Napinga kura za nje ya nchi

Napinga kura za nje ya nchi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Mimi si Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Lakini,kama mtanzania wa kawaida sana,nina haki za kutoa maoni juu ya jambo lolote lihusulo nchi yetu. Na leo,natumia haki yangu hii iliyopo chini ya Ibara ya 18 ya Katiba ya sasa kupinga kimaoni kuhusu Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kupiga kura wakiwa nje ya nchi. Ninazo sababu mbalimbali za kupinga kimaoni suala hili.

Mosi, utaratibu wa kupiga kura kwa namna hiyo haukuwahi kuwepo na wala haupo hapa nchini mwetu. Kuanzia Katiba, Sheria za Bunge na hata Sheria Ndogondogo,hakuna suala kama hilo. Kwakuwa Bunge Maalum la Katiba linasimamiwa na Katiba ya sasa, Sheria ya Bunge Sura ya 83/2011 na Kanuni zake, sivyema kuleta jambo jipya lisilotambulika hata na Katiba ya sasa.BL halina upekee wowote wa kishera na kimantiki.

Pili, Bunge Maalum la Katiba lisilazimishe akidi. Kama Wajumbe hawapo basi.Waliopo wapige kura. Hakuna haja kuwatafuta popote walipo ili tu kukamilisha akidi ya wapiga kura na ya wakupitisha Rasimu. Hakuna cha kuwahi wala kuchelewa. Katiba ni yetu wenyewe. Twende taratibu.

Tatu, wananchi watataka kuona na kusoma nyuso za Wajumbe siku ya kupiga kura. Kupigia 'kifichoni' hakutaleta picha nzuri. Napinga suala hilo.

Nne, kura za walio nje zina utata huu au ule. Mjumbe aweza kushawishiwa na alipo au aliye naye huko na kupiga kura kutokana na ushawishi huo. Pia,itakwa ngumu kujua wangapi wamepiga na wamepigia upande gani. Napinga suala hili.

Kimsingi, kura za Wajumbe watakaokuwa nje ya nchi zisiruhusiwe. Kwanini ziruhusiwe sasa tu?
 
Wapige kura wasipige kura bunge lote la katiba ni genge la wahuni tu walioamuwa kula kodi zetu.
 
Wasira: katiba haitengenezwi barabarani
Ukawa warudi BUNGENI
Pinda: tumewambia hawa wenzetu wa ukawa
Kuwa katiba haitengenezwi mabarabarani
Warudi BUNGENI
Sita :: mahali sahihi pa kutengeneza katiba
Kisheria ni hapa BUNGENI hawa ukawa
Wasiendelee kuwahadaa watanzania
Kauli nyingi Kama za Akina
Makonda na wengine zilitolewa kupinga
Ukawa wasijadili katiba nje ya bunge

Lakini Leo watu wale wale wamekuwa wa
Kwanza kula matapishi Yao wanataka
Katiba ipigiwe kura hata mabarabarani
Hawa Kama sio wehu na majambazi nini
Sheria zinapindishwa ziendane na matakwa Yao
Wakiona kuna mahali panawabana
Kesho wakutanikapo ni kubadilisha vifungu na
Kanuni Hali hii mpaka lini ? Mbona bado
Tuko utumwani ?
 
Kuna Wajumbe hawatakuwepo Bungeni kwakuwa wanapinga kinachoendelea pale indirectly.Hawapaswi kulazimishwa
 
Hoja yako ni yamsingi sana; hicho wanachotaka kufanya ni ukanjaja; lakini kwa kuwa sasa hakuna tena matarajio ya katiba mpya; tunawapa ilani kwamba hapo watakapomalizia kutunga katiba mpya ya CCM ndio hapo hapo harakati mpya za kudai katiba mpya na nchi yetu ya Tanganyika zitakapoanzia;

CCM mjiandae kwa harakati ngumu; ndefu na za hatari sana.
Aluta continua!
 
Mkuu Petro, kutokuwepo utaratibu fulani nchini hakumaanishi kuwa utaratibu kama huo haufai. Ni sisi ndio tunaotunga sheria/kanuni na taratibu zenu na kama hivyo ndivyo tunaweza kurekebisha na kuboresha kukidhi matakwa na mahitaji.

Mwenyekiti 6 yupo sahihi kabisa, hatuwezi kukwamsha zoezi ambalo kimsingi limefikia ukingoni.

Pia, kwa wale waliotoka nje ya bunge kwa kupinga kama ndugu zako Ukawa, kanuni hii mpya haitawalazimisha kupiga kura.

