Kwa hili naweza kukuunga mkono. Hii hamisha hamisha ya watendaji wabovu inalea ubovu, tunakuwa tunahamisha tatizo toka sehemu moja kwenda nyingine. Lakini nadhani tuende hatua mbili mbele. Pendekeza katika chama chako na serikali, kwamba baadhi ya nafasi ambazo kwa sasa ni za kuteuliwa, zigeuzwe kuwa za kugombania katika soko la ajira, tuziondoe katika uteuzi wa Raisi. Hapa ninaongelea nafasi hizi:-
1. Makatibu wakuu wa Wizara
2. Wakurugenzi wa vitengo vya wizara
3. Wakurugenzi wa wilaya
4. Wakurugenzi wa miji na majiji
5. Watendaji mbalimbali wa Ikulu
Tukifanya hivyo itakuwa rahisi kuwawajibisha pale wanapoboronga, kama ilivyo kwenye sekta binafsi. Lakini kwa sasa inakuwa ngumu hata kwa waziri mkuu kumwajibisha mteule wa raisi, kisa? Hajamteua yeye. Hii ndio sababu inayofanya tunakuwa na akina Jairo na Nyoni kibao katika nchi. Hawa wanawajibika kwa aliowateua, si kwa wananchi, ndio sababu inayofanya wanakuwa na kiburi, nadhani unanielewa. Hizo nafasi tajwa hapo juu inatakiwa ziwekwe kwenye soko la ajira, zisiwe za uteuzi. Nadhani suala hili tuliingize katika katiba mpya!
Mkuu Idimi naomba nitaje sababu kuu ya Serikali ya CCM kuendelea kuweka wateule katika nafasi za kiutendaji ambazo tungetegemea zifuate taratibu za competition katika soko la ajira.
Hizo nafasi ulizozitajaa CCM hawawezi kukubali ziende kwa makundi mengine ya watu hasa wanaogopa zinaweza kuangukia mikononi mwa watu wa vyama pinzani au wanaharakati wa kweli wenye lengo la kufanya kazi bila ufisadi.
Kuna kipindi nilipata nafasi ya kuwa kwenye team ambayo ilizunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wadau na kufanya utafiti kuhusu maendeleo ya zao fulani ambalo ni muhimu hapa nchini.
Moja ya wadau walikuwa hao namba 2.Wakurugenzi wa wilaya na wakuu wa wilaya.Kila ofisi niliyoingia nilikuta ilani ya CCM kwenye ofisi ya hawa watendaji hakuna kitu kilicho nitia simanzi kama hicho kwa kuwa ni conflict of interest ya hali ya juu.Pata picha mkuu wa mkoa ni mteule wa mwenyekiti wa CCM,Mkurugenzi wa mji pia,mkuu wa wilaya hali kadhalika,mkurugenzi wa wilaya pia.Kwenye vikao vya halmashauri mbalimbali ni nani atathubutu kumkosoa mwenzake wakati wote ni magamba na wanatokana na chanzo legelege,fisadi na dhalimu?
Illustration:
Naomba nitoe mfano hai ili tuone uhalisi wa hili suala.Tulipita wilaya ya Korogwe huku tukiwa na appointment na Mkuu wa wilaya Bw.Erasto Sima lakini yeye asubuhi hiyo hakuwa ofisini kwa hiyo tukaambiwa na Katibu Mhutasi ametoka kidogo ila twende tukazungumze na Mkurugenzi wa wilaya huyo akatuambia mkuu wake wa kazi ameenda vijijini kufuatilia masuala muhimu atarudi jioni sana.Tukajadiliana machache na huyo DED then tukaaga na kuahidi tutarudi kesho kutwa yake.
Kwa kuwa tulihitaji kuwahi wilaya nyingine na tulikuwa nyuma ya muda ikabidi tupate lunch ya mapema then tuwahi kwa wadau wengine wilaya ya Lushoto badala ya kupoteza siku Korogwe.Narudi zangu hotelini nilipofikia namkuta Mkuu ya wilaya yako counter/reception akipata vinywaji laini akiwa na mrembo aliyejazia na kwa kuwa hakuwa ananijua sikuwa na haja ya kusalimiana naye nikaendelea na shughuli zangu za kukusanya makabrasha na nguo zangu na kurudi(niliporudi sikumkuta pale reception na sitaki ku-speculate kilichoendelea) kwenye usafiri wetu kuanza safari ya Lushoto.
Kesho kutwa yake tukarudi tena Korogwe na kupata mahojiano na Bw.Erasto Sima huku akianza kwa kuomba msamaha kwa kushindwa kuonana na sisi jana yake kutokana na majukumu ya kiofisi.Pia hakutupa strategic inputs muhimu ikionyesha hakujiandaa wala hakujua lolote kuhusu mazao ya wilayani mwake.Bahati nzuri DALDO(Afisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya) alikuwepo na akatusaidia sana.
Kwa ufupi hawa watu wameshajimilikisha ofisi ambazo zinaendeshwa kwa kodi za wananchi na wanatenda vyovyote vile watakavyo.Hayo ndio madhara ya mfumo wa uteule huku takwa mojawapo likiwa kuwa na kadi ya CCM.
Naunga mkono kuwe na badiliko katika katiba mpya.
Nawasilisha.