Napenda kujua kwanini mume na mke wakiishi pamoja muda mrefu wanafanana?

Ata watoto mara nyingi wanafanana na mama zao coz wanakaa na mama muda mrefu.. So kama baba unataka fanana na mwanao jaribu kuwa karibu naye..
 
486911d0f20a2091391472b5ea2840c7.jpg
Check na hawa wanavyofanana
 
Najaribu kufikiri miaka mingi baadae Beyonce afanane na Jay Z au Jay Z afanane na Beyonce.

Huwa hawafanani, ila ukizoea kuwaona pamoja kwa muda mrefu ukimuona huyu unnapata na taswira ya yule mwingine.
 
Ni kweli nakuunga mkono mtoa mada,jambo hili husababishwa na kula vyakula vinavyofanana pamoja na kushabihiana kwa tabia na kutumia baadhi ya v2 vinavyofanana kama vile mafuta ya kujipaka na hata maji
 
aaahh kumbe hata kama marafiki wakikaa mda mrefu wanafanana bas tusimlaumu sana harmonize kwa kufanana kila kitu na diamond
 
Kufanana kunakosemwa labda ni kwa hali ya afya.
Mume akiwa duni na mke anadhoofika kwa ukata.
Ukiwa tajiri unanawili mke ananawiri.
Kama mnakaribisha mazungira ya uchafu wote mnakuwa wachafu.

Labda hivyo.
 
Nimekuwa nifuatilia watu wanaishi kama mke na mme na mara nyingi ukiwaangalia wanafanana kama mtu na dada yake.Je nini inasababisha naomba kujuzwa
Vinasaba vinaungana in nature na kusababisha watu kufanana.kisayansi huwezi kuipata ila ktk imani na mambo ya rohoni
Nimewaza kwa sauti
 
Jamii imeshajengeka kisaikolojia kuwa jane mumewe ni John hivyo kila mtu akimuona Jane anatengeneza mfananisho wa kisaikolojia. Pia watu wanakaa pamoja mke na mume kuna mambo mengi ikiwemo tabia wanafanana na mambo ya saikolojia.pia kumbuka kuhusu maumbo watu wengi wanapenda watu wa maumbo yao kama mke mfupi mume mfupi,
 
Back
Top Bottom