Nape muasi namba moja CCM - Nangole

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,524
13,098
Saturday, 15 October 2011

HALI imezidi kuwa tete ndani ya CCM na sasa mpasuko ambao umekuwa ukitajwa kukigawa chama hicho kikongwe nchini ni dhahiri. Hali hiyo inatokana na hatua ya makada na viongozi wake waandamizi kurushiana maneno makali nje vikao vyake rasmi kama ambavyo awali kilikuwa kimejenga msingi imara wa taratibu za kumaliza mambo yake ya ndani kimyakimya.

Jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole aliibuka na kumshambulia hadharani Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye akimwita: "Muasi namba moja." Nangole alikuwa akijibu kauli ya Nape aliyoitoa wiki hii akisema ndani ya chama hicho kuna kundi la waasi wanaokihujumu chama na hasa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Akijibu shutuma hizo jana, Nape alisema: "Ukirusha jiwe kwenye giza, halafu ukasikia mtu akiguna ujue huyo ndiye uliyemponda. Sasa mimi kwenye press release (taarifa kwa vyombo vya habari) sikutaja jina la mtu wala mkoa, sasa iweje yeye leo aanze kujibu?"

"Ninamheshimu sana Mzee Nangole lakini sidhani kama waliomshauri kutoka wamemshauri sawasawa, kama anaweza namshauri akasome taarifa yangu halafu aje tena kwenye press (vyombo vya habari), atazungumza vizuri," alisema Nape.

Malumbano hayo baina ya Nangole na Nape wote wakiwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), yamekuja siku moja tu tangu mwanasiasa mkongwe nchini, Jaji Joseph Warioba alipovionya vyama vya siasa nchini hususan chama hicho tawala kutokana na kile alichokiita kuwa ni "kukosekana kwa nidhamu ya kuzungumza."

Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1), Warioba alisema hali katika vyama vya siasa inasikitisha kwani kumekuwa na malumbano makali baina ya viongozi.

Jaji Warioba aliyepata kuwa Waziri Mkuu alisema hali hiyo inakiathiri zaidi CCM ambacho ni chama tawala na akahoji sababu za kuachwa kwa misingi ya mwanzo ya kuzungumza kwa nidhamu mambo yanayokihusu chama hicho.

"CCM kinaathirika zaidi na hali hii ya kutokuwepo kwa nidhamu ya kuzungumza ndani ya vyama, maana chenyewe kiko madarakani, unashangaa kimetokea nini kwa chama ambacho kilikuwa na nidhamu ya hali ya juu ya kuzungumza," alisema Warioba.

Kauli ya Nangole
Nangole katika mkutano wake na waandishi wa habari jana alimtaka Nape aachane na malumbano yasiyo na tija ndani ya chama na badala yake asisitize utekelezaji wa Ilani ya CCM kwani malumbano hayo yanaashiria dalili mbaya za anguko la chama hicho siku zijazo.

Alimtaka Nape ajikite kutangaza mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na chama hicho badala ya kuendeleza malumbano kila kukicha.

"Tufanye shughuli za kukijenga chama. Mimi nilidhani Nape atakuwa akisisitiza utekelezaji wa Ilani za chama lakini yeye kila siku ni 'gamba, gamba tu.' Haya yatatufikisha wapi? Watu wanataka maendeleo," alisema Ole Nangole. Alisema ndani ya CCM kwa sasa kumekuwa na makundi mbalimbali ambayo yanasigana bila tija huku akionya kuwa dalili hizo za makundi zitaifikisha pabaya.

Akizungumzia kauli ya Nape kwamba kuna uasi ndani ya CCM, Mwenyekiti huyo wa Mkoa alisema ikiwa ni kweli, basi uasi wa kwanza ulifanywa na Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM, kwani aliwahi kutajwa kuwa mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ).

Alisema mara kwa mara Nape amekuwa akituhumiwa na baadhi ya makada wa chama hicho akiwamo aliyewahi kuwa Mbunge wa Kishapu, Shinyanga, Fred Mpendazoe kuwa ni miongoni waanzilishi wa CCJ na hivyo kutamka kuwa kama ni suala la uasi basi Nape huenda akawa wa kwanza kuasi CCM.Ziara ya UVCCM
Mwenyekiti huyo alipongeza ziara iliyofanywa na wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) hivi karibuni mkoani Arusha, ambayo kimsingi ndilo chimbuko la malumbano yanayoendelea hivi sasa.

Alisema ziara hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa ilipaswa kupongezwa kwa kufufua uhai wa chama wilayani Arusha badala ya kubezwa hasa ikizingatiwa kuwa wakati huu, chama cha upinzani, Chadema kimeweka himaya yake maeneo mengi ya Mkoa wa Arusha.


