Nape na posho za Wabunge

Nape na posho za Wabunge

Kwani Nape kuna ugumu gani wa kuunganisha ubongo kwanza kabla ya kufungua mdomo ??? Kwa spidi hii watakutema mapema.
 
Zitto unatushangaza sana kuhusu suala lako la Posho yako kupelekwa KDI. Kama wewe unadhamira njema na si kutafuta umaarufu na ghiliba kwa Watanzania kwa nini usingepeleka hoja binafsi ya kubadili sheria bungeni ili muifute? Sheria huvunjwa kwa kupeleka Mswada bungeni sasa kijana unategemea kweli utaivunja kwa kumwandikia spika barua au kwa kuongea mitaani na barabarani. Zitto kuwa makini katika hili watu wanaokuheshimu na kukuona wewe kama mtu makini wanakudharau.
ACHEBE hivi unajiita au wanakuita greatthinker? jiulize mara mbilimbili. Unashangazwa wewe na nani wenzio?
Kwa utafiti ganiitto anadharauliwa, kweli ulikuwa nae Udsm ktk nyanja ipi labda gardener au canteen kwasababu unaonyesha upeo mdogo mno ktk kujadili mada. Go back and come with a thread that can upgrade you.
 
Wabunge wanne wa NCCR toka mkoa Kigoma, wameungana na mh Zitto kutaka posho zao zielekezwe ktk maendeleo ya Kigoma kwani pamoja na mkoa huo kuwa nyuma kimaendeleo, ktk bajeti hii umetengewa kiasi kidogo sana kuliko mikoa yote kwa ajili ya maendeleo
 
Hii nzuri sana Chadema na NCCR waungane na wapinzani wengine kutoka CUF wakatae posho waachieni CCM wazichukue. Hakimu atakuwa 2015 uchaguzi ukija kama CCM itapata viti 15 sijui labda wachakachue sana!!!!!
 
Zitto unatushangaza sana kuhusu suala lako la Posho yako kupelekwa KDI. Kama wewe unadhamira njema na si kutafuta umaarufu na ghiliba kwa Watanzania kwa nini usingepeleka hoja binafsi ya kubadili sheria bungeni ili muifute? Sheria huvunjwa kwa kupeleka Mswada bungeni sasa kijana unategemea kweli utaivunja kwa kumwandikia spika barua au kwa kuongea mitaani na barabarani. Zitto kuwa makini katika hili watu wanaokuheshimu na kukuona wewe kama mtu makini wanakudharau.
Hiyo ni hatua ya kwanza, na kwa sababu hiyo hoja si yake pekee yake bali ya chama hivyo chama ingelitolea ufafanuzi na kutoa tamko rasmi pindi watakapokuwa wakiwakilisha bajeti kivuli J5. Lakini wakati akisubiri hayo ndiyo ameamua kuchukua uamuzi huo, sasa ubaya uko wapi?
 
Inawezekana kuishi bila posho mbona miradi ya yote ya kimaemndeleo inayofadhiliwa na world bank hapa nchini haina bajeti ya sitting allowance ingawa katika kutekeleza miradi hiyo vikao vinakuwepo na sitting allowance hailipwi.

Na hata GIZ ni wajerumani wao hufadhiri hasa katika maswala ya maji hawana utaratibu wa sitting allowance na shughuli zao zinakwenda vizuri.
Good start, we can make it possible
 
safi sana vijana inaelekea mnaanza kuwa na akili kidogo. sasa nataka muendelee kujadili kama kweli wanauchungu na hizo pesa kwa nini wawe na uchungu na hizi na wasiwe na uchungu na milioni 7 isiyotozwa kodi wanayomlipa Slaa. Acheni kuwa makasuku hapa hakuna nia yeyote njema zaidi ya kutaka umaarufu. lakini kwa miaka hii yote mitano iliyopita alipokea. Amekumbuka nini mwaka huu? I know Zitto vizuri toka nikiwa naye UDSM. He is the same hajabadilika ila kwa ninyi msiomfahamu endeleeni kula chaka.

Tofautisha haki ya mtu na ufisadi wa kiidara. Posho anayolipwa Dr Slaa ni haki yake lakini mnayochukua bungeni ni ufisadi. Chukueni hizo hela zetu za kodi makutano ni 2015!!!!
 
