Nape na mafisadi wa CHADEMA

Ni misemo ya babu zetu kuwa '' DEBE TUPU HALIKOSI KUTIKA'' nape inabidi kumuonea huruma kwani hajui anachokifanya kama chama naye HANA DIRA WALA MUELEKEO hivi si ajabu kwa debe tupu kutika.
Ni dhahiri kifo cha nyani miti yote huteleza kwa sasa C.C.M haina jipya, mbele ya nguvu ya umma hawawezi kudanganya tena. Tumuuomde Dk slaa ampe notes za ufisadi Nape kama ana uwezo mzuri wa kusoma ili aweze kusoma na kuelewa maana ya ufisadi iikibidi apewe darasa na CHADEMA wenye mikakati yao ili ajue nini anazungumza.
 
Siasa za Bongo jamani zinachekesha sana. Huyu Nape majuzi tu alisema wanajivua magamba lakini wameshindwa kufanya hivyo - Rostam, Lowassa na Chenge wanapeta ndani ya chama hali chama wakijua hawa watu sii wasafi.. Sasa imekuwa vipi mchawi awe Chadema hali ahadi wamezitoa wao?..

Au pengine Nape kuzungumzia mshahara wa Dr.Slaa anataka CCM wamtazame na yeye mshahara wake? Hivi Nape anapokea ngapi kama Katibu wa CCM?..kwa sababu sioni kabisa mahusiano ya mshahara wa mtu na Ufisadi ikiwa leo hii hatufahamu mshahara wa rais wetu acha mbali mshahara wake yeye mwenyewe.
Nape jivueni magamba hayo mlowaahidi wananchi hizi habari za Chadema sijui wasafishe kwanza nyumba yao unataka kusema kwamba Taifa zima ni nyumba ya CCM na haiwahusu Chadema?..mbona mnatuchanganya na hizi siasa za kuokoteza!
 

dah,mkuu heshima kwako,...
unaona mbali sana,na hili nadhani ndilo analo kusudia
"mbona chadema wanatoa mshahara mnono,na mimi pia"
 

Kaka mchambuzi.
Kweli hata sielewi ni wapi umesimama. Kama Mchambuzi umeshindwa kutambua kuwa ufisadi ndiyo umesababisha matatizo katika mahitaji muhimu kwa watanzania basi huna budi kulikana aidha hilo jina au salutation hiyo.

1. Ufisadi umechangia wananchi kuzidi kuwa maskini.
2. Ufisadi umechangia wananchi kuzidi kupoteza maisha yao kwa kukosa madawa hospitalini.
3. Ifisadi umechangia akina mama kujifungulia barabarani, misituni kwa kukosa huduma karibu.
4. Ufisadi umesababisha Usalama wa Taifa letu kuwa mikononi mwa genge la watu wasiokuwa waadilifu.
5. Ufisadi umesababisha uchumi wetu kuwekwa mikononi mwa watu wachache wasio na mapenzi na uzalendo wa nchi nyetu.
6. Ufisadi umesababisha serikali kutojali wananchi wake walio na dhamana ya nchi yao.
7. Ufisadi umesababisha serikali ya JK anayeongoza Taifa letu kuendeshwa kwa REMOTE CONTROL.
8. Ufisadi umesababisha wananchi wanakosa haki ya kuwa na kiongozi waliyemchagua kwa kura halali.
9. Ufisadi unasababisha wananchi wananyimwa nafasi kujadili mustakabali wa Taifa lao, eti ukizungumzia Muungano au madaraka ya Rais basi unafungwa. Bulls@%#&*^t
10. Ufisadi unasababisha serikali kufuja hela za walalahoi kwa semina elekezi ambazo hata huhitaji kwenda darasani.
11. Ufisadi unasababisha familia ya viongozi wasio na uadilifu kujilimbikizia mali akiwemo Kikwete.
12. Ufisadi umesababisha vijana wetu wasomi kutaabika kwa kukosa mikopo ya elimu huku Vasco da Gama safari kila kukicha.
13. Ufisadi unasababisha watoto wetu wanakosa elimu ambayo ni haki ya msingi.


Nikiendelea kuandika madhara ya Ufisadi nitajaza pages and pages, lakini Mkuu Mchambuzi anadai haya si ya muhimu, tujadili mengine ya muhimu. Kama hayo mengine unayoamini ni muhimu hayatokani au hayana uhusiano kwa njia moja au nyingine na haya niliyotaja, basi hapo hatuna budi kuacha kuzungumzia ufisadi.

Nafikiri ungejipa masaa 9 kujipima kuona kama unafaa kuwa mchambuzi, husisubiri kupewa ushauri kutoka kwa pacha wako MS ambaye hata akiambiwa kuwa "ndege inaweza kufunga breki angani na kutoa vumbi" atakubali tu huku akijua ni uongo.
 
<br />
<br />
 

Umejibu vyema ndugu Speaker. Ufisadi ni ufisadi tu bila kujali kama mtu yuko serikalini au sehemu nyingine.

Kuhusu ruzuku inayotolewa na serikali kwa CDM, matumizi yake yako wazi. matumizi hayo yamefafanuliwa na Athony Komu katika waraka wake no. C/HQ/ADM/MS/11 WA TAREHE 11/02/2011. KWA HIYO KILA MWANA cdm WA KWELI ATAKUWA ANAJUA NINI ALIANDIKA NA MATUMIZI YOTE YAKO WAZI. Mwache Nape aendelee kupiga domo.

Kuhusu mshahara wa Dr. Slaa, tayari Mwenyekiti aliishatoa ufafanuzi wiki iliyopita tena mbele ya vyombo vya habari. Kwa hiyo makamanda, msiwe na hofu wala wasiwasi. Endelea kupambana... Hakuna kulala mpaka Kieleweke.
People's ........... Power
 
Aliyeshindwa hakosi sababu, alinyimwa cheo chadema fasta akapewa wilaya sasa anadhan akilopoka pumba atapewa urais! Tatizo kubwa alilonalo anaongoza ccm
yenye makund makuu mawili mbumbu sanaa na welevu lakn walio wezi balaa! Akiongea pumba wanampuuza kwa kumpigia makofi huku wakitaka muda uzid kupita lakn wale mbumbu tutawakomboa kwa kuwapa elimu ya kiraia wajitambue waikomboe nchi yao. Kumbuken ruzuku ya chadema hata m500 haikufika kwa kipind kilichopita je hizo zingetutoa matopen hata kama chadema wasingepewa ?
 
jamani nape ni vuvuzela kweli...yaani ni watu wanaosimama na kuongea pumba tu....yaani ni zaidi ya mjinga, tena namfananisha na mbunge jirani yangu wa arusha town (Lema) wote hawa wanaenda kwa upepo jamani, wakisimama majukwaani hakuna jipya zaidi ya unafiki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…