Napendekeza serikali ihamie Arusha badala ya Dodoma

Napendekeza serikali ihamie Arusha badala ya Dodoma

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,814
Reaction score
46,936
Kwa sababu zifuatazo:

1.) Ipo karibu na vivutio vingi sana, hivyo tutakuwa tumekuza utalii wa ndani kwa kiasi kikubwa sana, ukizingatia utalii unaongoza kuliingizia taifa mapato ya kigeni na tukiongeza ya ndani itakuwa safi sana, pia watalii watatua Arusha moja kwa Moja badala ya kupitia Jomo Kenyatta na kilala mahoteli ya huko.

2.) Ipo karibu na Kenya na hivyo itakuwa rahisi kujiambukiza maendeleo kutoka Kenya ikiwemo Teknolojia na ustaarabu wa kimaendeleo, pia tutalikamata solo la Kenya kwa ustadi mkubwa zaidi na hivyo kukuza uchumi.

3.) Tatu Arusha ipo tayari zaidi kirasilimali watu na kimiundombinu kuweza kuipokea serikali bila ukakasi wowote ule ukilinganisha na Dodoma.

4.).........5.).........
 
Number mbili kweeli?????
Come on wakenya wana technology gani ya kutupa watanzania jamani??

Mpaka saivi Tanzania ndio inaongoza kuuza bidhaa Kenya zaidi yao kwa Tanzania.

Watalii wengi wanalala Arusha mpaka muda huu ninazo taarifa kwenye makarabrasha yangu zaidi ya hotels 5 za five stars zipo under construction Arusha achilia mbali mahotel yaliyopo na yaliyo kwenye pipeline.
 
Watalii kulala Arusha wenyeji wanajua namna unavyoweza kupiga virgin money kwa blind lodges ni Arusha pekee mtu unageuza nyumba yako na kuwa lodge bila hata kuhama na ukapiga pesa.
 
nani apeleke nchi Arusha kule hakufai kabisa aisee...bora nchi ipelekwe singida kuliko arusha, kule wamejaa watu wenye roho mbaya kinyama, wakatili na wabinafsi sana...acha tu iendelee kuwa sehemu ya wazungu kushangaa ngedere
 
Ni sawa kwa kuwa ndio sehemu yenye hali ya hewa nzuri sana hata wageni wengi wanakupenda.
 
Ningependa kujuzwa ni kwa nini miaka yote kulikuwa na vugu vugu la serikali kuhamia dodoma na si mkoa mwingine..nikahisi dodoma ipo katikati ya Tanzania lakini kuna singida pia au kwa kuwa ni mji mkuu, lakini mbona makao yalikuwa dar hapo awali....kwa maoni yangu, na kwa kuwa sioni vigezo vya dodoma ningependa makao ya serikali yahamie mkoani MARA kwa sababu moja kuu...Ulinzi ni wa kuaminika kiasi kwamba idadi ya polisi inazdi ya raia hasa tarime na rorya.
 
Mkuu Kwanza Dodoma ni makao makuu ya nchi ndio maana kuliwekwa ikulu ndogo kule na kuhusu serikali kuwepo Dar ni kwa sababu mji uliendelezwa zamani na wakoloni na serikali ikaona bora ijipange kwanza kabla ya kuamua rasmi kwenda DOM na pia uhuru wa nchi ulitangzaziwa DSM kama sijakosea.
Huo ni mtazamo wangu pia katika kutoa maoni kulingana na uzi husika
 
Aisee
nani apeleke nchi Arusha kule hakufai kabisa aisee...bora nchi ipelekwe singida kuliko arusha, kule wamejaa watu wenye roho mbaya kinyama, wakatili na wabinafsi sana...acha tu iendelee kuwa sehemu ya wazungu kushangaa ngedere[/QUOTE AISEE CHALI ANGU MBONA UNATUPONDA KIIVYO SIO POWA
 
Nadhani inawachanganya kati ya mji mkuu wa Tanzania na makao makuu ya chama na serikali....
 
Tunahamia ambako wananch hawajaelimika tukawatawale milele..hehee
 
Back
Top Bottom