Nape Nnauye: Tumehujumiwa..

Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.

Hata hivyo, Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "Mbona Igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...
Nape arudishe tu kadi, CCM sio deal anymore mbaya zaidi CCM inakataliwa sehemu za vijijini ambazo rahisi kuwahadaa kwa vijisenti,

Sasa watu hawadanganyiki tena, Nape kama anaipenda Tanzania ahame CCM
 
Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.

Hata hivyo, Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "Mbona Igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...

Nape asitudanganye..... Nani kamhujumu? maana chama chake kilipeleka kila aina ya watu wenye ushawishi ndani ya CCM wakijua wanashinda lakini Peoples power imefanya kazi yake, Zaidi awpongeze kina Mwigulu, BWM, Lowasa, Lusinde kwa Matusi yao...

Waambieni zama tutanunua ndege ya Rais hata waTZ wakila nyasi zimepita sasa ni msipotenda haki iwe polisi, CCM, UWT JWTZ naSerikali tunafanya tunachokitaka...

Nawahakikishia wazee wa miaka 60 kwenda juu na wanawake hawawezi kutuzuia kuleta mabadiliko nchi hii....
 
Nape is damn right. Kuna MPAMBANO (hujuma) wa makundi NDANI ya chama kuelekea 2015.
 
Usahihi ni kuwa,CCM mmefanya kila mliloweza kuhujumu uchaguzi. Jana kuanzia asubuhi hadi jioni, nimeshuhudia magari ya CCM (yanayodhaniwa kuwa yalibeba masanduku ya kura) yakifuatiliwa kwa kwa mwendo -kasi wa juu na makamanda waliokuwa katika LandCruiser za Ndesamburo. CCM ilifanya hivi ili kuiba kura. Kwa mujibu wa kamanda Nassari, wakati akihutubia umati wa watu saa moja pale kambi ya CHADEMA, nyinyi watu wezi, wahujumu na ving'ang'anizi, mmeiba kura 14,000 za CHADEMA.
Aidha, jana asubuhi, Mwigulu Nchemba alikamatwa akigawa pesa kanisani na kushikiliwa kituo cha polisi USA RIVER .Kama anaubavu aje hapa akanushe, halafu sisi tutaweka video ya tukio zima.
 
Energy lower (el-2015) wazo hili lishindwe na lilegee katika jina la yesu na ndg zangu waislam kemeeni kwa dini yenu na hata wapagani kemeeni wazo chafu ilove cdm for my life for tanzania, god bless cdm god bless dr slaa for 2015
 
Nape,
punguza porojo kijana kama ulikuwa unayajua yote hayo ya kuhujumiwa kwa nini ulienda Arumeru kufanya kampeni..
Inawezekana hayo maneno amewekewa mdomoni, kwani naye amekanusha. Bila shaka yeye alisema (kwa mujibu wa wall yake ya fb)

Nape Nnauye
Hongereni watani (Chadema) kwa ushindi Arumeru Mashariki. Ninawapongeza mmeshinda! Ndio kauli ya wana Arumeru Mashariki nasi tunaiheshimu! Fanyeni kazi kutimiza mliyowaahidi wapiga kura. Kila lakheri!!

Hivi ndivyo washindani halisi na breakthrough leaders wanavyopaswa kuwa kwani, kunaworse things that can happen in life than losing in election, but we all know the pain we can feel after a difficult loss, or even the joy we feel after a great win.

Hongera CDM kwa kuonyesha njia. Hongera viongozi wa CDM kwa kutokata tamaa, at least kwa sasa score board imeanza kusoma na upande mwingine (8-1).

Kudos CDM
 
Nakubaliana na Nape,watu kama Lusinde hawakuwa na nia nzuri na mgombea,siamini kama matusi yale yaliyoidhoofisha sana CCM aliyatoa kwa bahati mbaya,bila shaka alitumwa na alilipwa kumdhoofisha Sumari kwa kisngizio cha kampeni.Pia kitendo cha kumleta mtu mwenye tuhuma nzito za ufisadi pia nadhani zimechangia kumuangusha.Nassari pia kapata kura za sympathy kwani kumsema mtu kuwa afahi ubunge kwa vile ni masikini na wakati huo huo unaowaambia hivyo ni masikini ambao ndio majority ni wazi watatoa kura za huruma kwa maskini mwenzao,next time kwenye kampeni CCM mtumie watu wenye Elimu na wanaojua psychology ya common people,what to say to them,when and how.Mkiendelea kutumia watu kama Lusinde na Nchemba na Wasira walahi mtaendelea kupoteza majimbo.Na kama kuna mtu amefuatilia kwa makini kampeni za Arumeru na zile za udiwani ni wazi kuwa sasa hivi CCM na CHADEMA nguvu sawa Tanzania nzima na hata uchaguzi mkuu ukirudiwa Tanzania leo hii CCM na CHADEMA wanaweza kugawana viti vya ubunge na hta kura za uraisi.CCM kaeni chini mtafakari where you went wrong and why,kamata watuhumiwa wote wa ufisadi peleka mahakamani ,kama watachiwa basi waachiwe na mahakama,with that angalau mnaweza kuregain confidence ya Watanzania,lakini huu usanii wa kujivua gamba mnaoufanya sasa hivi sio convincing kwa wananchi kwani watu wanaona kuwa it is just a mere slogan like other CCM slogans,hakuna gamba linalovuliwa,sana sana baadhi ya magamba yanajiandaa kuwania uraisi 2015.Mbadilike,watanzania wa leo sio wa mwaka 47.
 
Hongereni wana Arumeru kwa kufanya uchaguzi salama. Hongera Bwana Nasari na CDM kwa ushindi huo mzuri. WanaArumeru wana imani kubwa na Nasari pamoja na CDM kuwaletea maendeleo ya haraka.
 
Nape ungeshinda ungeongea hayooo yote

Ndio unakumbuka kuwa mna watu nambao hawakubaliki duuu hiiii kali

Pepoooooooooooo============

Mfa maji?????????????????????????/ ha
 
Ni kweli kauli ya SENDEKA ya kuendekeza ukabila na ile ya LUSINDE kumwaga matusi zaidi ya mlevi wa gongo hata kama mimi ningekuwa mpiga kura wa Arumeru nisengekipigia kura chama cha namna hiyo.

Wawatumie watu wenye staha na lugha njema kwenye kampeni zao


Usisahau na ile ya Mkapa kwamba "Vincent si wa ukoo wa Baba wa Taifa". Jamaa hawakuwa makini kwenye kampeni, lakini pia watu wamekichoka chama, wanataka kukipumzisha.
 
Mboma mtalaumu sana tu. Kuna mwandishi mmoja wa ki-America aliwahi kusema "The very important thing in life is not to capitalize on your gains, any fool can do that. The most important thing in life is to capitalize on your losses, that requires intergense. And it makes big difference between the man of sense and a fool" Kuna siku mtauliza bona hata Mbeya mjina tulishinda? Kumbe na kwenyewe Sugu ndo baba mwenye nyumba. Kaazi kwelikweliiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Back
Top Bottom