Hata hivyo, alisema chanzo cha migogoro hiyo ni chuki mbalimbali ndani ya CCM zinazosababishwa na vita ya urais mwaka 2015 na kwamba huenda ikakimaliza chama hicho kwa kukiweka pabaya kwenye uchaguzi huo.

"Chuki zote za kuchafuana ni maandalizi ya 2015 na hili ndilo linachangia kutumaliza. Hebu tutekeleze Ilani ya chama. Nawapa pole wanaosaka urais kwa sasa kwani bado mbali sana," alisema.

Kauli ya Nape Kwa upande wake, Nape alikanusha kuzungumzia ziara ya UVCCM Arusha katika mkutano wake na waandishi wa habari: "Naomba nieleweke, sijawahi kuzungumzia ziara ya umoja wa vijana mkoani Arusha, kwa hiyo madai yoyote yanayohusiana na suala hilo si yangu kwa sababu wanataka kunihusisha na jambo ambalo sihusiki nalo."

"Kama nilivyosema sikutaja jina la mtu wala mkoa, sasa kwa nini leo hii wasijibu wenyeviti wa Mwanza, Shinyanga, Morogoro au kwingineko na ajibu yeye?"

Kuhusu mbio za urais wa 2015, Nape alisema: "Sijui kwa nini haya mageuzi ya kujivua gamba yanapotajwa yanahusishwa na urais. Hili si sahihi hata kidogo. Kwa mfano, unanihusisha mimi Nape na wagombea watano, hata kama ningekuwa nashabikia hili, nitakuwa vipi na wagombea wote hawa?,"


Alisema Sekretarieti ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama imekuwa na kazi nyingi za chama na si kutafuta mgombea wa urais wa 2015 na kwamba hao pengine wanaolizungumza kila wakati ndiyo wenye wagombea wao.

Alipoulizwa CCM kutokuwa na utaratibu wa kutoa taarifa Nape alijibu: "Sasa ninyi mngekuwa mkinisaidia kuwahoji hao, kwamba wanazungumza kama kina nani, maana utaratibu wa chama unaeleweka na msemaji wa chama anafahamika."

Kauli nyingine
Oktoba 12 mwaka huu, Nape aliwaambia waandishi wa habari kuwa kumeibuka kundi la watu wenye nguvu ya fedha wanaokisaliti chama kwa kuendesha propaganda za kupotosha dhana ya kujivua gamba.

Alisema kundi hilo linamhujumu pia Rais Kikwete lakini akasema chama kimejipanga kuwashughulikia wanaounda kundi hilo.

Alipotakiwa kutaja hujuma za kundi hilo dhidi ya Mwenyekiti wa CCM, Nape alisema: "Ni nyingi, moja ni kusambaza hoja ya kutaka nafasi ya urais itenganishwe na ile ya mwenyekiti wa chama."

Nape ilitoa matamshi hayo siku chache tangu Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa atoe kauli ya kukikosoa chama na Serikali yake akiwataka makada wa CCM kuacha kuingilia siasa za Chadema na pia kuitaka itafute suluhu ya matatizo yanayokabili wananchi.

Benno alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara Mjini Arusha, eneo ambalo linaonekana kuwa chimbuko la malumbano yanayoendelea hivi sasa ndani ya CCM.

Mkutano huo ndiyo pia chimbuko la tukio la Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya kusakwa na polisi kwa tuhuma kwamba alitoa matamshi yenye kuchochea vurugu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema jeshi hilo linamsaka Ole Millya kuhusu kauli yake kwamba mtoto mmoja wa kigogo alitoa maagizo kwa polisi kuzuia UVCCM wasifanye mkutano siku hiyo.

Msuguano wa ndani
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na misuguano ndani ya chama hicho, huku kukiwa na kundi ambalo linadaiwa kuwa na ajenda dhidi ya utekelezaji wa falsafa kujivua gamba iliyopitishwa na NEC ya CCM ikiwataka watuhumiwa wa ufisadi kuachia nyadhifa zao.

Habari kutoka ndani ya CCM zinasema kundi hilo la waasi linaungwa mkono na wenyeviti wa CCM wa mikoa zaidi ya 10 na kwamba ndilo linalosukuma ajenda ya kutaka kutenganishwa kwa kofia ya Rais na Mwenyekiti wa CCM.

