Nape kwa asili ni mtu mwenye mizaha, tabia hii imemsaidia kwingi lakini pia imemuumiza katika mambo mengi. Sio mara ya kwanza kwa Nape kutoa kauli zenye utata kuhusu ushindi wa CCM dhidi ya Upinzani Tanzania. Mwaka 2015 aliwahi kutamka kuwa CCM itashinda hata kwa bao la mkono. Mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu tulishuhudia waziwazi bao la mkono maana yake ni nini.
Wiki iliyopita Nape akiwa mkoani Kagera alisikika na kunukuliwa vizuri na media akisema; ushindi katika uchaguzi hutegemea nani anahesabu kura na pia nani anatangaza matokeo. Kumbe mpinzani anaweza kushinda lakini kura zake za ushindi zisihesabiwe akashinda mwingine asiyechaguliwa na wananchi. Au mpinzani akapata kura za ushindi lakini akatangazwa mtu mwingine kuwa ni mshindi.
Mpaka sasa maneno ya Nape yamesababisha viongozi wengine hata wasio wa kisiasa kuondolewa madarakani kutokana na kuonekana kumshukuru Nape kwa utendaji wake wakati akiwa waziri wa Habari na Mawasiliano.
Kosa la Nape ni kuusema ukweli wa chaguzi za Tanzania. Nape ameweka wazi kabisa yanayotendeka nyuma ya pazia katika chaguzi zetu. Mamlaka zilipaswa kuchunguza hoja za Nape na kujirekebisha kuliko kumwondoa tu katika nafasi yake.
Nape amewakosea wenye mamlaka (CCM) na serikali yake lakini amesema ukweli ambao Wananchi tunapenda kuujua.
Pia soma