Napenda kupiga push up

eneo nalokaa halina mlima alafu saa 11 kuamka kukimbia naona msala,kingine kamba mikono inakaza naogopa kukomaa

na upunguze ubishi…..fanya mazoezi kama unavyoshauriwa…..mwishoniutaogopa hata kugegeda eti kiuno kinauma sana? shieee
 
mpenzi wangu yuko mbali so hizo hints ni nzuri lakini hazijatua sehemu husika,asante
Si lazima iwe na mpenzi wako....la muhimu ni work out uwe fit au sio?km ndio u can try me..teh teh the..
 
Ndiyo umetoa maelezo ya mazoezi yako lakini kupata ushauri ulio bora na manufaa kwako ni lazima vitu vifuatavyo vizingatiwe:

1.Kitu cha kwanza ni afya yako,hii ni pamoja na magonjwa yoyote hatarishi ikiwemo MOYO WAKO.

2.Uzito wako ni muhimu sana katika kuchagua ni zoezi lipi uanze nalo na siyo bora zoezi ilimradi utoke jasho.Ni muhimu kuwa na mzani nyumbani kabla ya kuanza mazoezi ili kujua umeanza mazoezi ukiwa na kilo ngapi,pia itakusaidia kujua unapungua au unaongeza kilo wakati wa mazoezi.

3.Chakula gani unachokula katika mzunguko wako wa kila siku. Hili litakuasaidia katika kupunguza kilo za mwili au kuongeza kilo za mwili kwa wale wanaotaka kuongeza.

4.Unywaji wa vimiminika visivyo na kileo ni muhimu sana kwa yeyote anaeanza mazoezi.Hapa naongelea MAJI NA JUICE fresh za matunda.Maji husaidia sasa tena sana wafanya mazoezi katika kulileta jasho.Wiki ya kwanza inakua ngumu kunywa maji kwa kiwango cha juu lakini kadili utavyoendelea utaona kiwango kinaongezeka taratibu. Maji ya uvuguvugu pia yanasaidia kuleta jasho kwa haraka lakini pia yanaweza kukupeleka katika mlolongo mwingine tofauti na mazoezi yako.

5.Tambua mazoezi yanayofanywa na wanawake au wanaume wengi katika kujenga sehemu muhimu za miili yao. Mfano,wanawake walio wengi wanajenga sehemu za miguu,mabega,mapaja,makalio na shingo huu ni kwa uzoefu wangu. Sasa wewe unataka kutengeneza nini hasa? Hili ndiyo liwe swali lako la msingi

6.Tambua zoezi la kuanza. Hata nyumba huanzwa kwa kujengwa msingi na iwapo msingi ukiwa legelege madhara yake ni makubwa. Ni muhimu kuiandaa miili yetu kwa tukio lijalo mbele.Mfano kama unajijua wewe unataka kuanza kupiga push up lazima uanze kukimbia iwe nje au ndani angalau kwa siku 7. Hili litakusaidia kuzistua hizo nyama zilizolala usingizi coz ukikimbia mikono inafanya kazi,miguu,akili,bila kusahau macho nayo yanapepesa huku na huku kuangalia hatari yoyote. Kwa wale wanaojiweza ndiyo hao wanajinunulia machine kama hizo treadmill,baiskeli za ndani zile kama za gym n.k.

7.Tambau unataka kua kama nani.Nani umevutiwa naye kiasi kwamba uanataka kuanza mazoezi kuwa fit kama yeye. Pengine ni mcheza sinema,mwanamieleka,mwanamuziki au hata jirani yako nyumbani au kazini. Nimesema hivi kwasababu umejitambua hauko fit so unataka kuwa fit. Mfano ukienda sehemu zenye gym utakuta picha za wanyanyua vitu vizito ukutani walio maarufu duniani. Hata watoto wadodo siku hizi vyumba vyao utakuta vina picha za Superman,Spiderman,Scooby doo au tom n jerry n.k. Hizi picha zinawasaidia sana wahusika kuwapa msukumo fulani.

8.Elewa kwamba katika kufanya mazoezi yanayohusu mwili wakati wote yanakua na matokeo ya aina mbili. Moja ni kuongeza uzito na pili ni kupunguza uzito. Hivi hutokea pasipo wewe kujitambau na kulingana na aina ya mazoezi. Kupiga push up kwa asilimia kubwa utaongeza uzito,kuruka kamba kutakufanya upunguze uzito kwa urahisi huku ukijengeka misuri ya miguu na mabega bila kusaha mgongo wako utakua kakamavu sana.