Habari zaidi zinasema kuwa baada ya uchaguzi wa Igunga, kundi hilo lilipata nguvu zaidi kutokana na kuanza kuungwa mkono na mmoja wa makada wa siku nyingi wa chama hicho kutoka moja ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Miongoni mwa mikakati ya kundi hilo ni kuhakikisha ajenda ya kuteganishwa wa nafasi hizo mbili inafanikiwa, kufutwa kwa mpango wa kujivua gamba na kumng'oa Nape katika nafasi yake ya sasa kwa madai kwamba anakiharibu chama.


Habari hii imeandikwa na Moses Mashalla, Arusha na waandishi wetu Dar (Mwananchi)
 

BBJ

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
1,183
159
tehe..tehe..teheee....!!MAGAMBA yanazidi KU PARAGANYIKA..watu waliowaua Igunga na kwingineko bila hatia damu yao imeanza kufanya kazi,na bado!
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,711
7,151
Guuuuud Nyuuuuuzi....najihisi niko peponi mahala palipo juu kwa KUPASUKA huku kwa kishindo kwa chama cha mahustler wanaoendesha umafia hapa Tanganyika

Hata Roman Empire finally ilipasuka!
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,524
13,098
Hicho kikao cha halmashauri kuu kitawaka moto.Inadaiwa makundi yote mawili yana nguvu sawa,pia makundi yote yana tofauti ambazo ni vigumu kukaa pamoja tena.
 

WILLY GAMBA

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
211
87
Naungana na Mzee Warioba kuhusu mfumo wa kutoa taarifa za kichama, kila mtu anaongea lakini anaetakiwa kudhibitiwa ni huyu Nape, abadili mfumo wake wa kutumia na maneno ya kejeli kwa Magamba. Atumie academic approach - sio mafumbo na vijembe mpaka magamba yamechukia na yamegoma kutoka sababu yamedhalilishwa kiasi cha kutosha.
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Mkuu CCM wamefikia mwisho na wameona mwenye afadhali na mvuto ni Nape sasa unategemea wafanya mabadiliko lini tena .Acha wakabane tu .
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,524
13,098
Nape asipokuwa makini kundi la wapinzani wake litamuondoa kwenye nafasi yake.
 

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,680
249
Naungana na Mzee Warioba kuhusu mfumo wa kutoa taarifa za kichama, kila mtu anaongea lakini anaetakiwa kudhibitiwa ni huyu Nape, abadili mfumo wake wa kutumia na maneno ya kejeli kwa Magamba. Atumie academic approach - sio mafumbo na vijembe mpaka magamba yamechukia na yamegoma kutoka sababu yamedhalilishwa kiasi cha kutosha.

Fafanua usemi wako juu ya kuungana na Warioba, Kwani Warioba na wewe hamjui kuwa Nape ni nani CCM sasa mnataka nani atoe taarifa za CCM.Nyie wote mnashabikia Magamba sijui yanawapa nini,ila mtashindwa tu subirini mda utatupa jibu.
 

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
1,014
613
Nape asipokuwa makini kundi la wapinzani wake litamuondoa kwenye nafasi yake.

Inasemekana yeye ndiyo alikuwa anahudumia GREEN GUARD huko Singida ndio maana hakuende kwenye kampeni Igunga. Huyu kijana ni mnafiki sana tunamkumbatia ni kijana mwenzetu kumbe anataka kutumaliza. Moto anao sijui atauzima vipi.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Itakuwa furaha sana kama ccm wataenda na mwendo huu huu mpaka 2015.
 

Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
Mnaijua sera ya ccm ya tukose wote??
Mnaweza mkashangaa wakaamua mwenyekiti awe mwanamke...wakampa Anna Abdala, halafu come 2015 wakampa takataka kama Kigoda kuwa mgombea wao...hawa ni vichaa hawa, na ndio mtaji wa CHADEMA.
 

Mzalendo80

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
2,509
1,334
Nape sasa ndio atakayekisukuma chama cha Magamba makaburini, watanzania sasa ndio wakati muafaka wa kukizika. tusmsubirie Nape atuletea Makaburini sisi tumalize kazi.
 

WILLY GAMBA

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
211
87
Fafanua usemi wako juu ya kuungana na Warioba, Kwani Warioba na wewe hamjui kuwa Nape ni nani CCM sasa mnataka nani atoe taarifa za CCM.Nyie wote mnashabikia Magamba sijui yanawapa nini,ila mtashindwa tu subirini mda utatupa jibu.
Kaka mimi ni Gwanda..ila nguvu yetu CHADEMA inasaidiwa na Nape anapo watukana Mapacha, Naomba hayo magamba yasiachie
 

WILLY GAMBA

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
211
87
Naomba magamba mtusaidie kwa hili- endeleeni kuvurugana na EL na Chenge na msimbadilishe Nape nafasi yake maana wanaweza kumweka mtu mwenyewe akili timamu mpaka2015
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom