Nditu
Member
- Mar 12, 2011
- 84
- 26
Jana nilikuwa namtazama EDWARD LOWASA akichangia hoja bungeni kwa mara ya kwanza toka ajiuzulu, lengo ilikuwa kupima nguvu na uwezo alionao ndani ya ccm baada ya propaganda ya kilivua gamba iliyoanzishwa dhidi yake ukweli ni kwamba Nape anajihangaisha na ukweli wa mambo ni kwamba waliompa hii kazi hawana nia njema na future yake kwani watammaliza mtoto wa watu kisiasa namuonea huruma kwani bado kijana mdogo anapaswa ajiulize kwanini wakubwa wake akiwamo mwenyekiti wake hathubuti kunyanyua mdomo dhidi ya LOWASA? Nape nakushauri swala la kuvua gamba wamekutupia zigo huwawezi hata kidogo wamekudhidi umri na hata ushawishi wewe endelea na kazi zingine za chama ambazo hata hivyo zinaboa kwani wananchi wamekata tamaa na nyie
Nape ni kipofu na ni zao la ufisadi. Nyerere (RIP) alishatueleza kwamba hakuna kiongozi anayetokana na ufisadi atakayemudu kuupiga vita ufisadi.
Nape haiwezi vita dhidi ya ufisadi kwa vile tayari watu wameshaijua bei yake. Mnakumbuka alipopigapiga kelele dhidi ya ufisadi ndani ya CCM hadi kuanzisha CCJ Kikwete alilijua hilo, kwamba ni njaa tu iliyokuwa inamsumbua. Ndiyo maana alimhonga kitu kiduchu tu akamsambaratisha, nacho kilikuwa cheo cha Ukuu wa Wilaya. Kijana alijiona kama amepelekwa nusu ya mbingu na pole pole alianza kuitikia kiitikio cha '"Si CCM wote Mafisadi.... bali wachache...'" Hakuishia pale bali alianza kufurukuta tena kwenye ukurasa wake wa Facebook na mwerevu Kikwete akaona amwongezee zigo la uongozi ndani ya chama chakavu, kilichochakachuliwa na mafisadi na kubakizwa pumba tupu cha CCM ambako aliingia kichwa kichwa na sera yake ya kuwapa aliowaita mafisadi siku 40 kujivua magamba! Sasa ni zaidi ya siku sitini na ameufyata mkia bila ya kuchukua hatua yoyote.
Nape ni mropokaji kama Makamba na Tambwe Hiza, na laana ya kuusaliti msimamo wa kisiasa wa Hayati Baba yake aliyekufa akiwa mwadilifu, mwenye kuheshimiwa na kutukuka na akiwa mjamaa wa kweli itamwandama maishani mwake mwote. Kina Lowasa, Chenge, Rostam Aziz, Kikwete, Mkono na orodha ndefu ya mafisadi ndani ya CCM ni werevu kuliko Nape na wanajua fika wanachofanya. Kwa vile ni suala la wakati Nape na wapambe wake wataumbuka na kama kawaida mafisadi watashinda.
Vita dhidi ya ufisadi kamwe haitaweza kusimamiwa kikamilifu na CCM - chama kichakavu, kinachougua kansa na kilichokwisha poteza mwelekeo bali chama kipya, chenye ari na dhamira ya kweli kama CHADEMA. Watanzania wameshalijua hilo na ni suala la muda tu kabla hawajachukua hatua. Binafsi naamini 2015 utakuwa ndiyo mwisho wa usanii unaoendelea sasa wa hili dude linaloitwa CCM.