Achana na push up zitakutanua mabega bure,mwanamke anatakiwa apige lile punching bag kwa ajili ya ufit wa mikono,so tafuta kiroba weka machanga anza tizi.Mchanga bure, kiloba bure sasa wewe nunua pro gloves tu kama zile za mabondia.

Pia kwa ajili ya miguu nenda tafuta tairi la motokaa lilokwisha tumika saizi yoyote kulingana na uzito wako. Akikisha unapata lililo na resistance sawa na uzito wako utakapo likanyaga. Siyo wewe una kilo 90 ukachukua tairi ya bodaboda.Pia kama unajiweza tafuta kifaa fulani kipo kama ngazi (stepper) hivi ambacho unaweza ukawa unakikanyaga huku umeshikilia ukuta au sehemu yoyote ili usianguke. Hiki kitajenga mguu na makalio na jasho unalolitafuta litakutoka,kifaa hiki hakitumii umeme na ni rahisi kukihifadhi coz kiko kama kilo 5 max.

Pia unaweza nunua baiskeli za ndani zisizotumia umeme,ila pia itategemea unanafasi kiasi gani unapoishi. Na usisahau hizi baiskeli zinakawaida ya kuongeza makalio na kuyafanya kuwa na umbo nzuri bila kusahau sehemu za mapaja. Pia kwa walio na matatizo ya mgongo au kushindwa kusimama kwa muda mrefu hii ni kiboko yake.

Kumbuka mafanikio ya mazoezi yako huja kutokana na mazingira unayoishi ,pamoja na msukumo ulionao muhusika hasa katika kufuatiria ratiba yako ya mazoezi na kutokuishia katikati uwapo mazoezini.

kila lakheri
 
Tafuta/download dancing exercise program, then kila ukitaka kufanya mazoezi unaplay on tv afu unawaiga step to step, itasaidia kupingua uniformly bila kutoka viazi or kuwa kama John Cena:thumbup:😎
 

asante sana mkuuu aisee hiyo ngazii inakuaje,ila naona baiskeli nayo nzuri na huo mchanga na kiroba inasaidia nini mikono?
 
Tafuta/download dancing exercise program, then kila ukitaka kufanya mazoezi unaplay on tv afu unawaiga step to step, itasaidia kupingua uniformly bila kutoka viazi or kuwa kama John Cena:thumbup:😎

thanx mmkuuu
 
 

Achana na push up zitakutanua mabega bure,mwanamke anatakiwa apige lile punching bag kwa ajili ya ufit wa mikono,so tafuta kiroba weka machanga anza tizi.Mchanga bure, kiloba bure sasa wewe nunua pro gloves tu kama zile za mabondia.
Mkuu asante sana kwa darasa, ila naona hapo juu sidhani kama ataweza kwa jinsi alivyojielezea jana. Mleta mada anataka mazoezi mepesi.

Pamoja
 
Mkuu asante sana kwa darasa, ila naona hapo juu sidhani kama ataweza kwa jinsi alivyojielezea jana. Mleta mada anataka mazoezi mepesi.

Pamoja

Yeah man uko sawa. Nimefatilia uzi wake tangu mwanzo ikiwa ni pamoja na michango ya watu humu lakini nikaona imekaa vibaya. Ila nilichofanya ni kupiga moyo konde kwa manufaa yetu wote nikaamua kuja na hizo bunduki.

Hii itawasaidia wengi hasa beginners na wazoefu kujifunza machache,tatizo la wadada walio wengi ni waoga na wakati mwingi wanazani kufanya mazoezi ni kujikomaza au kujiumiza. Pia Tanzania hatuna wataalamu wa kutosha wa kuelimisha masuala ya mazoezi na utumiaji wa vifaa mbadala wa vile vya wenzetu.
 
Mkuu asante sana kwa darasa, ila naona hapo juu sidhani kama ataweza kwa jinsi alivyojielezea jana. Mleta mada anataka mazoezi mepesi.

Pamoja

haaha HARUFU nisije nikakomaa kuliko baibe
 
Sasa kama limeuma usiache, badae piga mbili ongeza ongeza tu idadi, kifua pembeni kdogo karibu na kwenye joints na mabega kutauma bcoz of pushups ila kutazoea soon hutosikia maumivu, maumivu yataacha, ila usiache kupiga walau mbili kwa siku, tatu, siku zinavozidi kwenda utazidi zoea na utazidi enjoy.
Halafu huko viwanjani wanapocheza boli si unakuwa unakimbia pembezoni tu,
Au unaona soo utatazamwa, we vaa zako earphones kimbia round tano au zaidi utavoweza kuhimili, rudi kwako,
Mazoez yana faida kibao usiache
 
Asante sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…