Nashangaa watu wanavyomsifu Pole pole but me sion kazi waliyofanya kwenye chama chetu hiki ye na mwemzake
Nape na Kinana waliipambania CCM 2015 kabla ya uchaguzi walizunguka nchi nzima wakipambana na kurudisha uhai wa chama huku wakikagua mirad iliyokuwa kwenye ilan ya chama
Nape na mwenzake walipambana na upinzani ukiwa wa moto
Hawa pimbi wawili Pole pole na Bashiru wamefanya nn zaid ya kuua upinzani kwa mabavu(kwa mamlaka ya kidikteta ya Mwendazake) na kununua wapinzani
Wapi waliimarisha chama au kupambania chama zaid ya kupambana kuua upinzani?
Nakuuliza wewe chuki binafsi!
Kwamba !
Kinana (mzee wa kusafirisha ndovu)
Na
Nape
(Mzee wa goli la mkono).
Walikuwa wanafufua chama kilichouwawa na nani?
Wauwe wao halafu wafufuwe wao?
Muwe mnatunza kumbukumbu vizuri.
Bashiru aliongoza tume iliyoundwa kukusanya na kuorodhesha mali zote za CCM.
Mmojawapo wa watuhumiwa waliokutwa na ubadhirifu mkubwa ni huyo Nape Nauye ambaye alikuwa ameficha mpaka V8 mpya za chama nyumbani kwake.
Achilia mbali uuzwaji wa kifisadi mitambo ya Tanzania printpark na Chanel Ten TV.
Yoote hayo JPM alisamehe.
Huyu Kinana yeye alifikia mahali mpaka akasajili meli na kuitumia kusafirisha meno ya tembo toka nchini kwenda ughaibuni.
Mpaka pale ilipokamatwa na Interpol .
Sauti za yeye kumkashifu marehemu JPM zilivuja mitandaoni,lakini JPM alisamehe.ingekuwa ni huyu mama sijui ingekuwaje?
Yule Bulembo yeye shule za iliyokuwa TAPA, jumuia ya wazazi aliziuza kama mali yake.
Mfano hai kule Musoma kuna kesi iko mahakamani hivi tunavyoongea. Ni sekondari ya Isango.
Sasa hawa leo ndio watetezi wa Mh Samia?
Ushindi mkubwa wa kihistoria kwa CCM ulitokea chini ya uongozi wa hao unaowaita Mapimbi.haijawahi kutokea.
Watanzania tuna laana ya wizi unafiki, na uvivu na hatupendi ukweli na wakweli wake.
Huo ndio uhalisia
....acheni kuishi kwa visasi
2025 sio mbali na hakika CCM na mama yao huyu watawajua Watanzania wa leo.
MUNGU IBARIKI AFRIKA NA UWABANIKE WANAFIKI WA AFRIKA.
[emoji1241] TANZANIA IWE NA AMANI mengine yatajinyoosha yenyewe kama ambavyo katiba mpya inaelekea kujileta yenyewe.
[emoji120][emoji1241][emoji288]