Thanks mkuu kwa kutuweka sawa katika hili. Mimi nafikiri wana JF wengi humu ndani wanapenda kujenga hoja kwa kufuata mkumbo tu. Kwa kuwa magazeti yamesema fulani mbaya, basi kila mtu anadakia tu na kuunga kukubaliana bila kufanya uchunguzi. Kwa jinsi ambavyo nimesoma mfululizo wa posts humu nimegundua kabisa Msema hovyo si wa hovyo kama anavyojiita. Huyu jamaa anajenga hoja na anaweza kuitetea. Na kile alichokidai hadi sasa hakuna aliyeweza kukileta (ushahidi wa ufisadi wa Lowassa). watu wamebaki kumbeza na kumdharau, lakini ukweli utabaki palepale, Lowassa ni kiongozi super. Na hizo hoja za ufisadi zina chimbuko ambalo CCM na hasa JK ndiye anayelijua. Lakini uzuri matokeo ya ubaya hulipwa hapa hapa duniani. Majonzi ya Lowassa naamini yatasikika mbele za Mungu.1990-akiwa chief whip na disaster under pmo- aliondoa urasimu wa usafiri kwa wabunge, ndie alieasisi wabunge kukopeshwa magari-walianza na shangingi zile tzc....., ktk majanga kijana alikuwa nyota kila linapotokea alifika na suluhisho ndipo akaingia matatizoni na wenye hamu ya kumrithi mwinyi-akaondolewa pale kwa mzee malecela na kupelekwa ardhi......ndie aliewahimiza wananchi kutwaa mabati uwanja wa mnazi mmoja baada kuwepo kwa ujanja wa kubinafsisha viwanja vile.......taratibu watz walianza kumtambua ni nani huyu edward ngoyai lowasa....ktk michakato hii ndani ya zama za ruksa lazima kulikuwepo dosari ambazo aidha ziliwanufaisha baadhi ya watu au kuwaumiza baadhi ya watu...., tangu awali hakuwa tayari kuukubali umaskini wetu hivyo akawa highly spirited kujijengea nguvu za uchumi, nakumbuka rai likiwa chini ya jenerali twaha ulimwengu walimshamtoa front page 1995 "ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke......" by then nilikuwa mvulana mdogo sana lakini ninakiri kuwa licha ya ukwasi wake alikuwa my nambari wani kwa warithi wa mzee alhaj mwinyi na siyo vinginevyo....., 1995-07 alitoswa na mkapa na sababu wanazijua uvccm ya guninita ingawa mnataka sana hapa ndani tuamini ni mwal. Nyerere ndie aliemkataa....la hasha! Ilikuwa ni kazi ya rais mwenyewe ktk kuijenga nchi na chama kimoja na kuwa tayari kukubali matokeo na maamuzi ya chama..... Edward lowassa was dumped just because alikuwa true friend wa jakaya na alimaini 1995 ilikuwa zama ya uvccm kuitwaa nchi kitu ambacho mwalimu alikipinga kwa kumptisha mzee benjamin mkapa by then 56. Ni edward lowassa na ndg yangu na kaka yangu jj.guninita(shikambaku) walioweka wazi kuwa ccm imeidhulumu uvccm kwa kumpitisha bw mkapa......., lowassa alitolewa ktk gazeti la uhuru akiwa amekaa chini analia na tai yake ikiwa lose just because of jakaya candidacy......., ile image haikuwa nzuri kwa ccm, na hata jk aliposema kambi yake imevunjwa na inamuunga mkono mzee wetu mkapa wao wote hawakuwa wakweli ila ni hao wawili walishindwa kuwa wanafiki (lowassa na guninita), system ilijua na chama kilifahamu wakaadhibiwa, uwaziri ukamkosa lowassa licha ya ya mzee mwinyi kumsihi sana mkapa baada ya kuteuliwa mbele ya ccm -gm 1995 , "nakuomba usiwatupe ndg.lowasa na jndg.Kikwete, ni vijana wangu waaminifu na wachapa kazi, watakusaidia" tafuteni video ile ya kizota 1995. Ni jakaya tu alirudi novemba 1995, guninita pia alipoteza ukuu wa wilaya ya kigoma na hatimae alikimbilia chadema.......,
regime ya mkapa 1997-2005: Mazingira alifanya kazi tukufu.....maji :alipafanya pasikike na paheshimike na 2005-2008 under Jakaya aliimarisha zaidi nuru ya serikali na watumishi kuheshimu mamlaka na kuwajibika........, sidhani kama dhambi zake zitaishinda nuru yake na ule utamaduni wake wa kupenda kuwa mbali na unafiki......Edward Lowassa si mnafiki, ni rafiki wa ukweli na yuko tayari kuwajibika kwa gharama yake na taasisi anayoisimamia,kazi kwenu na tumhukumu kwa ukweli na si majungu...........

