Nape Nnauye: Tumehujumiwa..

hakuna kitu kibaya duniani hapa kama kuchezea mguvu akili muda wa wananchi na kuwadanganya kama watoto wadogo kwa kuchakachua Kura. ni wakati sasa umefika kuheshimu Maamuzi sahihi ya wananchi
 
Ni kweli kauli ya SENDEKA ya kuendekeza ukabila na ile ya LUSINDE kumwaga matusi zaidi ya mlevi wa gongo hata kama mimi ningekuwa mpiga kura wa Arumeru nisengekipigia kura chama cha namna hiyo.

Wawatumie watu wenye staha na lugha njema kwenye kampeni zao
nimeshangaa hata baada ya hayo yote bado wamepata kura nyingi sana, hawakustahili hata kura elfu moja. Waliniudhi sana hao ndugu, hasa huyo wa pili, hata jina lake sitaki kulitaja
 
Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.

Hata hivyo, Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "Mbona Igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...

Nnape,Nnape,Nnape acha porpjo za kilevi. Kuanzia sasa tunaanza kukuita NEPI. Hili jina litakufaa sana!

Nakumbuka juzi tarehe 31/3/2012 siku ya kufunga harakati za Kampeni wewe mwenyewe Mhe. Nnepi na rafiki yako Lowassa RichMonduli mlikwenda Arumeru East ukatamba kuwa CCM mtashinda kwa kishindo na ukadai ETI VIONGOZI WAKUU WA CDM Mbowe na Slaa wajiuzulu baada ya matokeo ya Arumeru East yatakayo onyesha CCM imeshinda.

Pole sana Mhe. Nnepi. Bila shaka hukuwa umeijua nguvu ya CDM huko Arumeru East,na laiti ungelijua usingeropoka manemo hayo. Pale kwenye nyekundu nataka nikwambie hivi:Kwa taarifa yako IGUNGA CCM HAMKUSHINDA KABISA HUO NI UKWELI NA HATA WEWE UNAJUA HIVYO.

Siyo Igunga tu hata UCHAGUZI MKUU WA 2010 CCM HAMKUSHINDA. Tutakutana 2015 KWENYE BALLOT BOX.

Wasaalamu.
Ushindi wenu wa Igunga ulikuwa wa KUIBA,KUGUSHI NA KUCHAKACHUA.
 
Nape Nape ubado kijana mdogo katika siasa za TZ hebu tafakari kwa makini kama CCM ni mahala salama kwa kuendeleza career yako ya siasa. Taifa linawahitaji watu kama Nape na > Mtatiro but either kwa tamaa ya madaraka na mali ama ufinyu wa kufikiria vijana kama nyie mnapotea kabisa. Time bado inaruhusu mnaweza badilika sasa na kuchagua mahala salama pakufanyia siasa zenu
 
ccm bwana yaani wamezoea wizi basi wanapata tabu kweli wakishindwa...hahaaa si walikuwa wanajidai na mivitambi akina wassira na mkapa....Yaani mkapa kajidhalilisha sana ..apumzike tu anywe ma Grants yake watu watamuelewa sio kujiingizakwenye mambo haya
 
Nape kweli kiazi...huyu si alikua anasema lazima washinde?leo imekuaje??anajua maana ya "LAZIMA TUSHINDE" kweli mfa maji haachi kutapatapa
 
Ndugu yangu Nape,kusoma hujui hata picha nayo huoni ,..tatizo lenu ninyi CCM ni kwamba, kwa sasa HAMKUBALIKI kamwe hata angeenda nani mkeshindwa tu,mbona huko Kiwira na Kirumba mmewapeleka hao wewe unaowaita WASAFI,nako chali,kiufupi TUMEWACHOKA kwa kuwa mgawanyo wa keki sio mzuri,kulindana,wizi wa kutisha wa mali za umma na kila uovu ninyi tu..yaani kwa ufupi mpo mpo tu!
 
