Napendekeza TISS ivunjwe, iundwe Upya

Napendekeza TISS ivunjwe, iundwe Upya

Hii Taasisi ilikuwa imara sana enzi za mwalimu Nyerere na mwisho kabisa kwa Mkapa,baada ya hapo imekuwa Taasisi ya kisiasa.

Inafanya kazi kwa maslahi ya wanasiasa na siyo Taifa na ndiyo sababu hali ya maisha ya watu inazidi kuwa mgumu kila siku iitwayo leo.

Kazi kubwa ya TISS ni kulinda usalama wa nchi kiuchumi na mipaka yake, hii Taasisi inayohitaji watu wanaoipenda nchi yao kwa Dhati, yaani Wazalendo kweli kweli na siyo makada wa UVCCM.

Siku hizi mtu akiwa kada mwaminifu wa Chama anapewa kazi TISS.

Ndo maana yameibuka magenge mengi mno yanayohujumu Uchumi wa Tanzania kuanzia mitandaoni hadi mitaani.

TISS ivunjwe, iundwe upya.
Kwa hili hata sijiulizi mara 2, naunga mkono hoja.
 
Sasa nani kakwambia NCHI HAIKO SALAMA?
 
Waanze kuvunja wapi sasa?
Kwamba wavunje vuup?
Halafu kitokee nini?
Mizizi yote mpaka washona viatu waganga wauza kahawa wote wavunjwe?

Halafu hao wapya waanzie wapi kupata habari? Nani awafunze hao wapya.
Wakati hao wapya wakiwa mafunzo shughuli zao nani atazisimamia?.
Umeuliza vitu vya kufikirisha sana mkuu. Ni kweli kabla ya kuivunja taasisi kama hii ni muhimu kujiuliza hayo mambo ili kupata mwendelezo wa kazi za kitaasisi.

Ila nadhan wafanye kama 1964 ambapo jeshi la Tanganyika rifles lilivunjwa na kuundwa JWTZ.
 
Mi naona ingebadilishwa jina ikapewa jina la kijanja kama vile wenzetu.Wao wana majina ya kijanza zaidi utasikia MI 6,MI 5 n.k
Labda na sisi ingekuwa Tz 61, Department 7.N.k
 
Logically hata ikivunjwa, ikaundwa upya watendaji wake bado watakuwa walewale.
 
Back
Top Bottom