Mkuu, kujiuzulu ni hulka ya mtu na nia ya kuwajibika kutokana na yanayotokea chini ya usimamizi wake. Mbona Ali Hassan Mwinyi naye alijiuzulu uwaziri wakati wake? Je alikosa nini? Lakini hapohapo geukia watu kama akina Hussein Mwinyi ambapo mabomu ya jeshi yamekuwa yakiua watu wasio na hatia na hajachukua hatua yoyote, unataka kusema hana makosa? Au mwangalie ngeleja. Pamoja na kushindwa kabisa kutatua tatizo la umeme linaloikabili nchi, bado hajaona sababu ya kujiuzulu. Lowassa angeweza angeamua kujikausha. After all, report ya akina Mwakyembe haikumtaja Lowasa moja kwa moja. Kwa hiyo angeweza tu kujikausha asijiuzulu kama ambavyo akina Hussein Mwinyi na Ngeleja walivyojikausha.
Mimi nashangaa mnaweka blabla nyingi tu juu ya ufisadi wa Lowasa cha ajabu hamsemi ni wapi ambapo paliibiwa na ikabainika kwamba aliyeiba ni Lowassa. Nataka hapo. Nakumbuka hata Nyerere wakati anamkataa Nyerere alimkataa kutokana na utajiri wake. Hakutaja popote kwamba Lowassa ni mla rushwa. Sasa hii habari ya ufisadi mnaoutaja ninyi leo upo wapi? Nataka mseme alichukua hela mahali fulani (kama ambavyo tunataja za Kagoda au za Rada). Lowassa alichukua zipi?
Kuna kitu hapa nafikiri hamjakielewa kuhusu Nape. Huyu bwana amewekwa ili kumsafishia njia Kikwete. Kwa kuwa Nape alishaonyesha mapema ubavu wa kupingana na Lowassa hadharani, basi Kikwete akamwona ndiye anayefaa katika hiyo shughuli ya kummaliza na kumwangamiza rafiki yake. Kwahiyo Nape anatumika kama vuvuzela la Kikwete kwa ajili ya kupazia sauti ya kuwafukuzia mbali marafiki zake wa zamani. Kutokana na tofauti zao zaz kiuongozi. Remember, Lowassa alikuwa anaonekana kuwa na mamlaka mkubwa kumshinda Kikwete wakati akiwa waziri mkuu, na hii ikawa ni threat kubwa kwa Kikwete, kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere na Sokoine.