Sometimes kujitetea kwingine ni kuzidi kuonyesha weaknesses; now we know sio kwamba tu wameshindwa bali wenyewe kwa wenyewe wana hujumiana (as if we did not know that already)......., Such comments just shows the limit of the Chap's thinking capacity.
 
CCM hawajafanyiwa hujma yoyote. Waliofanyiwa hujma tena za hali ya juu ni wananchi walala hoi wa nchi hii - kwa miaka 50!
 
Hello JF members ninayo furaha kubwa kujiunga na mtandao wawanajamii kutoa michangao mbalimbali ya ukombozi wa nchi yetu na bara la Africa. Kwa leo napenfa kuipa hongera Mh, Nasari, viongozi wa Chadema na wanachama na mashabiki wao wote, Aidha napenda kuwapa pole wana CCM wote kwa kupoteza Jimbo kwani hizo ndio siasa na asie kubali kushindwa sio mshindani. Kwapamoja sasa tushirikiane kujenga nchi yetu na kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inapata Katiba huru katika mchakato wa katiba utakaonza hivi karibuni.
 
Huu ni upuuzi. Watu wasiokubalika? Kwani Rostam Aziz anakubalika na jamii? Mbona alipanda jukwaani Igunga na CCM ikashinda?(Kama kweli ilishinda), maana hata kura za Urais 2010 hatujui jumla zilikuwa ngapi?
 
katibu mwenezi wa ccm,nape nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa ccm katika uchaguzi wa ubunge wa arumeru mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na kagenzi na kuonyesha kuwa joshua nassari wa chadema ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa ccm.

Hata hivyo, nape hakuwataja watu walioihujumu ccm uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "mbona igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...

nahisi nape amechanganikiwa.anaona kobe anajitoa gamba lake ambalo ndiyo uhai wake..ikimaanisha ndiyo kifo chake..ccm gamba linakwisha na ndiyo kifo chenu..........viva arumeru.
 
Amlaumu Lusinde kwa matusi, na waone aibu kupeleka jeshi zima arumeru, mkapa, wassira, lowassa. Wamejihujumu wenyewe kwa hiyo aongee na kikwete mwenyekiti wake. Sisi anatupotEZEA MDA TU KUTUelezea yasiyo tuhusu
 
Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.

Hata hivyo, Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "Mbona Igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...

Kama unamsingizia basi unapata dhambi kubwa sana na kama amesema kweli basi leo ndio nahitimisha doubts juu ya ubongo wake:
1. Anaposema kuna watu wasiokubalika kwenye jamii, NANI ALIWAWEKA? YUPI ANAYEKUBALIKA? Na je, wanafiki wanakubalika? (Kama hawakubaliki basi na yeye hakubaliki kwani anaongea unafiki)

2. Sidhani kama kuna mtu aliihujumu CCM kwa makusudi. Navyofahamu, maneno kama yale ya Lusinde (kijana apewe nafasi ya marehemu baba yake ili apate mshahara...thawabu....huruma....) ni zao la ubongo wake na siasa za CCM. Kilichowahujumu ni wingi wa shule kanda ya Kaskazini na sio Lusinde, Lusinde ameongea kwa kadiri ya akili zake na siasa za CCM ambazo huhitaji MDOMO na TUMBO tu na si akili.

3. (Mbona IGUNGA hatukushindwa?!) Kwa Nape kushindwa kuna maana gani? Hivi kudrop toka 87% mpk 4?% ni ushindi kweli kwa mtu anayejua hisabati?!!! Ina maana Nape hajui kuwa Arumeru hakuna uwezekano wa kuwagawa watu kwa HIJAB?

Kama mlitaka ya Igunga yajirudie mngesubiri kipindi cha njaa ndio muitishe uchaguzi Arumeru ili mkagawe mahindi na sukari siku moja kabla ya siku ya kupiga kura ndio mngeshinda.
 
Back
Top Bottom