Kwa taarifa yako wabunge wa NNCR nao kesho wanapeleka barua kuomba posho zao za sitting allowance zielekezwe kwende Vote 74 ya Kigoma ambayo ina fungu dogo kuliko mikoa yote Tanzania. Hawakuishia hapo bali watapeleka mswaada wa kufuta posho hiyo.
 
Mkuu nadhani tatizo la Watanzania siku zote ni ktk maswala ya siasa. Tuna ujinga fulani ambao hauwezi kuelezeka kirahisi bila kuhoji dhamira za watu.

Labda nikukumbushe tu kwamba swala la posho za vikao halikuanza jana wakati Zitto anahoji posho hizi, lipo bungeni na limekuwepo kwa muda isipokuwa viongozi wetu hawataki kusikia kabisa kuondolewa kwa posho. na hakuna ujanja mwingine wowote wa kuwabana viongozi isipokuwa kwa mmoja wao kuwapa mtihani ambao hawataukubali ili mradi swala zima la posho lipate kuzungumziwa.

Sisi kama wananchi tunachotakiwa kujiuliza ni kwa nini wabunge wetu wanaotuwalikisha hawataki posho hizi ziondolewe! Kwa nini haramu hii inazidi kutukuzwa bungeni badala ya wao kama wawakilishi wa wananchi kufuata na kutumikia maagizo ya wananchi na sio kutafuta vijisababu vya kupinga dhamira ya Zitto ili mradi Zitto mwenyewe ndiye awe sababu.

Sijui kama unamkumbuka Babu wa Loliondo, yeye alikuwa akitoza Tsh 500 tu kwa dawa ya ponya yake lakini wapo watu waliompa ama kutaka kumpa fedha zaidi akawaambia wapeleke kanisani, sasa ukianza kujiuliza kwa nini anataka hizo fedha zaidi ziende kanisani kwa fikra kwamba yeye ni mchungaji hivyo anataka kujinufaisha kwa kupitia huko unakuwa unapotosha maana kwani hoja nzima ni kwamba Uganga wake unagharimu Tsh. 500 tu.
Na wala haikuishia hapo tu kuna watu walihoji vikombe, masufuria, mahema na hata nyumba alokuwa akihudumia mchungaji wakamwona tapelii tu wakati hawa hawa watu wana magonjwa makubwa yanayohitaji sana msaada wake na wala isingewagharimu hata kama dawa hiyo haitawaponya lakini inawapa unafuu fulani..

Hii ndio tabia ya Wadanganyika, tabbia ambayo siku zote hulalamikia hata vitu ambavyo malengo yake ni kuwaponya wao wkani Zitto anachokifanya hapa lengo lake haswa ni kuhakikisha Posho hizi zinaondolewa na fedha hizo zipelekwa (re allocated) ktk matumizi mengine ya msingi..

Jamani ebu irudieni kuisoma Bajeti utaona kwamba tunapanga matumizi ya trillioni 13 na kati ya hizo karibu trillioni moja imetengwa kwa posho tu, fedha ambazo zingeweza kabisa kuondoa matatizo mengi ya mishahara ya walimu, madaktari au hata kuboresha shule na hospital zetu lakini viongozi wetu wamegoma kabisa kuondoa hizi posho ambazo kusema kweli wao wenyewe wanasema hupokea zaidi ya mishahara yao..

Dhamira ya Zitto ni kuhamasisha wabunge wazikatae hizi posho lakini imeshindikana hivyo swala kubwa kwetu iwe kuuliza hawa wabunge kwa nini wamekataa kuondoa Posho hizi hali sisi wananchi tunaambiwa tujifunge mkanda hali ya uchumi ni mbaya na nakumbuka Ngeleja aliwahi kusema kila mtu atakula kwa jasho lake!

Mkuu,

Usimwamshe mtu aliyelala kwani Zitto anachojaribu kukifanya ni kuleta heshima na uwajibikaji serikalini waache watakaokubali wakubali halafu wananchi wataenda kufahamishwa vizuri kwanini akina Zitto walikuwa wakizipinga bungeni.
 
Kuna wakati nahisi kama kiongozi wa NCCR-bungeni ni Zitto Kabwe - Mbatia anabaki kuongoza huku uraiani, think!
 
unajua licha ya hiyo sitting allowance ya Tsh. 70,000 kwa kila kikao bado analipwa per diem/Night Out Allowance ya Tsh. 80,000 kila siku anayokuwa Bungeni
 
Dr. SLAA AKIWA MBUNGE NDIO ALIANZA SASA CHADEMA INAMALIZIA!!!!

Zitto yeye kasema kwa kipindi watakapokua bado hawajaifuta ipelekwe Kigoma!
 
du hii ni atari aisee na wengine wamegomea posho sasa mambo yanaonekana nguvu ya uma inawaakumba wengi big up kwa wanaharakati wa kweli na sio maneno:lock1:
 
unajua licha ya hiyo sitting allowance ya Tsh. 70,000 kwa kila kikao bado analipwa per diem/Night Out Allowance ya Tsh. 80,000 kila siku anayokuwa Bungeni
80,000.00 per diem inawatosha kabisa, vinginevyo wapandishe posho ya per diem tunufaike sote badala ya kujirundikia maposho mengo peke yao.
 
Zitto unatushangaza sana kuhusu suala lako la Posho yako kupelekwa KDI. Kama wewe unadhamira njema na si kutafuta umaarufu na ghiliba kwa Watanzania kwa nini usingepeleka hoja binafsi ya kubadili sheria bungeni ili muifute? Sheria huvunjwa kwa kupeleka Mswada bungeni sasa kijana unategemea kweli utaivunja kwa kumwandikia spika barua au kwa kuongea mitaani na barabarani. Zitto kuwa makini katika hili watu wanaokuheshimu na kukuona wewe kama mtu makini wanakudharau.

mimi sijui wewe ni mtanzania au ni mzimu uliofufuka? au wewe nae ni mbunge wa upinzani ambaye unahisi zitto kawapa mtihani, kwa kuwa mlienda bungeni kutafuta posho tu, anyway lakini kuwa makini sana na urpokokaji wako.
wewe hujui nchi hii inavyofunika kombe....., angepeleka mswaada inamaanisha usingepitishwa na miposho ingeliwa kama kawa. punguani weee
 
safi sana vijana inaelekea mnaanza kuwa na akili kidogo. sasa nataka muendelee kujadili kama kweli wanauchungu na hizo pesa kwa nini wawe na uchungu na hizi na wasiwe na uchungu na milioni 7 isiyotozwa kodi wanayomlipa Slaa. Acheni kuwa makasuku hapa hakuna nia yeyote njema zaidi ya kutaka umaarufu. lakini kwa miaka hii yote mitano iliyopita alipokea. Amekumbuka nini mwaka huu? I know Zitto vizuri toka nikiwa naye UDSM. He is the same hajabadilika ila kwa ninyi msiomfahamu endeleeni kula chaka.

naona umejiondoa kwenye hoja yako uliyoianzisha kimyakimya, sisi watu makini tunakuomba ueleze nini unachotaka tujadili! Zito uliyemfaham UDSM? Dhamira ya kuacha posho za vikao? Zito anatafuta umaarufu? Kuwa staight.
Jiulize kwanza, siasa bila umaarufu ni siasa? Lazima ujulikane, watu waone makeke yako ndio wakuchague! Wewe mbona hujachaguliwa hada kuwa diwani? Ni kwa sababu hujulikani na hujafanya watu wakujue!
Sio ila hoja mkatae kwa kuwa amesema mpinzani! Zito ameenda hatua zaidi, ametekeleza kwa vitendo dhamira yake, na si maneno,!
 
kawaida yake kupayuka
Nimesoma gazeti moja la leo nape akikiri sio yote wasemayo wapinzani ni ya kupuuza (posho) na akasema ishu ya posho hataisemea coz yeye c mbunge sasa huko itv kafuata nini, mbona haeleweki.
 
sio hao wa ccm tu, hata wa cdm nao wapo nawajua wamejisikia hovyo sna ila wanaona aibu tu mzeee, wanalo mwaka huu.
mahesabu yao yote ya kuezka kwa vigae kwa viposho yamezimwa mwaaaaaaaa, zitto kawapa mtihani mzee
 
Back
Top Bottom