Nape na Waraka wa Kuituhumu CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape na Waraka wa Kuituhumu CDM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mashikolomageni, Sep 20, 2011.

 1. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii nimekutana nayo FB ikanistua sana nimeona niilete hapa kwa great thinkers tuijadili na mwenye habari zaidi atupashe I

  [h=6]York David Drexell

  ANGALIZO HATARI KWA WATANZANIA WOTE POPOTE PALE WALIPO;

  Watanzania wote kwa ujumla wetu, wakubwa kwa wadogo, wanaharakati, asasi binafsi na za uuma, viongozi wa dini nk. yatupasa kuamka na kutambua nini kinachoendelea ndani ya nchi ya Tanzania na kukemea kama sio kulaani mbele ya Muumba wetu harakati hizi za umauti:

  Mh. Nape Nnauye kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi "CCM" ni binadamu hatari sana, sio tu kwa amani ya nchi ya ...Tanzania halikadhalika kwa jumuiya nzima ya kimataifa kwa vizazi hata vizazi.

  Upo waraka umekamatwa leo hii na taasisi moja binafsi hapa nchini ulioandaliwa na kusainiwa na kada tajwa hapo juu, aliouandaa na kuusambaza kwa wajumbe wa kamati kuu ya ccm (Nec) kupitia moja ya vikao vyake ukiwaamuru kwa makusudi kabisa wajumbe hao wa kamati tajwa kukihujumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo "CHADEMA", kwa kuhakikisha kwamba kinapoteza uaminifu, utashi na kukubalika mbele ya jamii kwa kutekeleza yafuatayo;

  1. Kuandaa nyaraka feki zitakazouaminisha umma kwamba cdm ni chama cha kidini na ukabila kadiri itakavyowezekana.

  2. Kuandaa nyaraka zitakazo uaminisha umma kwamba, cdm kipo kwenye mpango wa makusudi kabisa kuhakikisha wanatekeleza uhaini ndani ya nchi kwa kutumia mamluki (waasi) toka jamuhuri ya kidemokrasia ya watu wa Congo.

  3. Kuandaa taarifa feki zitakazouaminisha umma kwamba, cdm ndicho chama kinachoratibu na kutekeleza mauaji ya raia wasiokuwa na hatia yanayoendelea hapa nchini.

  4. Kuwahujumu viongozi wa cdm kwa kuwabambikizia kasha mbalimbali nzito hasa za kukutwa na madawa yakulevya hali kadhalika kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi duniani yanayoongozwa na Al-qaeda.

  5. Kutengeneza nyaraka feki ambazo zitauaminisha umma na ulimwengu kwa ujumla kwamba, cdm kipo na mpango wa makusudi kabisa kuhakikisha Tanzania inajiondoa kwenye jumuiya ya umoja wa mataifa "UN" kwa kuafikiana na itikadi za kikundi cha kigaidi cha Al-qaeda na washirika wake kwa kutumia vivuli vya viongozi wake wa juu.

  Source: Wajumbe ndani kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi wenye uchungu na nchi yao waliojawa na hofu ya Mwenyezi Mungu.
  [/h]
   
 2. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Magamba in action! Kuweni na subira tu watanzania wenzangu tutasikia mengi sasa hivi maana watu wakiishiwa sera na mvuto ukapauka ujue wanaweza hata kusema "Slaa anatembea na mke wangu" na vilaza wenzie wakajitokeza kuandamana kuunga mkono! This is only the beginning, there is much more coming!
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  It will take a tommyrottish credulous clown to take this story seriously.
   
 4. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata kama mtu hatakuwa na akili nyingi hatashindwa kutambua kuwa hizo nyaraka zitakuwa zimekosa maana kabla hata haijafikishwa kwa watu. Kwanza, ni kweli CDM kimehujumiwa kwa mikakati ya kukipaka matope kwamba ni cha kidini. Ni gani hiyo?(walisema ni cha Kikristo). Pili, kama CDM kina mwelekeo wa Kikristo basi kingependelea ukiristo na kuchukia Uislamu(ambao Al - Qaeda unahusishwa nacho).

  Kama hoja ya kwanza inakubalida, ya kwamba CDM ni chama cha kidini na dini hiyo ni ya Kikristo basi hoja ya pili ya kukihusisha CDM na Al-Qaeda haiwezi kukubalika. Hivyo, mtoa mada hapo juu ninaona kuwa ama umeleta suala hilo wewe mwenyewe au hao wanaoanda mkakati hawajui wanachofanya.
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  mh! Mbona kazi ipo unafiki on making,hatudanganyiki na ulichokiandiki
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Hebu tuletee huo waraka wenyewe tuuone.
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Umeona eeh!, authenticity ya habari hii kuwa waraka uliandaliwa na Nape iko wapi? BTW-siasa ni mchezo mchafu so the opposite might be correct.
   
 8. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa Magamba kila kitu kinawezekana!
   
 9. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Japokuwa NAPE anamadhaifu mengi Sidhani kama ni mpumbavu kiasi hicho. Hii itakuwa imetiwa chunvi, lakini ni nzuri. It seems to me you cany make a good political strategist


  I
   
 10. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nape ni jalala na atayemfuata ni shetani tu hakuna mtu wa kawaida atakayefanya hivyo.
   
 11. n

  nyantella JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  tuletee waraka wenyewe maana it seems wamekupa au ulikaa waka kuhadhia tu? rudi waambie wakupe waraka halisi uuweke hapa!
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ninachokifahmau mimi kuwa ni kama ajenda kukinukisha chama cha CDM machoni pa wananchi kuwa;
  1. Ni chama cha wahuni, wasiofuata utaratibu katika mambo yao. Hili linakololezwa kwa tabia ya CDM kupenda kutoa hisia kwa njia ya maandamano. Hoja inyaojengwa kila siku maandamano, maandamano hayo yanasaidia nini? Uchaguzi ulishakwisha, hivyo tufanye kazi tujenge nchi yetu. Hili kwa watu wasio na upeo wa kuona mbali limekuwa likiwaingia pole pole.
  2. Kuhakikisha wabunge wote machachari wanakesi mahakamani za kujibu na kujenga hoja kuwa hawa watu hawana muda wa kuwatumikia wananchi kila siku wanashinda mahakami. Hili nalo lisipofatutiwa tiba litapunguza kura siku za usoni
  3. Kuwaaminisha wananchi sehemu nyingi zilizochagua upinzani hazina maendeleo kutokana na wawakilishi wao aidha kutokuwa na muda wa kutulia majimboni mwao au kuwaaminisha wananchi kuwa serikali imefanya hujuma kutoleta maendeleo kama adhabu kwa wananchi hoa kuchagua upinzani. Ukweli katika jambo hili, ni kuwa sehemu nyingi hata ambazo CCM na serikali yake bado ndiyo ngome yake hazina maendeleo ya kutosha kama inaaminishwa machoni pa wananchi.
  4. Njia nyingine ni kutumia udini, ukabila kuwagawa watu. Hapo awali ilidhaniwa kwa kuwa Dr. Slaa aliwahi kuwa padri basi angeliungwa mkono na wakristo wengi na kupenyeza udini na ukabila ili uwe msalaba kwa CDM. Hili nalo limeanza kufa baada kuonekana CDM kuna waislam wengi na htaimaye hoja hiyo kuenakana hiana mashiko.
  Mwisho fitna ulizozisema za Nape ni ndogo na bado Nape hakubaliki sana na makundi ylaiyopo ndani ya CCM ambapo kundi la mafisadi ndilo lenye nguvu mpaka kufikia kutishia mtandao wa JK ulioasisiwa na hao mafisadi 2005.
  Ni mtazamo tu.
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  sasa km udini mbona ccm ndiyo chama cha kidini?.,.....mpaka wanaamua kuweka mambo ya dini ya kiislamu kwenye ilani yao wakati wanaamini mdomoni kwa vyama na serikali havina dini.......................cuf kilka mtu anajua kuwa ni taasisi ya kiislamu na mfungmano mzuri kabisa na al-shababu ila kitendo cha ccm kuikomalia cdm ni kwa sababu ushindi wa ccm ndo huohuo wa cuf kwani sera zao zaudini wa kiislamu na kutuletea viongozi legheleghe na wachovu km kiwete zinafanana kabisa
   
 14. A

  Anold JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Ni kisiasa zaidi, utafiti zaidi
   
 15. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kila kitu kina mwanzo na mwisho wake,tusubiri???
   
 16. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160

  Kwamaana hiyo hapo hakuna hoja kwa sababu hata hiyo ya kwanza haikubaliki.
   
 17. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  nape yupo humu tunaomba akanushe hii habari au kukubali,right to be heard kabla ya kuhukumu
   
 18. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  yani magamba wana plan A,B,C hadi Z
   
 19. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #19
  Sep 21, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Panga hoja vyema achana na majungu yasiyo na mwelekeo,kichwa wala miguu..Nape ana mapungufu (Kilaza) sana ila hapa unatupotosha
   
 20. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  bora nawewe umemshtukia mleta mada,nadhani huu waraka kauandaa yeye,mtu kama Nape kama anaweza kuandika waraka wa kitoto unaojichanganya kama huu...hizi ndio aina ya siasa ambazo mh.Samuel Sitta alizibatiza jina la siasa za maji taka,jina ambalo limekua maarufu mpaka leo.Hivi kwanini huyu kijana some folks humu tunamchukia sana wakati amajitoa mhanga kupambana na ufisadi na mafisadi waliokiteka chama kinachounda serikali
   
Loading...