Wakuu unajua Nape anasemwa sana kama ni gamba lisilojitambua. Lakini kwa hakika Nape ni aina ya wanasiasa wasiopenda kufanya siasa za uvunjifu wa amani. Anachukizwa sana na siasa zonazofanywa na Mh. Mwigulu Lameck Nchemba. Ndio maana ameamua kukaa kimya amuache bwana Nchemba na timu yake wafanye hizo aina zao za siasa.
kiroba:
Kwa sehemu nakubaliana na wewe na kwa sehemu sikubaliani.
Nnape huyu huyu ndiye aliyewaambia Watanzania kuwa CHADEMA WAMEJILIPUA wenyewe baada ya mlipuko wa Bomu na kuua watu 4 kwenye mkutano wa CDM pale Soweto.
Nnepi,Mchembe na Wassira huwezi kuwatenganisha katika mikakati na njama za kuihujumu CHADEMA. Kwa hiyo ukimya wa Nepi usije ukafikiri kwamba hapendi siasa za vurugu!
Kwa mtazamo wangu mie ni kwamba baada ya matokeo ya Udiwani katika kata 4 za Arusha mjini na CCM kushindwa vibaya hawa jamaa kina Nepi na Mchembe wamepatwa na ganzi kabsaa. Ukimya wao huu ni AIBU kubwa iliyowapata baada ya matokeo hayo. Kwa kweli inavoonekana kwa sasa hawa jamaa na CCM yao wanatafakari watasema uongo gani kwa sasa baada ya matokeo ya udiwani kuwavua nguo!
Yawezekana kabisa kwasasa Nepi na Mchembe wamekalia kuti kavu ndani ya CCM baada ya kuonekana kwamba mbinu wanazotumia kuichafua CHADEMA na kujaribu kushinda chaguzi ndogo mbalimbali zimeanza kupoteza mwelekeo na hata hao mabosi wao Kiwete,Kinana na Mangula wana wasiwasi sana na hawawaamini tena!
Juzi tumesikia kuhusu BIFU lililopo kati ya Mwigulu Mchembe na Nepi Nauye kwamba Mchembe kafanya njama za kumdhalilisha Nepi kwa kumtega na jimama kwenye hoteli moja huko jijini Dar na kupiga picha za utupu wakila uroda Nepi na hilo Jimama na picha hizo anazo Mwigulu Nchemba! Kwa hiyo inaonyesha kwamba tayari hawa wawili hawaelewani na tayarei wamehsaanza kufitinishana ili aidha mmoja wao ahame chama au apelekwe Mabwepande!J
JK Nyerere(RIP) alisema kuwa ukishaanza dhambi ya Ubaguzi haitakuacha. Itakutafuna mpaka siku ya mwisho. Kwa hiyo hawa CCM walianza na kubagua wapinzani ili kuwachafua lakini tayari hiyo dhambi imeshaingia kwao na imeanza kuwatafuna. Mimi nasema na iwatafune kwelikweli mpaka washike adabu zao!
Acha iwatafune maana tumechoka!