Jamani waacheni wabunge wengi popote pale walipo washiriki katka zoezi hili la kihistoria.

Katiba itapatikana
Vifungu vitapitishwa
Na wananchi watapiga kura ya ndio

Mtake ni hivyo, msitake ni hivyo.
 
Kuna Wajumbe hawatakuwepo Bungeni kwakuwa wanapinga kinachoendelea pale indirectly.Hawapaswi kulazimishwa

Mkuu Petro E. gari likigosa mwelekeo (BMK) barabarani haichagui pa kuangukia kwa hiyo nje ya nchi au ndani ya nchi isikusumbue, kazi iliobaki ni trafic (wananchi) kupima ajali na awasikilize majeruhi (ccm akina Kessy) kama dereva wao Sita alikuwa kalewa, au mwendo kasi ili afunguliwe mashitaki.
 
Mkuu Petro, kutokuwepo utaratibu fulani nchini hakumaanishi kuwa utaratibu kama huo haufai. Ni sisi ndio tunaotunga sheria/kanuni na taratibu zenu na kama hivyo ndivyo tunaweza kurekebisha na kuboresha kukidhi matakwa na mahitaji.

Mwenyekiti 6 yupo sahihi kabisa, hatuwezi kukwamsha zoezi ambalo kimsingi limefikia ukingoni.

Pia, kwa wale waliotoka nje ya bunge kwa kupinga kama ndugu zako Ukawa, kanuni hii mpya haitawalazimisha kupiga kura.

Jamani waacheni wabunge wengi popote pale walipo washiriki katka zoezi hili la kihistoria.

Katiba itapatikana
Vifungu vitapitishwa
Na wananchi watapiga kura ya ndio

Mtake ni hivyo, msitake ni hivyo.

Nimekupata Mkuu Tume ya Katiba.Lakini,kwanini sasa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Petro, kutokuwepo utaratibu fulani nchini hakumaanishi kuwa utaratibu kama huo haufai. Ni sisi ndio tunaotunga sheria/kanuni na taratibu zenu na kama hivyo ndivyo tunaweza kurekebisha na kuboresha kukidhi matakwa na mahitaji.

Mwenyekiti 6 yupo sahihi kabisa, hatuwezi kukwamsha zoezi ambalo kimsingi limefikia ukingoni.

Pia, kwa wale waliotoka nje ya bunge kwa kupinga kama ndugu zako Ukawa, kanuni hii mpya haitawalazimisha kupiga kura.

Jamani waacheni wabunge wengi popote pale walipo washiriki katka zoezi hili la kihistoria.

Katiba itapatikana
Vifungu vitapitishwa
Na wananchi watapiga kura ya ndio

Mtake ni hivyo, msitake ni hivyo.

Unaongea pumba aisee..! Yani mnataka watu wapigie kura katiba ya nchi wakiwa juu ya vifua vya watu? Au wengine wakiwa chooni wanakata gogo? Aisee jamani, this is too much....
 
Km ww ni mjumbe wa BMK ulikuwa Wapi kumpinga mkiti leo ASB? HATUTAKI UNAFIKI KAA KIMYA KATIBA TAYARI IMEPATIKANA.
 
Hujaelewa. Mimi si Mjumbe wa Bunge la Katiba. Usiwe na haraka wala shaka.Utapata tu buku saba yako
 
Mimi si Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Lakini,kama mtanzania wa kawaida sana,nina haki za kutoa maoni juu ya jambo lolote lihusulo nchi yetu. Na leo,natumia haki yangu hii iliyopo chini ya Ibara ya 18 ya Katiba ya sasa kupinga kimaoni kuhusu Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kupiga kura wakiwa nje ya nchi. Ninazo sababu mbalimbali za kupinga kimaoni suala hili.

Mosi, utaratibu wa kupiga kura kwa namna hiyo haukuwahi kuwepo na wala haupo hapa nchini mwetu. Kuanzia Katiba, Sheria za Bunge na hata Sheria Ndogondogo,hakuna suala kama hilo. Kwakuwa Bunge Maalum la Katiba linasimamiwa na Katiba ya sasa, Sheria ya Bunge Sura ya 83/2011 na Kanuni zake, sivyema kuleta jambo jipya lisilotambulika hata na Katiba ya sasa.BL halina upekee wowote wa kishera na kimantiki.

Pili, Bunge Maalum la Katiba lisilazimishe akidi. Kama Wajumbe hawapo basi.Waliopo wapige kura. Hakuna haja kuwatafuta popote walipo ili tu kukamilisha akidi ya wapiga kura na ya wakupitisha Rasimu. Hakuna cha kuwahi wala kuchelewa. Katiba ni yetu wenyewe. Twende taratibu.

