwa maslahi yangu binafsi
 
Kwa miaka yote hii ambapo Dar 'ilikuwa kama ndio capital city', miji ya Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe, Rufiji, etc ambayo ipo karibu na dar imeendelea kiasi gani? Mbona watu wanajibana pale pale Dar? Hapa suala ni upangiliaji. Kama watu wataruhusiwa kujianzishia vijimakazi vyao, Dodoma nayo itakuwa squatter kama Dar na hayo 'maendeleo' hayatafika Singida, achilia mbali Tabora.
Dar imewahi kua capital city lini mkuu?
 
Naunga mkono wazo la kuhamishia serikali Dodoma. Huko dar msongamano umezidi wacha watu wapungue kidogo angalau na viwanja vipande bei Dodoma.
 
Inasikitisha kwamba serikali bado ina ndoto za kufanya Dodoma iwe mji mkuu wa Tanzania kiutawala. Kusudi Dodoma iwe makao makuu inabidi serikali itumie hela nyingi kujenga majumba ya wizara mbalimbali, nyumba za watendaji, miundombinu n.k. Hiyo yote itagharimu hela nyingi ili kufanikisha azma ya kuhamia Dodoma.

Lakini kwa nini makao makuu ya serikali yahamie Dodoma? Kwani huko kuhamia kutaongeza ufanisi wa utendaji kazi serikalini? Si rahisi. Ukweli ni kwamba serikali itaongeza gharma za kujiendesha na kuongeza ufisadi kwa kiwango kikubwa tu.

Hili zoezi la kuhamia Dodoma lilianzishwa mwaka 1973, na mpaka leo ni wizara moja tu (TAMISEMI) ndiyo ipo Dodoma. Na hata hivyo watendaji wake wa juu muda mwingi wapo Dar es Salaam wakihudhuria vikao mbalimbali, wakiongezea serikali gharama - nauli, posho, mafuta ya magari, n.k..

Kwa sabau serikali tayari imeisha poteza pesa katika huu mradi wa kuhamia ni vema iachane nao, kusudi iokoe pesa zingine ambazo zitafanya shuguli zingine za kimaendeleo, k.m. ujenzi wa barabara, zahati, mashule, nyumba za walimu, n.k. Watanzania tuachane na tabia za kutumia au kuishi kupita uwezo wetu. Dhana kwamba Dodoma ikiwa katikati ya nchi huduma na maendeleo vitapatikana kwa urahisi na bei nafuu haina punje ya ukweli wowote.

Nchi nyingi tu duniani miji yao mikuu ya kiutawala au kiuchumi haiko katikati ya nchi hizo. Mifano michache itatosha kuonyesha upotofu wa dhana hii ya kuhamia Dodoma: Washington na New York ya Marekani, Moscow ya Urusi, Beijing Uchina, n.k. Tuachane na tabia ya kuteng'eneza ulaji kwa mafisadi.

Kuhamishia makao makuu Dodoma ni dhambi. Ni dhambi kwa sababu watanzania wengi wanapoteza haki zao za kupata huduma stahili toka serikalini, na wanaendelea kuteseka huku wachache wakiendelea kutafuna hela za walipakodi kwa visingizio vya kuhamia Dodoma.

Watanzania wote tupendao nchi yetu tukatae huu ufujaji wa pesa zetu.
Nigeria, Malawi na South Africa serikali hazipo miji ya biashara na maendeleo yapo na baadhi ya wizara na ofisi za balozi zipo miji ya zamani na huduma zinapatikana Kama kawaida, kubali ukatae jiji la Dsm limejaa watu maendeleo yanachelewa mikoani lazima serikali uhamie Dodoma isambaze maendeleo Kwa kasi kubwa .
 
Ni jambo la kheri sana kuhamia ddm ili kupeleka maendeleo huko.
Natamani hata iwe mwezi ujao.
 
Naunga mkono wazo la kuhamishia serikali Dodoma. Huko dar msongamano umezidi wacha watu wapungue kidogo angalau na viwanja vipande bei Dodoma.
Tanzania ni Nchi pekee Duniani wakuu wa wilaya,mikoa,wabunge , mawaziri , wakurugenzi nk ni wakazi wa jiji moja Dsm wanaenda kufanya kazi Kisha wakiwa rikizo wanaenda Dsm , Kwa style hii ni vigumu kupata maendeleo mikoani , lazima serikali uhamie Dodoma maendeleo yasambae kote .
 
Sawa, naongelea huko huko kuhamia maana imechukua miongo na miongo tangu maamuzi hayo yalipofikiwa enzi za mwalimu.
Kuna watu wanaleta utoto sijui Dar kuna bahar sijui starehe huu ni uzuzu
 
Ni jambo la kheri sana kuhamia ddm ili kupeleka maendeleo huko.
Natamani hata iwe mwezi ujao.
Serikali ikihama toka jijini foleni na misafara itakwisha Pesa za kupanua barabara nk zitatumika kuijenga Dodoma na kuleta maendeleo Nchi nzima , hii tabia ya Kila mtu kulundikana Dsm itapungua sana .
 
Dar imewahi kua capital city lini mkuu?
Nimeweka kwenye inverted comma, nadhani unaelewa maana yake. Kama haikuwa hivyo, kwa nini tunaongelea 'kuhamisha' serikali?
 
Kuna miji kama Manyoni kukua na kupanuka kutokana na kuwa karibu na mji mkuu.Biashara zitaongezeka.Hii ni faida.
 
Kuna watu wanaleta utoto sijui Dar kuna bahar sijui starehe huu ni uzuzu
Kule Darban South Africa na Mombasa Kenya kuna Bahari kuna Bahari na serikali hawapo huko na Johannesburg na Nairob ni majiji makubwa hayapo karibu na Bahari .
 
Kuna miji kama Manyoni kukua na kupanuka kutokana na kuwa karibu na mji mkuu.Biashara zitaongezeka.Hii ni faida.
 
Back
Top Bottom