Nape Nnauye kauli yako kwa Mbowe kuhusu Arusha kabla ya mabomu ukiwa Dongobesh, mbulu nieleweshe!

Wakuu,
Kwa zaidi ya siku 10 nilikuwa likizo nyumbani Mbulu. Nikaamua kutumia likizo yangu Dongobesh ambako kulikuwa na uchaguzi wa Udiwani. Kama mnavyojua tuliwashinda ccm kirahisi. Na nitaeleza zaidi mbinu iliyotumika kuwashinda kirahisi kwenye uzi mwingine.

Hata hivyo, kwa leo naomba kupata ufafanuzi kutoka kwa Nape Nnauye katibu mwenezi wa CCM Taifa kuhusu kauli aliyoitoa Mbulu tarehe 15/6/2013, kata ya Dongobesh katika mkutano wa hadhara uliofanyika karibu na ofisi za CCM. Naomba ufafanuzi wa kauli yake hiyo, kwa sababu kwangu mimi inaleta utata mkubwa sana kwa kuzingatia kilichotokea siku hiyo hiyo Arusha tena kwa mtu ambaye yeye alimtaja kwa jina - yaani Freeman Mbowe.
Nanukuu kauli Nape Nnauye katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika baada ya Mbowe Kuondoka kutokana na watu wote kuhamia kwa Mbowe na Nape Nnauye kulazimika kusubiri Mbowe aondoke kwanza ndiopo afaye mkutano.
katika mkutano wake Nape Nnauye alisema;

kwanza nawapa pole kwa kuachiwa mavumbi na helikopta ya CHADEMA. Kabla Mbowe hajapaa nilimwandikia meseji kwenye simu yake. Nilimwambia kuwa watu wa Arusha wamechoka na Maandamano sasa wanataka amani. Nikamwambia utaikuta aibu yako Arusha.

Maswali,
kwa kuwa jumamosi siyo siku ya uchaguzi, uchaguzi ni siku inayofuata, mimi nikajiuliza ni aibu gani atakayoikuta Mbowe Arusha jumamosi ya 15/6/2013? Maana angesema kuwa Kesho (jumapili ya 16/6/2013) ningefikiri kuwa Nape Nnauye anazungumzia aibu ya CHADEMA kushindwa uchaguzi. Mbowe Arusha alikutana na Mabomu ambayo kuna kila dalili kuwa yalimlega yeye na Lema. Swali langu ni Je, mabomu hayo ya Arusha ndiyo aibu ya Mbowe aliyoizungumizia Nape Nnauye huko Dongebsh Mblu?

Pili, Nikiunganisha kauli hii ya Nnauye na kauli ya Mwigulu Nchemba kwamba msipoichagua CCM Arusha mtakufa, halafu nikaunganisha dots zangu na kauli ya Mbowe kuwa anaushahidi wa video wa Polisi kuhusika na tukio la mauaji ya Arusha, mwishowe nikahitimisha kwa kauli ya Waziri mkuu Pinda kwamba bomu hilo lilitengenezwa China na huwa linatumiwa na wanajeshi kujilinda, napata jibu langu la uhakika moyoni. Sijui wewe.


Je kuna mtu amlirekodi hotuba ya Nape hapo Dongobeshi? Nadhani ushahidi huu ni tosha kuunganisha dots. Yaani kama mpaka hatua hii CCM hawajakubali kwamba Mungu amewakataa basi wasibirie muziki wake kamili pia.
 
Napendekeza iundwe tume huru ya kuchunguza haya mambo, kama kuna tetesi kwamba poilis walihusika katka hili, basi hawawezi kujichunguza wenyewe, kwa maana hiyo basi iundwe tume huru isiyo na maslahi na chama, jeshi la polis au serikali kuchunguza hili tukio na kutupa majibu kamili. Tunaona uchungu sana kushuhudia haya yanayotokea Tanzania leo, kwa mwananchi mweye akili timamu, kitendo kama hiki cha kujirudiarudia kwa kulipuliwa mabomu kule Arusha kinaweza kuwa na siri nzito sana nyumba yake. Kila tetesi ifanyiwe kazi ili kupata ushahidi wa kusaidia hiyo tume. Hakuna mshindi katika hili, si ccm, si chadema wanaouwawa ni walipa kodi wasio na hatia, wengi ni wamama na watoto ambao hawajafika hata umri wa kupiga kura (kama tutalihusisha hili jambo na chaguzi zinazoendelea hapa Nchini) Bomu si kitu cha kufumbiwa macho kabisa, kama lilitengenezwa nchini Uchina, basi hata siku lilipoingizwa Nchini itajulikana, hata mrushaji pengine anweza kujulikana kama utaratibu wa ki intelejensia utatumika zaidi ya jazba na vitisho wanavyotoa wanasiasa. Ni maoni yangu tu kwamba hili swala la mabomu kujirudiarudia kule Arusha, liangaliwe kwa jicho la ziada...


Nakubaliana na wewe 100%
 
Je kuna mtu amlirekodi hotuba ya Nape hapo Dongobeshi? Nadhani ushahidi huu ni tosha kuunganisha dots. Yaani kama mpaka hatua hii CCM hawajakubali kwamba Mungu amewakataa basi wasibirie muziki wake kamili pia.

Mkuu hiki kitu alikisema kwenye mkutano wa hadhara mashahidi wako 100 wakitakiwa. Kumbuka wapo hata watoto, vijana na wazee waliomsikiliza.
 
Wakuu wa jamvi hili nisaidieni,Hivi ndani ya chama cha mapinduzui hakuna kabisa vijana makini, waadilifu,wastaarabu,wenye hofu ya Mungu,na wenye kujua nini maana ya Demekrasia,ni kweli wamekosekana kabisa mpaka ikapelekea ccm wakawaweka hawa vijana?

wapo ila inawezekana hawa wanaotumika sasa ndio wanafaa kwa kazi waliyotumwa kufanya.
 
Back
Top Bottom