Tatu, wananchi watataka kuona na kusoma nyuso za Wajumbe siku ya kupiga kura. Kupigia 'kifichoni' hakutaleta picha nzuri. Napinga suala hilo.

Nne, kura za walio nje zina utata huu au ule. Mjumbe aweza kushawishiwa na alipo au aliye naye huko na kupiga kura kutokana na ushawishi huo. Pia,itakwa ngumu kujua wangapi wamepiga na wamepigia upande gani. Napinga suala hili.

Kimsingi, kura za Wajumbe watakaokuwa nje ya nchi zisiruhusiwe. Kwanini ziruhusiwe sasa tu?

Mie upinge usipinge sina mpango wa kupiga kura bongo, ndiyo kwanza najipanga kuwa raia wa dunia.

Ila kesho msije kulalamika tu kwamba diaspora haina mchango bongo.

Ntakunanga "Baniani mbaya, kiatu chake dawa".
 
Mimi si Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Lakini,kama mtanzania wa kawaida sana,nina haki za kutoa maoni juu ya jambo lolote lihusulo nchi yetu. Na leo,natumia haki yangu hii iliyopo chini ya Ibara ya 18 ya Katiba ya sasa kupinga kimaoni kuhusu Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kupiga kura wakiwa nje ya nchi. Ninazo sababu mbalimbali za kupinga kimaoni suala hili.

Mosi, utaratibu wa kupiga kura kwa namna hiyo haukuwahi kuwepo na wala haupo hapa nchini mwetu. Kuanzia Katiba, Sheria za Bunge na hata Sheria Ndogondogo,hakuna suala kama hilo. Kwakuwa Bunge Maalum la Katiba linasimamiwa na Katiba ya sasa, Sheria ya Bunge Sura ya 83/2011 na Kanuni zake, sivyema kuleta jambo jipya lisilotambulika hata na Katiba ya sasa.BL halina upekee wowote wa kishera na kimantiki.

Pili, Bunge Maalum la Katiba lisilazimishe akidi. Kama Wajumbe hawapo basi.Waliopo wapige kura. Hakuna haja kuwatafuta popote walipo ili tu kukamilisha akidi ya wapiga kura na ya wakupitisha Rasimu. Hakuna cha kuwahi wala kuchelewa. Katiba ni yetu wenyewe. Twende taratibu.

Tatu, wananchi watataka kuona na kusoma nyuso za Wajumbe siku ya kupiga kura. Kupigia 'kifichoni' hakutaleta picha nzuri. Napinga suala hilo.

Nne, kura za walio nje zina utata huu au ule. Mjumbe aweza kushawishiwa na alipo au aliye naye huko na kupiga kura kutokana na ushawishi huo. Pia,itakwa ngumu kujua wangapi wamepiga na wamepigia upande gani. Napinga suala hili.

Kimsingi, kura za Wajumbe watakaokuwa nje ya nchi zisiruhusiwe. Kwanini ziruhusiwe sasa tu?

Huna ulicho andika cha maana zaidi ya utashi wa nafsi yako na sio utaifa. Yaonekana umeleta mada hii kwa kutumika zaidi
 
usipinge kura za wajumbe walio nje tu, pinga bunge lenyewe la katiba kwa sababu lishapoteza mwelekeo na haliwezi kutuletea katiba iliyo bora, kwanza uko ndani ya bunge au haupo?
 
Sipo na wala sijawahi kuwepo
 
Wasira: katiba haitengenezwi barabarani
Ukawa warudi BUNGENI
Pinda: tumewambia hawa wenzetu wa ukawa
Kuwa katiba haitengenezwi mabarabarani
Warudi BUNGENI
Sita :: mahali sahihi pa kutengeneza katiba
Kisheria ni hapa BUNGENI hawa ukawa
Wasiendelee kuwahadaa watanzania
Kauli nyingi Kama za Akina
Makonda na wengine zilitolewa kupinga
Ukawa wasijadili katiba nje ya bunge

Lakini Leo watu wale wale wamekuwa wa
Kwanza kula matapishi Yao wanataka
Katiba ipigiwe kura hata mabarabarani
Hawa Kama sio wehu na majambazi nini
Sheria zinapindishwa ziendane na matakwa Yao
Wakiona kuna mahali panawabana
Kesho wakutanikapo ni kubadilisha vifungu na
Kanuni Hali hii mpaka lini ? Mbona bado
Tuko utumwani ?

Sasa hivi ruksa katiba kutungiwa barabarani hahahahaa
 
Back
Top Bottom