Nape, tuambie ufisadi wa Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape, tuambie ufisadi wa Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msema hovyo, Jul 16, 2011.

 1. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Katika kuchunguza kwangu uhalisia wa mambo nimegundua kwamba Lowassa anasakamwa kutokana na kuonekana kuwa ni mtendaji mzuri kumshinda Kikwete, jambo ambalo lilikuwa linahatarisha reputation ya Kikwete kama Rais.

  Nape naye kwa kutokuelewa akakakurupuka tu na kuanza kumtaja Lowassa kama fisadi. Lakini mimi leo nataka mwenye data za ufisadi wa Lowassa na aseme hapa. Lowassa amefisadi nini? Watu mnapayuka tu Richmond, richmond, lakini hakuna anayesema Lowassa alipata bei gani kutoka kwenye ile Kampuni. Wote tunajua kwamba Rostam alipata bilioni 40 za kagoda kupitia kagoda, pia tunajua ndiye aliyekuwa mmiliki wa Richmond ambayo baadaye ilibadilishwa na kuwa dowans. Pia tunajua kwamba Chenge alituibia hela ya rada.

  Sasa Lowassa ameiba nini kilicho dhahiri? Ninachoamini mimi Lowassa aliponzwa na utendaji wake, wa kutaka kupush mambo yaende. Hakuwa legelege kama Pinda ambaye anang'aa tu macho huku watanzania wakiteseka kutokana na ukosefu wa umeme. Lakini katika harakati za kuhakikisha watanzania wanapata umeme ontime Lowassa alijikuta analazimika kumpush Msabaha aharakishe utoaji wa tenda kwenye kampuni iliyopitishwa na kamati, bahati mbaya kampuni iliyopitishwa ikawa fake.

  Lowassa hakuwa kwenye kamati ya kupitisha mzabuni wa kuleta mitambo ya umeme, na wala hakuna mahali panapoonyesha kwamba Lowassa alimwambia Msabaha lazima apitishe richmond badala ya makampuni mengine. Tuna ushahidi wa kimazingira juu ya ufisadi wa Chenge (vijisent), na ule wa Rostam ambaye alijitambulisha kuwa msimamizi wa Dowans. Sasa Lowassa ufisadi wake upo wapi?

  Ninaamini kwamba Lowassa anaandamwa kutokana na utendaji wake, ati ni tishio kwa uongozi wa Kikwete, pia na fitina za Nape dhidi yake.
   
 2. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli magamba watoana macho hapa
   
 3. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haha hakuna kutoana macho, tunataka evidence tu hapa. Si kumsakama mtu bila sababu.
   
 4. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unakumbuka bifu la Nape na Lowassa kuhusu jengo la uvccm?
   
 5. s

  seniorita JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa kwani kaajia kiti? Kamwulize yeye
   
 6. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sana tu, ndo maana nataka Nape aseme ukweli kama Lowassa ni fisadi au ni visa binafsi tu? kama ni ufisadi basi atuambie Lowassa alifaidi bei gani kutoka Richmond, na ziliingia kwenye akaunti gani? Mwenzake Slaa huwa anataja hadi chain ya hela iilivyokuwa. Sasa mbona yeye anapiga tu kelele majukwaani hatuambii ushahidi kamili wa huo ufisadi?
   
 7. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona huulizi kwanini siku zile Mwinyi aliachia nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani? Je kile kilichotokea kwa Mwinyi kilimaanisha kwamba yeye ndiye aliyesababisha wafungwa wafe? Au ilikuwa ni kwa sababu yeye alikuwa ndiye waziri mwenye dhamana? Basi kama mwinyi hakufunga milango wafungwa wafe, na bado akawajibika, vivyo hivyo Lowassa aliwajibika kutokana na nafasi yake na si lazima kwamba yeye aliiba hela akapeleka popote. Kama aliiba basi Nape atuambie ilikuwa ni bei gani? Na aliipeleka wapi? CCM wanapenda sana siasa za maji taka.
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  huo utendaji uliomponza na kutosimamia haki ndio maana hahitajiki tena kule ccm
   
 9. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #9
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hakusimamia haki katika lipi? Na iwapo hiyo ndiyo sababu ya msingi ya kutomtaka Lowassa kule CCM basi wasiendelee kumchafua kwa kumwita fisadi. waseme tu kwamba wanamchukia kutokana na utendaji wake. Lowassa is not and has never been a fisadi, rather a very strong leader who knows how to risk for the benefit of the people.
   
 10. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Nape hana ushahidi na hata hana uhakika ka Lowassa ni fisadi au la, kama ni usafi hakuna aliye msafi ktk serikali ya JK mawaziri ni kama madalali wao wanaangalia madeal. Ila sababu JK ni mnafki kaamua kumtosa rafiki yake baada ya kuona anamfunika katika utendaji kazi kaamua kumtoa mhanga ktk deal ambalo hata yeye JK ni partcipant. Afu ndo akakumbuka kuna msema hovyo mwenye beef na EL ndio wakamuweka Nape ili alipe kisasi lakini sasa anambwelambwela. Walivyoona hiyo inaishiwa nguvu wakatumia mbinu ya kingmaker kujivua gamba lakini bado EL ni strong na hatishiki na siasa uchwara zao na JK analijua hilo vizuri saaana
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,424
  Likes Received: 19,747
  Trophy Points: 280
  hajui, huyu kazi yake ni kudandia vitu .. chadema wakianzisha yeye hudakia.
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kuwajua mafisadi na Lowasa akiwemo.

  • Nenda tume ya maaadil na vingozi wa umma angalia mali walizondikisha Ho viongozi na thamani yake .( Assuming utapewa acess za viongzi wote na lowasa akiwemo
  • Nenda UK waombe SFO wachungeze list yaviongiz wakuu wenye mali na account katika domain ya UK( Assmuning SFO watakubali na kuja na some evidence kama zile New jersey na majumba wanayonunua huko). Sasa bado huko Uswisi na USA.

  Si ajabu hata wewe utakuwa shocked. Hawa viongozi unaowasifia wachapakazi sio waadilifu na hawana uzalendo. Sifa za kiaongozi bora zinatakiwa kufuta mtiririko maalum.

  • Uzalendo
  • Uadilifu
  • Uchapakazi
  • ..... endelea

  Sasa washabikiwa lowasa wamekuwa wanataka kuwaka uchapakazi kama sifa ya kiongozi bora. Kiongozi akishaoksa kuaminiwa na watu Maana yake si muadilifu .Hata awe na sifa gani hafai .  Lowasa hacafuliwi kama ni kuchafuiwa basi ni hizo hizo mbinu alizotumia kuwachafua wenzake. Siku hizi malipo ya dhambi ni hapa hapa duniani.

  Kusema kwamba Lowasa ni strong leader si sahii. He is just an arrogant leader. nimeona Lowasa kwa kuutaka sifa za kinafkim mbele ya wananchi akiwa PM anawaibisha ma ma DC na ma RC kwenye mikutano yenye kamera.

  Yes style hiyo ilimpatia sifa lakini ni sanaa. Any strong leader should have known better jinsi ya kudeal na viongozi wanaokosea na ambao wako chini yake.

  Kuna mkuu wa wilaya mmoja alimtolea uvivu na kumwamboa PM anayoyasema na kuyaangiza mkutanoni ayaweke kwenye maandishi then akishindiwa uyatekeleza amfukuze kazi. lakini uzuri huyu mkuu wa wilaya hakumjibu vile kwenye mkutano bali ni nyuma ya pazia.
  Do u know nini kilifuata.............
   
 13. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu mtazamaji ninaamini utakuwa hujamtendea haki kabisa Lowassa iwapo utamhukumu kutokana na uwingi wa mali alizonazo. Kiasi cha mali ambazo mtu anamiliki kinategemeana na akili yake binafsi. Thus, kama Lowassa alijua namna ya kutunza vizuri hela kumshinda Kikwete, basi hiyo isiwe ni sababu ya kuwafanya ninyi mmuone kwamba ni fisadi. Ana ng'ombe wa urithi huko, kama aliweza kuwauza na kuanzisha miradi mbalimbali ya kumuingizia kipato, basi hamna sababu ya kusema sasa ni fisadi. Ili kuweza kujiridhisha kwamba ni fisadi, nendeni mkatuonyesha mahali ambapo Lowassa alichota hela. Kama nilivyosema awali, tuna ushahidi kuhusu Rostam, tuna ushahidi kuhusu Chenge, wa Lowassa uko wapi? Usiseme tu niende tume ya maadili ya viongozi, maana kule wana orodha tu ya mali yake lakini hawana ushahidi wa mahali alipoiba Lowassa. Kwangu mimi naona hilo ni suala tu la akili ya mtu katika kujitafutia kipato. Kama tukisema hivyo, basi akina Mohamed enterprises, Bhahlesa na wafanyabiashara wengine wakubwa wote watakuwa ni mafisadi.

  Kuhusu utendaji wa Lowassa ndugu yangu hatuhitaji kuandikia mate wakati wino upo. Lowassa alikuwa hafanyi kazi kwenye kamera. Kila alichokuwa anaagiza kifanyike, ndicho kilichokuwa kinafanyika. Sote tunakumbuka vizuri alivyosimamia ujenzi wa shule za sekondari na shule zikajengwa. Kile alichokuwa anaanzisha Lowassa alikuwa pia na uwezo mkubwa sana wa kukisimamia. Naamini kama sera ya kiilimo kwanza ingekuwa mikononi mwa Lowassa, basi sasa hivi tungekuwa tunaongea kitu kingine. Tusingekuwa bado tunaongelea njaa nchi hii kama ambavyo mambo yanakwenda hovyohovyo katika kipindi hiki cha Pinda. Niambieni leo, tangu mwaka 2008 Pinda amesimamia mradi gani uliofanikiwa?

  Yaani huyu waziri mkuu wa sasa amepinda kama jina lake. hakuna jipya linaloendelea chini yake. Na yeye anakaa na kulalamika badala ya kuchukua hatua. Zaidi sana anakaa na wabunge wa CCM kuwadhalilisha watanzania kwamba ni ombaomba wa posho zao. Pinda is one of the hopeless PM katika nchi hii. Lakini pia kwa kuwa anajua kwamba Kikwete ni mzee wa visasi, inawezekana anaogopa kushine sana kwa kuhofia kung'olewa kama alivyofanyiwa mwenzake.
   
 14. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asiyejua ufisadi wa Lowassa ima atakuwa chizi, fisadi, mnafiki, nepi hata mpumbavu. Mie naanza na Richmond ukiachia mbali kujilimbikizia mimali ya wizi na ujambazi. Kama unataka kujua ufisadi wa Lowassa jiulize kwanini huwa hataki kujibu tuhuma zinazomkabili. Lowassa ni fisadi ambaye hata kuku wanamjua kuwa ni fisadi sawa na pacha wake Jakaya Kikwete, Rostam Aziz, Andrew Chenge, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na wengine malizia.
   
 15. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #15
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wee huna hoja, nimesema mtuambie ni wapi palipochotwa hela na mkaambiwa kwamba amechota Lowassa? Tupe ushahidi kwamba yeye alikusanya hela ya Richmond kwa namna yoyote ile. Na kwamba yeye ndiye aliyeingia mkataba ya Richmond au kujihusisha na Richmond kwa namna yoyote ile. Hatutaki blabla, leteni ushahidi. Mbona ushahidi wa Chenge kushiriki kwenye wizi wa Rada mmeutoa, lakini wa Lowassa hamleti? Huu ndo ulimbukeni wa watanzania walio wengi. Wanaishi kwa kuamini magazeti, ndiyo maana hata pale mlipodanganywa na magazeti kwamba kikwete ni rais mzuri mkampa kura kwa asilimia 80, kumbe mwenzenu anakwenda kucheza disco Ikulu. Fanyeni utafiti na si kuamini katika udaku. Ukisema Lowassa ni fisadi kwa kuwa ni tajiri, basi hata Mohamed enterprises naye ni fisadi kwa kuwa naye ni tajiri. Utajiri ni akili ya mtu na si lazima kila anayekuwa na hela awe ameiba.
   
 16. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #16
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndugu Nape Nnauye, kwa kuwa katika namna yoyote, wewe na wanamagamba wengine kama Sitta na Chiligati mmeshindwa kuthibitisha ufisadi wa Lowassa mbele ya jamii, nafikiri umefika wakati sasa wa kurudi nyuma na kumuomba radhi mheshimiwa huyu kutokana na kumchafua bila sababu.

  Nilianzisha thread juzi ya kuwataka watanzania walete ushahidi wa ufisadi wa Lowassa, watu wamebaki tu kuniambia eti ni tajiri. That is nonsense, kwani matajiri wote ni mafisadi. Kwa kuwa wewe huna mbinu za utafutaji hela, basi mwenzako akijinyima na kuwekeza sehemu productive unamgeuka na kumwita Fisadi? Sasa nyie magamba kwakuwa hamna ushahidi wa ufisadi wa Lowassa, tunataka sasa mmuombe radhi mbele ya halaiki kama mlivyofanya wakati wa kumchafua.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,424
  Likes Received: 19,747
  Trophy Points: 280
  msema ovyo unamsafisha Lowasa?
   
 18. K

  Kamura JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli wewe ni msema hovyo2. Umetumwa!
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Csiem hakuna msafi!
   
 20. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Siku mjumbe wa nyumba kumi atamiliki Jet wapambe wake watasema alikuwa anadunduliza..!!(?) Kweli kuchelewa kufa ni kuona mengi...!! Hakyamungu, Yesu, Maria na Masawe!!
   
Loading...