Kwanza kabisa nakupongeza Msema ovyo kwa swali makini ambalo ni watu ''makini'' tu ndiyo wanauwezo wa kuuliza swali makini kama hili. Nape amekurupuka na hajui siasa, baada ya kupewa cheo hicho alisahau kabisa kuwa mwaka jana alikuwa mtu aliyetupwa jalalani akakataliwa kabisa na wana ccm kiasi cha kunyimwa nafasi ya kugombea nafasi ya ubunge ubungo. Huyu Nape ndiye yule ambaye aliwahi kuchanganya jumuiya ya vijana kiasi cha kutaka kutimuliwa kwenye umoja huo, Kimsingi Nape nimwepesi wa kusahau, Nape alijulikana kuwa ni sumu mbaya ambayo haifai kuwa sehemu ya chama cha ccm. Leo hii nape amesahahu, anaeneza chuki na fitna kwenye chama. Lowasa alikuwa kiongozi wa juu ambaye hata kwa akili ya kawaida tu haiwezekani ahusike kwenye ununuzi wa mitambo, kipindi kile tulitangaziwa kabisa kuwa kama hali ya kupungua kwa kina cha maji ingeendelea vile nilazima nchi nzima ingezimwa umeme. HIVI INGEKUWA NI AINA GANI YA SERIKALI AMBAYO HAICHUKUI HATUA HATA BAADA YA KUAMBIWA HABARI HIZO MBAYA? kimsingi sio mwakyembe wala nani ambaye ameshasema ni kiasi gani Lowasa kachukua. Kwa nguvu zangu zote naamini Lowasa Hakuhusika kwa namna yeyote na kama amehusika basi baraza lote la mawaziri pamoja na mwenyekiti wao hawawezi kujitenga na ufisadi kitu ambacho naamini haiwezekani kwani naamini walikuwa na nia nzuri kwa Taifa bali watendaji wabovu ndiyo walistahili kubebeshwa lawama hizi vinginevyo SIJAONA TATIZO LA LOWASA, Kwa hawa wengine kama Rostam na Chenge siwezi kuzungumza maana kwa namna moja au nyingine mambo waliyotajwa nayo wanaukaribu nayo. Mimi sitaki dhambi!!!!!! LOWASA HANA HATIA ila kuliko kuendelea kuwepo kwenye chama cha kinafiki namna hii afadhali aondoke awaache hao wasafi tuone kama mambo yataenda. Kazi ya Lowasa waliowengi wanaitambua, na uchapakazi wake unaeleweka, sasa kuliko kuendelea na siasa hizi UCHWARA awaache illi watakapo garagazwa mwaka 2015 wasije sema ni Lowasa. Hivyoo awaandikie waraka wa HAMAN ili wakafie huko.!!!Katika kuchunguza kwangu uhalisia wa mambo nimegundua kwamba Lowassa anasakamwa kutokana na kuonekana kuwa ni mtendaji mzuri kumshinda Kikwete, jambo ambalo lilikuwa linahatarisha reputation ya Kikwete kama Rais.

Nape naye kwa kutokuelewa akakakurupuka tu na kuanza kumtaja Lowassa kama fisadi. Lakini mimi leo nataka mwenye data za ufisadi wa Lowassa na aseme hapa. Lowassa amefisadi nini? Watu mnapayuka tu Richmond, richmond, lakini hakuna anayesema Lowassa alipata bei gani kutoka kwenye ile Kampuni. Wote tunajua kwamba Rostam alipata bilioni 40 za kagoda kupitia kagoda, pia tunajua ndiye aliyekuwa mmiliki wa Richmond ambayo baadaye ilibadilishwa na kuwa dowans. Pia tunajua kwamba Chenge alituibia hela ya rada.

Sasa Lowassa ameiba nini kilicho dhahiri? Ninachoamini mimi Lowassa aliponzwa na utendaji wake, wa kutaka kupush mambo yaende. Hakuwa legelege kama Pinda ambaye anang'aa tu macho huku watanzania wakiteseka kutokana na ukosefu wa umeme. Lakini katika harakati za kuhakikisha watanzania wanapata umeme ontime Lowassa alijikuta analazimika kumpush Msabaha aharakishe utoaji wa tenda kwenye kampuni iliyopitishwa na kamati, bahati mbaya kampuni iliyopitishwa ikawa fake.

Lowassa hakuwa kwenye kamati ya kupitisha mzabuni wa kuleta mitambo ya umeme, na wala hakuna mahali panapoonyesha kwamba Lowassa alimwambia Msabaha lazima apitishe richmond badala ya makampuni mengine. Tuna ushahidi wa kimazingira juu ya ufisadi wa Chenge (vijisent), na ule wa Rostam ambaye alijitambulisha kuwa msimamizi wa Dowans. Sasa Lowassa ufisadi wake upo wapi?

Ninaamini kwamba Lowassa anaandamwa kutokana na utendaji wake, ati ni tishio kwa uongozi wa Kikwete, pia na fitina za Nape dhidi yake.
Thanks mkuu kwa kufafanua haya. Mimi nilikuwa siyajui!! Kumbe jamaa kafanya mengi kiasi hiki? Waache kutuchezea akili zetu hawa. Wanatuletea Pinda analia tu bungeni na hana lolote jipya la kufanya? Kuna haja ya kusimama na kusema no.1990-akiwa chief whip na disaster under pmo- aliondoa urasimu wa usafiri kwa wabunge, ndie alieasisi wabunge kukopeshwa magari-walianza na shangingi zile tzc....., ktk majanga kijana alikuwa nyota kila linapotokea alifika na suluhisho ndipo akaingia matatizoni na wenye hamu ya kumrithi mwinyi-akaondolewa pale kwa mzee malecela na kupelekwa ardhi......ndie aliewahimiza wananchi kutwaa mabati uwanja wa mnazi mmoja baada kuwepo kwa ujanja wa kubinafsisha viwanja vile.......taratibu watz walianza kumtambua ni nani huyu edward ngoyai lowasa....ktk michakato hii ndani ya zama za ruksa lazima kulikuwepo dosari ambazo aidha ziliwanufaisha baadhi ya watu au kuwaumiza baadhi ya watu...., tangu awali hakuwa tayari kuukubali umaskini wetu hivyo akawa highly spirited kujijengea nguvu za uchumi, nakumbuka rai likiwa chini ya jenerali twaha ulimwengu walimshamtoa front page 1995 "ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke......" by then nilikuwa mvulana mdogo sana lakini ninakiri kuwa licha ya ukwasi wake alikuwa my nambari wani kwa warithi wa mzee alhaj mwinyi na siyo vinginevyo....., 1995-07 alitoswa na mkapa na sababu wanazijua uvccm ya guninita ingawa mnataka sana hapa ndani tuamini ni mwal. Nyerere ndie aliemkataa....la hasha! Ilikuwa ni kazi ya rais mwenyewe ktk kuijenga nchi na chama kimoja na kuwa tayari kukubali matokeo na maamuzi ya chama..... Edward lowassa was dumped just because alikuwa true friend wa jakaya na alimaini 1995 ilikuwa zama ya uvccm kuitwaa nchi kitu ambacho mwalimu alikipinga kwa kumptisha mzee benjamin mkapa by then 56. Ni edward lowassa na ndg yangu na kaka yangu jj.guninita(shikambaku) walioweka wazi kuwa ccm imeidhulumu uvccm kwa kumpitisha bw mkapa......., lowassa alitolewa ktk gazeti la uhuru akiwa amekaa chini analia na tai yake ikiwa lose just because of jakaya candidacy......., ile image haikuwa nzuri kwa ccm, na hata jk aliposema kambi yake imevunjwa na inamuunga mkono mzee wetu mkapa wao wote hawakuwa wakweli ila ni hao wawili walishindwa kuwa wanafiki (lowassa na guninita), system ilijua na chama kilifahamu wakaadhibiwa, uwaziri ukamkosa lowassa licha ya ya mzee mwinyi kumsihi sana mkapa baada ya kuteuliwa mbele ya ccm -gm 1995 , "nakuomba usiwatupe ndg.lowasa na jndg.Kikwete, ni vijana wangu waaminifu na wachapa kazi, watakusaidia" tafuteni video ile ya kizota 1995. Ni jakaya tu alirudi novemba 1995, guninita pia alipoteza ukuu wa wilaya ya kigoma na hatimae alikimbilia chadema.......,
regime ya mkapa 1997-2005: Mazingira alifanya kazi tukufu.....maji :alipafanya pasikike na paheshimike na 2005-2008 under Jakaya aliimarisha zaidi nuru ya serikali na watumishi kuheshimu mamlaka na kuwajibika........, sidhani kama dhambi zake zitaishinda nuru yake na ule utamaduni wake wa kupenda kuwa mbali na unafiki......Edward Lowassa si mnafiki, ni rafiki wa ukweli na yuko tayari kuwajibika kwa gharama yake na taasisi anayoisimamia,kazi kwenu na tumhukumu kwa ukweli na si majungu...........
dah!kichwa ...hongera.Mbona huulizi kwanini siku zile Mwinyi aliachia nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani? Je kile kilichotokea kwa Mwinyi kilimaanisha kwamba yeye ndiye aliyesababisha wafungwa wafe? Au ilikuwa ni kwa sababu yeye alikuwa ndiye waziri mwenye dhamana? Basi kama mwinyi hakufunga milango wafungwa wafe, na bado akawajibika, vivyo hivyo Lowassa aliwajibika kutokana na nafasi yake na si lazima kwamba yeye aliiba hela akapeleka popote. Kama aliiba basi Nape atuambie ilikuwa ni bei gani? Na aliipeleka wapi? CCM wanapenda sana siasa za maji taka.
Mkuu mtazamaji ninaamini utakuwa hujamtendea haki kabisa Lowassa iwapo utamhukumu kutokana na uwingi wa mali alizonazo. Kiasi cha mali ambazo mtu anamiliki kinategemeana na akili yake binafsi. Thus, kama Lowassa alijua namna ya kutunza vizuri hela kumshinda Kikwete, basi hiyo isiwe ni sababu ya kuwafanya ninyi mmuone kwamba ni fisadi. Ana ng'ombe wa urithi huko, kama aliweza kuwauza na kuanzisha miradi mbalimbali ya kumuingizia kipato, basi hamna sababu ya kusema sasa ni fisadi. Ili kuweza kujiridhisha kwamba ni fisadi, nendeni mkatuonyesha mahali ambapo Lowassa alichota hela. Kama nilivyosema awali, tuna ushahidi kuhusu Rostam, tuna ushahidi kuhusu Chenge, wa Lowassa uko wapi? Usiseme tu niende tume ya maadili ya viongozi, maana kule wana orodha tu ya mali yake lakini hawana ushahidi wa mahali alipoiba Lowassa. Kwangu mimi naona hilo ni suala tu la akili ya mtu katika kujitafutia kipato. Kama tukisema hivyo, basi akina Mohamed enterprises, Bhahlesa na wafanyabiashara wengine wakubwa wote watakuwa ni mafisadi.
......Tusingekuwa bado tunaongelea njaa nchi hii kama ambavyo mambo yanakwenda hovyohovyo katika kipindi hiki cha Pinda. Niambieni leo, tangu mwaka 2008 Pinda amesimamia mradi gani uliofanikiwa?
Mkuu rejea sifa za kiongozi bora wa nchi au public. May be lowasa anaweza kuwa CEO bora wa kampuni. Amekaaa kibiashara biahsra zaidi. Lowasa hawezi kuwa kiongozi bora wa nchi. Uadilifu , uamnifu ni vitu muhimu kwa kiongoi wa umma lakini vinaweza visiwe muhimu kwa CEO wa makapuni ya biashara. Ndio maana unaona hata BAE walikubali kutoa mlungura.Kuhusu utendaji wa Lowassa ndugu yangu hatuhitaji kuandikia mate wakati wino upo. Lowassa alikuwa hafanyi kazi kwenye kamera. Kila alichokuwa anaagiza kifanyike, ndicho kilichokuwa kinafanyika. Sote tunakumbuka vizuri alivyosimamia ujenzi wa shule za sekondari na shule zikajengwa. Kile alichokuwa anaanzisha Lowassa alikuwa pia na uwezo mkubwa sana wa kukisimamia. Naamini kama sera ya kiilimo kwanza ingekuwa mikononi mwa Lowassa, basi sasa hivi tungekuwa tunaongea kitu kingine.
