kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,725
- 17,222
Kama tuna ushahidi kuwa miundombinu yetu na ya watu binafsi iliharibiwa kwenye vurugu za Oktoba 29 lazima walioiharibu na waliopanga uharibifu wakamatwe na kuadhibiwa mara moja ili iwe fundisho kwa wengine.
Yatakuwa makosa makubwa kama watu hawa wataachwa bila kuadhibiwa, itaacha kumbukumbu mbaya kwa taifa.
Kama serikali ikishindwa kuwachukulia hatua watu waliofanya makosa makubwa kama haya tutaiondoa madarakani kwa kushindwa kulinda kodi zetu ipasavyo.
Haifai kuendesha nchi. Nchi haiendeshwi kwa kutumia moyo na utashi, bali Katiba na sheria za nchi. Uchaguzi na namna unavyoendeshwa uko ndani ya katiba na sheria zetu ambazo viongozi waliapa kuilinda.
Hakuna mtu angeweza kuvunja Katiba kwa kufanya uchaguzi ulio nje ya Katiba hadi hapo Katiba nyingine itakapoandikwa na kupitishwa kutumika.
Hivyo, aliyetaka kusimamisha uchaguzi alikuwa anakwenda kinyume na katiba.
Kwanini serikali isiwachukulie hatua watu waliochoma vituo vya kupigia kura? Ndiyo kuilinda katiba huko?
Utafanye maridhiano na watu waliovunja Katiba (kuchoma vituo vya kupigia kura) na kuchoma mali za wananchi?
HUo ni woga au kushindwa kuongoza nchi? Wakati tunafanya maridhiano wale wote waliopanga na kutekeleza kuchoma vituo vya kupigia kura na mali nyingine lazima waende jela kwa mujibu ya sheria zetu.