Napenda kujua zaidi kuhusu Kilimo cha minazi (coconut tree)

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,208
18,476
Habari wa ndugu,

Napenda kupata maarifa zaidi kwenye ulimaji wa minazi, hasa kibiashara.
1. Wapi napata mbegu nzuri za kisasa
2. Utayarishaji shamba?
3. Muda gani wa kupanda, na namna gani nzuri.
4. Kwa ekari moja inaapendekezwa miti mingapi?

Na habari nyingine muhimu.

karibuni
 
TAARIFA MUHIMU 🔥🔥Miche ipo tayari weka oder yako mapema hii, miche hii hichukua miaka mitatu tu kubeba matunda na inasambazwa nchi nzima.
.
Ekari moja huingia miche 100-120
.
Inabumilia ukame na kukupa matokeo bora zaidi (hufanya vizuri katika hali nyingi za hewa nchini)
.
Wahi sasa 🥥🥥🥥
.
Muongozo wa upandaji unatolewa bure kabisa. +255 759 499 196 whatsapp
.
Bei ya mche 15000/=

Wacheki hao watakusaidia kwenye kilimo cha minazi
 
Minazi original haswaa inazaa after 5yrs
Zenji zililetwa mbegu wakasema ooo hii ni minazi mifupi na inazaa kwa muda mchache hatimae minazi ile imebaki kua historia haina kuzaa wala nn

Ukitaka ushahidi ulizia eneo kma unaenda kizimbani chuo cha kilimo utaoneshwa hiyo minazi

Usikurupuke mkuu katika kuchagua mbegu za minazi ila ni kilimo chenye tija sana baadae
 
..kwa hiyo hadithi za minazi mifupi ya Kipemba ni uzushi?

..nilifikiri minazi ya huku Tanganyika ni tofauti na minazi inayopandwa Pemba?
 
mnazi ni lulu shambani
kwanza utapata nazi
pili pombe ya mnazi
tatu makuti
nne mafagio ya chelewa
tano mbao
sita kivuli
saba malighafi za mikeka na mapambo
nafikiri faida ni nyingi sana
 
Vipi kwa mkoa wa Tabora inastawi
Huko Tabora panda chikichi mzee....utapata hasara ukipanda minazi. Yupo jamaa yangu alijaribu maeneo ya Kalunde karibu na JKT barabara ya Ulyankulu...yote ilikauka because of tough weather. Usidanganyike kuona minazi majumbani ndiyo ukaamua kuilima...!
 
Eneo langu lina mbuga kiasi,na itapandwa mvua za kwanza kabisa za Oktoba.
 
TAARIFA MUHIMU 🔥🔥Miche ipo tayari weka oder yako mapema hii, miche hii hichukua miaka mitatu tu kubeba matunda na inasambazwa nchi nzima.
.
Ekari moja huingia miche 100-120
.
Inabumilia ukame na kukupa matokeo bora zaidi (hufanya vizuri katika hali nyingi za hewa nchini)
.
Wahi sasa 🥥🥥🥥
.
Muongozo wa upandaji unatolewa bure kabisa. +255 759 499 196 whatsapp
.
Bei ya mche 15000/=

Wacheki hao watakusaidia kwenye kilimo cha minazi
Mkuu ekari moja miche 100-120 kwa spacing ipi? Kimataifa minazi mirefu ni meta 10 kati ya mche na mche na minazi mifupi ni meta 7 kati ya mche na mche. Kwa wastani ekari moja ni miche 70 hadi 80.
 
Huko Tabora panda chikichi mzee....utapata hasara ukipanda minazi. Yupo jamaa yangu alijaribu maeneo ya Kalunde karibu na JKT barabara ya Ulyankulu...yote ilikauka because of tough weather. Usidanganyike kuona minazi majumbani ndiyo ukaamua kuilima...!
Nimezaliwa Tabora na kukulia kule. Miaka hiyo kulikuwa na minazi kibao tena yenye kuzaa nazi nyingi. Tabora minazi inakubali ila hakuna wenye mwamko wa kuipanda. Mingi ilipandwa na Waarabu na ilishajifia kama ilivyo kwa miembe.
 
Mkuu ekari moja miche 100-120 kwa spacing ipi? Kimataifa minazi mirefu ni meta 10 kati ya mche na mche na minazi mifupi ni meta 7 kati ya mche na mche. Kwa wastani ekari moja ni miche 70 hadi 80.

..Je, ukiwa na chanzo cha uhakika cha maji kwa ajili ya umwagiliaji unaweza kuipanda karibu zaidi?
 
Minazi haihitaji maji mengi. Ukiipanda masika na ikishika vizuri inakuwa vizuri tu unless utokee ukame usio wa kawaida.
 
Minazi haihitaji maji mengi. Ukiipanda masika na ikishika vizuri inakuwa vizuri tu unless utokee ukame usio wa kawaida. Huwezi kuipanda minazi karibu karibu haitakiwi. Kwa ufupi panda kwa umbali ambao makuti hayatagusana yaani meta 10 kati ya shina na shina.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom