Nape: Siwajui Mbowe, Slaa

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika hali ya kushangaza amedai hawajui Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Katibu wake, Dk. Willbrod Slaa katika duru za siasa nchini.
Aidha, Nape aliziita tuhuma za ‘kipumbavu’ dhidi ya chama chake juu ya kile kilichodaiwa kuwepo kwa mipango ya kuwabambikizia kesi baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA kwa lengo la kuwadhoofisha wao binafsi na chama kwa ujumla.
Akihojiwa na Tanzania Daima kwa njia ya simu kuhusiana na tuhuma hizo, Nape alisema hawezi kujibu madai yasiyokuwa na maana na pia hawajui hao wanaoitwa Mbowe na Slaa.
“Nimesahau kama wapo Dk. Slaa na Mbowe ndiyo unanikumbusha wewe,” alisema na kuongeza kuwa viongozi wa CCM hawajakutana mahali popote kuzungumzia suala hilo na kueleza kuwa huo ni upuuzi usiokuwa na mashiko.
Alisema anaamini kinachofanyika sasa ni kwa viongozi wa CHADEMA kukimbia kivuli chao, kwani anaamini habari hizo zimetungwa na zina baraka za viongozi wao wakuu.
Nape alidai kuwa viongozi wa CCM hawana muda wa kuwafikiria CHADEMA, kwani si chama chenye maana kinachoweza kuwasumbua wala kuwapotezea muda.
“Uchaguzi umekwisha, hatuna muda wa kuwafikiria viongozi wa CHADEMA, kwanza si chama, sasa tunafikiria kutekeleza ilani ya chama chetu,’” alisema.
Alisema kuwa viongozi wa CHADEMA ndio wenye muda wa kuwafikiria viongozi wa CCM na kusema, “Wao ndiyo wanafikiria, ‘tumfanyeje Nape na JK’.”
Katika tuhuma hizo, baadhi ya viongozi wa CCM wanadaiwa kufanya kikao na wahariri kadhaa wa vyombo vya habari vinavyoegemea upande wake pamoja na maofisa wa Usalama wa Taifa, ili kuweka mikakati ya kuhakikisha wanaidhoofisha CHADEMA kabla ya mwaka 2013.
Miongoni mwa majina ya viongozi walengwa katika mkakati huo ni Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu (Mbunge wa Singida Mashariki) na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Kwa mujibu wa habari hizo, viongozi hao na wengine wanaoonekana kuisumbua zaidi CCM na serikali yake, watategeshewa kashfa kadhaa zitakazoandikwa na kutangazwa na vyombo hivyo vya habari ili kuwadhalilisha na kuwafanya waonekane hawana maana ndani ya jamii.
Mbali na hilo, mkakati huo unakusudia kuichimba CHADEMA kama taasisi na kuhakikisha inapandikiziwa mamluki ili wavuruge uchaguzi wa ndani wa chama hicho.
Majibu ya Nape yamekuja siku mbili tu baada ya kutoa matusi mazito katika mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Mwanza.
Katika mkutano huo ambao ulitawaliwa na vurugu kubwa zilizosababisha kupigwa na kuumizwa vibaya kwa vijana wawili wanaohisiwa kuwa wafuasi wa upinzani, Nape aliwatukana matusi mazito wanaoiunga mkono CHADEMA.
 
Walimtosa kugombea Ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CDM lazima awe na Hasira nao
 
Vijana wasiotumia akili zao na Nape ni mmoja wao, kitu ambacho ccm ndiyo wanakitaka
 
Hivi hii ndio kazi ya katibu mwenezi wa CCM? kuongea hata kisichokuwa na maana
 
Mimi nilifikiri labda Makamba na Tambwe Hiza ndiyo walikuwa waropokaji kumbe la hasha. Wote walikuwa cha mtoto, huyu wa sasa ni kiboko! Yaani analopoka mpaka basi si muda mrefu sana itawagharimu CCM.
 
Back
Top Bottom