Yaani huyu waziri mkuu wa sasa amepinda kama jina lake. hakuna jipya linaloendelea chini yake. Na yeye anakaa na kulalamika badala ya kuchukua hatua. Zaidi sana anakaa na wabunge wa CCM kuwadhalilisha watanzania kwamba ni ombaomba wa posho zao. Pinda is one of the hopeless PM katika nchi hii. Lakini pia kwa kuwa anajua kwamba Kikwete ni mzee wa visasi, inawezekana anaogopa kushine sana kwa kuhofia kung'olewa kama alivyofanyiwa mwenzake.
Ulikuwepo wakati wanatumana??!!!
Nguo za kubadili mwezi mzima huna, . . . unapoteza muda na mambo ya watu wanaojenga uchumi wa wajukuu zao. . . . .
Bunge linajadili na kupitisha bajeti wabunge hawapo haikuumizi kichwa uko busy na makundi na mambo yao. . . . . Taifa hasara sana hili
Lowssa alifanya ufisadi mwenyewe, halafu unasema mtu anatumwa kwenda kufanya ufiadi?Afanye uamuzi mgumu kwa kumtaja mchana kweupe. Vinginevyo, ni msala wake tu.
Wabunge wajinga wote, mil.230 wanachukua halafu wanajifanya eti ni watetezi wa wanyonge.Ulikuwepo wakati wanatumana??!!!
Nguo za kubadili mwezi mzima huna, . . . unapoteza muda na mambo ya watu wanaojenga uchumi wa wajukuu zao. . . . .
Bunge linajadili na kupitisha bajeti wabunge hawapo haikuumizi kichwa uko busy na makundi na mambo yao. . . . . Taifa hasara sana hili
Katika kuchunguza kwangu uhalisia wa mambo nimegundua kwamba Lowassa anasakamwa kutokana na kuonekana kuwa ni mtendaji mzuri kumshinda Kikwete, jambo ambalo lilikuwa linahatarisha reputation ya Kikwete kama Rais.
Nape naye kwa kutokuelewa akakakurupuka tu na kuanza kumtaja Lowassa kama fisadi. Lakini mimi leo nataka mwenye data za ufisadi wa Lowassa na aseme hapa. Lowassa amefisadi nini? Watu mnapayuka tu Richmond, richmond, lakini hakuna anayesema Lowassa alipata bei gani kutoka kwenye ile Kampuni. Wote tunajua kwamba Rostam alipata bilioni 40 za kagoda kupitia kagoda, pia tunajua ndiye aliyekuwa mmiliki wa Richmond ambayo baadaye ilibadilishwa na kuwa dowans. Pia tunajua kwamba Chenge alituibia hela ya rada.
Sasa Lowassa ameiba nini kilicho dhahiri? Ninachoamini mimi Lowassa aliponzwa na utendaji wake, wa kutaka kupush mambo yaende. Hakuwa legelege kama Pinda ambaye anang'aa tu macho huku watanzania wakiteseka kutokana na ukosefu wa umeme. Lakini katika harakati za kuhakikisha watanzania wanapata umeme ontime Lowassa alijikuta analazimika kumpush Msabaha aharakishe utoaji wa tenda kwenye kampuni iliyopitishwa na kamati, bahati mbaya kampuni iliyopitishwa ikawa fake.
Lowassa hakuwa kwenye kamati ya kupitisha mzabuni wa kuleta mitambo ya umeme, na wala hakuna mahali panapoonyesha kwamba Lowassa alimwambia Msabaha lazima apitishe richmond badala ya makampuni mengine. Tuna ushahidi wa kimazingira juu ya ufisadi wa Chenge (vijisent), na ule wa Rostam ambaye alijitambulisha kuwa msimamizi wa Dowans. Sasa Lowassa ufisadi wake upo wapi?
Ninaamini kwamba Lowassa anaandamwa kutokana na utendaji wake, ati ni tishio kwa uongozi wa Kikwete, pia na fitina za Nape dhidi yake.