Zitto unatushangaza sana kuhusu suala lako la Posho yako kupelekwa KDI. Kama wewe unadhamira njema na si kutafuta umaarufu na ghiliba kwa Watanzania kwa nini usingepeleka hoja binafsi ya kubadili sheria bungeni ili muifute? Sheria huvunjwa kwa kupeleka Mswada bungeni sasa kijana unategemea kweli utaivunja kwa kumwandikia spika barua au kwa kuongea mitaani na barabarani. Zitto kuwa makini katika hili watu wanaokuheshimu na kukuona wewe kama mtu makini wanakudharau.
Mkuu nadhani tatizo la Watanzania siku zote ni ktk maswala ya siasa. Tuna ujinga fulani ambao hauwezi kuelezeka kirahisi bila kuhoji dhamira za watu.
Labda nikukumbushe tu kwamba swala la posho za vikao halikuanza jana wakati Zitto anahoji posho hizi, lipo bungeni na limekuwepo kwa muda isipokuwa viongozi wetu hawataki kusikia kabisa kuondolewa kwa posho. na hakuna ujanja mwingine wowote wa kuwabana viongozi isipokuwa kwa mmoja wao kuwapa mtihani ambao hawataukubali ili mradi swala zima la posho lipate kuzungumziwa.
Sisi kama wananchi tunachotakiwa kujiuliza ni kwa nini wabunge wetu wanaotuwalikisha hawataki posho hizi ziondolewe! Kwa nini haramu hii inazidi kutukuzwa bungeni badala ya wao kama wawakilishi wa wananchi kufuata na kutumikia maagizo ya wananchi na sio kutafuta vijisababu vya kupinga dhamira ya Zitto ili mradi Zitto mwenyewe ndiye awe sababu.
Sijui kama unamkumbuka Babu wa Loliondo, yeye alikuwa akitoza Tsh 500 tu kwa dawa ya ponya yake lakini wapo watu waliompa ama kutaka kumpa fedha zaidi akawaambia wapeleke kanisani, sasa ukianza kujiuliza kwa nini anataka hizo fedha zaidi ziende kanisani kwa fikra kwamba yeye ni mchungaji hivyo anataka kujinufaisha kwa kupitia huko unakuwa unapotosha maana kwani hoja nzima ni kwamba Uganga wake unagharimu Tsh. 500 tu.
Na wala haikuishia hapo tu kuna watu walihoji vikombe, masufuria, mahema na hata nyumba alokuwa akihudumia mchungaji wakamwona tapelii tu wakati hawa hawa watu wana magonjwa makubwa yanayohitaji sana msaada wake na wala isingewagharimu hata kama dawa hiyo haitawaponya lakini inawapa unafuu fulani..
Hii ndio tabia ya Wadanganyika, tabbia ambayo siku zote hulalamikia hata vitu ambavyo malengo yake ni kuwaponya wao wkani Zitto anachokifanya hapa lengo lake haswa ni kuhakikisha Posho hizi zinaondolewa na fedha hizo zipelekwa (re allocated) ktk matumizi mengine ya msingi..
Jamani ebu irudieni kuisoma Bajeti utaona kwamba tunapanga matumizi ya trillioni 13 na kati ya hizo karibu trillioni moja imetengwa kwa posho tu, fedha ambazo zingeweza kabisa kuondoa matatizo mengi ya mishahara ya walimu, madaktari au hata kuboresha shule na hospital zetu lakini viongozi wetu wamegoma kabisa kuondoa hizi posho ambazo kusema kweli wao wenyewe wanasema hupokea zaidi ya mishahara yao..
Dhamira ya Zitto ni kuhamasisha wabunge wazikatae hizi posho lakini imeshindikana hivyo swala kubwa kwetu iwe kuuliza hawa wabunge kwa nini wamekataa kuondoa Posho hizi hali sisi wananchi tunaambiwa tujifunge mkanda hali ya uchumi ni mbaya na nakumbuka Ngeleja aliwahi kusema kila mtu atakula kwa jasho lake!