Napendekeza tulimalize suala la bandari kwa kufanya yafuatayo

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,361
5,879
Kwa heshima na taadhima, napenda kuwashukuru wote mliochangia mijadala mbali mbali ya kuhusu ukodishwaji wa sehemu ya bandari kwa kuwa nyote mlikuwa na nia njema ya kujenga na kulinda rasilimali za taifa letu.
Lakini katika kutekeleza hili, kulionekana mapungufu mbali mbali kama yalivyo ainishwa na wadau mbali mbali.
La kwanza lilikuwa ni la ukomo wa mkataba. Ni kweli! Ukomo wa mkataba ni jambo muhimu sana; China waliwahi kuvikodisha visiwa vya Hong Kong ka muda wa miaka mia moja na walipo vihitaji, walishindwa kuvirejesha ikabidi wasubiri hadi miaka mia ipite hadi mnamo mwaka 2007 kama sikosei ndio wakafanikiwa kuvirejesha visiwa hivyo kwenye himaya yao kutoka kwenye mikono ya waingereza.

Mapungufu ya pili yalionekana kwenye aina ya mikataba iliyopendekezwa kusainiwa. Ni kweli! Haitakiwi mtu yeyote kusaini mikataba ya manunuzi isipokuwa ile tu iliyoandaliwa na mamlaka ya manunuzi yani PPRA.
Tatu, uhalali wa Dubai Port kufanya kazi nchini.
Uhalali wa kampuni kufanya kazi nchini huamuliwa na taasisi zenye mamlaka ya kutoa vibali na leseni za kufanya biashara nchini kama vile Brela, TIC nk.

Uhalali wa Dubai port kufanya kazi za bandari.

Uhalali wa Dubai Port kufanya kazi za bandari huamuliwa na kamati ya manunuzi ya bandari kwa kuzingatia evaluation ya technical, financial nk kama ambavyo muomba dhabuni atakavyojieleza kwenye nyaraka za zabuni.

Way forward

Iwapo TPA wanaona kuna uhitaji wa Dubai Port kutoa huduma za bandari, basi TPA wamualike Dubai Port kuwasilisha nyaraka za tender kupitia mchakato wa tenda za kutoka chanzo kimoja.
Dubai Port watatakiwa kijionesha kuwa wamekidhi vigezo vya kiufundi kama vile kuwa na winchi za kutosha kupakulia mizigo, utaalamu wa wataalamu waliokidhi vigezo hivyo nk.
Upande wa kifedha, Dubai port watatakiwa kujionesha kwa TPA kuwa wamekidhi vigezo vya kutosha kifedha kwa kuwa na mtaji wa kutosha kutoa huduma bandarini na frame work ya gharama za kufanya shughuli za bandari.

Nyaraka za tender zimeshaandaliwa na PPRA kama jnavyoonekana kwenye website yao

Screenshot_20230628-115002.jpg


Dubai Port watatakiwa kupitishwa kwenye mchakato wa tenda ya chanzo kimoja (single source) ambapo watatakiwa kulipa ada za kushiriki kwenye mchakato wa tenda ambazo huwa ni USD 100 kwa kampuni za kigeni.
Baada ya kuwasilisha vitabu vyao vya tenda, kamati ya tenda ya TPA wataifungua tenda siku iliyopangwa mbele ya washiriki na waandishi wa habari na baada ya hapo, kamati ya manunuzi itafanya evaluation.
Iwapo Dubai Port watakuwa wamekidhi vigezo vilivyo ainishwa na TPA, wataambiwa wakidhi baadhi ya mashariti kama vile kuleta performance bond nk.
Baada ya hapo Dubai Port sasa wataweza kupewa mkataba wenye ukomo wa miaka kumi ambao utaweza kuongeza iwapo walionesha utendaji wenye kuridhisha katika miaka kumi ya mwanzo.
Nawatakieni wote utekelezaji mwema wa majukumu yenu ya kila siku. Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom