Nape muasi namba moja CCM - Nangole

Nape muasi namba moja CCM - Nangole

[QUOTE

=fmpiganaji;2649094]Nape asipokuwa makini kundi la wapinzani wake litamuondoa kwenye nafasi yake.[/QUOTE]
hawezi kuondoka ila cha moto anakiona,bila kumungunya maneno ukweli nape anajitahdi na ana moyo wa kufanya kazi aliyopewa.,penye ukweli tuseme ANAJITAHIDI na daima MWENYEZI MUNGU YU PAMOJA NAYE
 
Nakubaliana na Nangole. Kama uasi kwa Kikwete, basi Nape hawezi kuwa nje.

TANGU taarifa kwamba spika wa zamani wa Bunge, Samwel Sitta na Dk. Harrison Mwakyembe, ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa Chama cha Jamii (CCJ) ziibuke, mjadala mkubwa umekuwepo ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Makundi mawili yamechomoza. Wale wanaoshinikiza chama kuwafukuza uanachama wote waliohusika na uanzishaji wa CCJ, wakati wakiwa bado wanachama na viongozi wa CCM.

Wapo pia wanaowatetea kina Sitta na kutaka chama kupuuza madai hayo.
Mbali na Sitta na Dk. Mwakyembe wengine wanaotajwa kuwa waanzilishi wa CCJ, ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kada wa chama hicho, Daniel ole Porokwa na mwenzake Paulo Makonda.
Wanaotetea wale wanaoitwa "wasaliti wa ndani ya chama," wamejenga hoja kuu tatu kuhalalisha hoja yao.

Kwanza, kwamba shutuma hizo si za kweli, kwa hoja kuwa majina ya wote waliotajwa hayapo kwenye kitabu cha Msajili wa Vyama vya Siasa.

Pili, aliyekuwa mwenyekiti mwanzilishi wa CCJ, Richard Kiyabo amekana kuwafahamu Sitta, Dk. Mwakyembe na Nape katika kilichokuwa chama chake.

Tatu, hoja ya kuanzishwa CCJ, ni hoja mfu. Kwamba suala hilo limepitwa na wakati; na kwamba tayari msajili wa vyama alifuta chama hicho. Tuanze kujadili hoja mojamoja. Kwanza, kutokuwapo kwa majina ya watuhumiwa kuanzisha chama katika daftari la msajili wa vyama vya siasa. Hii si hoja yenye mashiko na haitoshi kuwa ni utetezi. Rostam Aziz, mmoja wa watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini, anamiliki makampuni mengi, lakini hakuna hata kampuni moja ambako jina lake linaonekana.

Hata hivyo, nani anaweza kutetea Rostam kuwa si mshirika kwenye wizi uliofanywa na makampuni ya Kagoda, Richmond na sasa Dowans?
Kikubwa cha kuangalia hapa, ni kwamba tuhuma hizi zimetolewa na watu waliokuwa wanafahamu kwa undani uanzishwaji wa CCJ.
Fred Mpendazoe, mbunge wa zamani wa Kishapu (CCM) na swahiba mkubwa wa Sitta na Dk. Mwakyembe, alishiriki katika hatua zote muhimu za kuanzisha chama hicho. Naye Porokwa amethibitisha kuwa CCJ, ni mali ya Sitta na Mwakyembe.

Aidha, mkakati wa kuficha majina unaweza kuwa ulilenga kutojulikana mapema, hasa ukizingatia kwamba wahusika walikuwa bado ni wabunge na watumishi katika chama na hivyo, wangependa kwanza wamalize kipindi chao cha ubunge ili wasipoteze mafao yao na hata kuharibu mpango.
Pili, kuhusu kauli ya Kiyabo, kwamba wahusika hawakuwa waasisi wa CCJ, nayo haiwezi kuaminiwa.

Kwanza, ni Kiyabo huyuhuyu aliyekuwa anahubiri kuwa chama chao (CCJ) kinaundwa na viongozi waandamizi ndani ya CCM.
Je, kama hao waliotajwa si miongoni mwao, wako wapi basi wale aliopata kuwaita wakati huo kama "viongozi waandamizi ndani ya CCM?"
Kwa wanaomjua Kiyabo wanafahamu kuwa tokea aliporejea chama hicho, Agosti mwaka jana, maisha yake yote yamekuwa yakitegemea CCM.
Hivyo katika hali ya kawaida, ilitarajiwa kuwa Kiyabo hawezi kuwataja wanaomfadhili hadi hapo Nape na wenzake watakaposhindwa kumwezesha.
Tatu, hoja kwamba CCJ haipo na hivyo hakuna sababu ya kujadili "waasisi," haiingii akilini. Kukubali hoja hiyo ni sawa na kusema waliokamatwa kwa uhaini wa kutaka kupindua serikali waachiwe kwa kuwa serikali haikupinduliwa. Ni sawa basi tuseme mwamuzi asimuadhibu mchezaji aliyemchezea rafu mwenzake mchezoni eti kwa sababu tu aliyelengwa hakuumia. Hatwendi hivyo.

Hoja kuu hapa kama alivyoeleza mchambuzi maarufu wa gazeti hili, Kondo Tutindaga, ni kule mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete kuzungukwa na vigeugeu, wasaliti na watu wanaoweza, wakati wowote, kukihujumu chama na yeye mwenyewe.
Kama walithubutu kutumia rasilimali za chama na serikali na kutumia madaraka waliyopewa na chama kukihujumu chama, kwa maslahi ya binafsi ya kufanikisha mipango ya kuanzisha CCJ, watashindwaje kumhujumu Kikwete? Inawezekana kwa sababu nia yao ya kuanzisha chama cha kukitoa madarakani CCM ilishindikana mwaka jana, lakini nani anaweza kueleza kuwa mpango huo hautaweza kufanyika tena?
Kwa nini tusiamini kuwa hata hicho kilichokuwa kinafanyika wakati huo – kuimega CCM vipande viwili – ndicho kinachofanyika sasa ili kurahisisha mpango wao wa kuiondoa CCM madarakani?

Hili linathibitishwa na matamshi ya Samwel Sitta kuwa mazungumzo na vyama vingine katika masuala ya siasa, ni jambo la kawaida.
Kama ni suala la mazungumzo hilo si tatizo. Lakini kilichoendelea hakikuwa mazungumzo; ulikuwa ni mkakati wa kuanzisha chama na wahusika hawakuwa wanachama wa kawaida. Ni viongozi waandamizi ndani ya CCM. Kama Kikwete anakitakia mema chama, ni muhimu akalizingatia hili. Vinginevyo, muda si mrefu umma utashuhudia akiachwa njiani na wale anaoonekana kuwaamini.

Mwandishi wa makala hii, amejitambulisha kuwa ni msomaji wa MwanaHALISI. Anapatikana kupitia imeili: allimussa@hotmail.com
 
TUHUMA za kukisaliti chama zinazowakabili spika wa zamani wa Bunge, Samwel Sitta na mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, zaweza kuwafukuzisha kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM), MwanaHALISI limeelezwa.
Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki na Dk. Mwakyembe wametajwa kuhusika na uanzishaji Chama cha Jamii (CCJ) wakiwa bado wanachama na viongozi katika CCM.
Aliyekuwa wa kwanza kutaja majina ya viongozi hao ni Fred Mpendazoe aliyekuwa mbunge wa Kishapu. Alihama CCM Aprili mwaka jana akituhumu chama hicho kukumbatia mafisadi na kupoteza mwelekeo.
Mpendazoe aliuambia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Njombe wiki iliyopita kuwa yeye, Sitta na Mwakyembe ndio walianzisha CCJ; bali yeye alitangulia kutoka CCM ili kurahisisha usajili wa chama hicho. Wenzake walikuwa wamfuate baadaye.
Wengine ambao Mpendazoe alitaja kuwa waanzilishi wa CCJ ni Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye. Alisema walianzisha chama hicho ili kipokee wanachama waliokuwa wanapinga ufisadi ndani ya CCM na ambao ingekuwa vigumu kwao kupitishwa kugombea ubunge.
Tuhuma kubwa zinazowakabili Sitta, Mwakyembe na wenzao ni utovu wa uaminifu na usaliti kwa kuanzisha chama ndani ya chama.
Wakati hao wametajwa hivi karibuni, Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge tayari wamethibitishwa na vikao kuwa wamedhoofisha chama chao mbele ya jamii na kusababisha kisifanye vema katika uchaguzi mkuu uliopita.
Dk. Hassy Kitine, mmoja wa makada wa CCM anasema, tuhuma za kuanzisha chama ndani ya chama ni kubwa na kwamba iwapo CCM inataka kuaminika mbele ya wananchi, sharti ifanyie kazi tuhuma hizo.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano ambayo yatachapishwa kwa ukamilifu katika toleo lijalo, Dk. Hassy Kitine amekitaka chama chake kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ushahidi wa tuhuma zote zinazowakabili viongozi wake.
"Kuhusu hili la hawa walioanzisha chama ndani ya chama; na wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi, ni lazima chama chetu kitafute ushahidi wa kutosha na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika kufuatana na katiba na taratibu za chama," ameeleza.
Dk. Kitine ambaye aliwahi kuwa waziri wa utawala bora wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, mkurugenzi wa usalama wa taifa, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anasema kuanzisha chama ndani ya chama ni kosa ambalo haliwezi kuachwa bila kutolewa maelezo.
"CCM isifanye parapara. Pamoja na kwamba kumfukuza mtu ndani ya chama ni hatua kubwa. Lakini utafutwe ushahidi; ikithibitika kwamba hawa watu walishiriki katika kuazishwa kwa chama wakiwa bado ndani ya CCM, basi wawajibishwe," ameeleza.
Anasema, "Ushahidi huu lazima ueleze ushiriki wa kila mmoja. Ukipatika wote wafukuzwe."
Anasema CCM hakiwezi kuwafukuza watuhumiwa wa ufisadi kikawaacha wanaotuhumiwa kukidhoofisha kwa kuanzisha chama ndani ya chama.
"Wote washughulikiwe kwa mujibu wa taratibu za chama chetu. Wapewe nafasi ya kujitetea. Umma uridhike kwamba haki imetendeka na wao wajiridhishe kuwa wametendewa haki. Kisha chama kiamue kufanya maamuzi magumu ya kuwafukuza," ameeleza.
Anasema, "Na hili ni kwa wote, wakiwemo wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi. Hapo ndipo chama chetu kitakapolinda hadhi na heshima yake mbele ya wanachama na wananchi wengine kwa jumla."
Kauli ya kutaka kufukuzwa waasisi wa chama ndani ya chama imekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Nape Nnauye ni miongoni mwa waazilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ).
Wachunguzi wa mambo ya kisiasa walitafsiri hatua ya akina Sitta kuwa ni kumweka Rais Kikwete katika wakati mgumu wa vyama viwili vya siasa katika utawala mmoja, mithili ya serikali shirikishi ya umoja wa kitaifa.
Sitta ni Waziri wa Afrika Mashariki na Mwakyembe ni naibu waziri wa ujenzi; naye Nape ni msemaji wa CCM. Wengine waliotajwa katika CCJ ni Daniel ole Porokwa, katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi Mjini na Victor Mwambalaswa, mbunge wa Lupa.
Jumapili iliyopita, Porokwa aliweka wazi ushiriki wake katika kuasisi CCJ na kushindilia akina Sitta kuwa walikuwa pamoja naye.
Katika tamko lake la kurasa nne kwa waandishi wa habari, Porokwa amesema CCJ ni chama kilichoanzishwa na kuasisiwa na Nape, Sitta, Dk. Mwakyembe na Mpendazoe.
Katika taarifa inayoonyesha kuugama, Porokwa anasema, "Nimeamua kuyasema haya ili kuondoa unafiki unaojengeka ndani ya chama chetu na taifa kwa jumla, kwamba kuna kikundi cha watu wanaotaka kupotosha umma juu ya uanzishwaji wa CCJ na ujio wake.
"Nikiwa kada wa CCM niliyefundishwa na kuaminishwa kuwa uongozi ni dhamana na ninayeamini katika misingi aliyotuachia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, nimeamua kuyasema haya ili ukweli ubaki ukweli katika historia ya taifa letu," alisema Porokwa.
Porokwa anasema, "Kuyumba kwa chama chetu na hata kufikia hatua ya kuanza kuporomoka kwa kupoteza nafasi mbalimbali kwa vyama vingine kwa wingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi katika nchi hii, ni kwa sababu ya kuwa na viongozi wenye malengo na ajenda binafsi, tofauti na zile za chama chenyewe."
Amemtaka Rais Kikwete kulitazama suala hilo kwa undani kwa kile alichodai "…katika timu yake, kuna wachezaji ambao wako tayari kujifunga na kuinyima timu yao ushindi."
Anasema, "Ni maoni yangu kwa dhati kabisa na rai yangu kwa viongozi wa chama changu, kwamba ni wakati mwafaka sasa umefika kwa watu kama hawa wawajibike au wawajibishwe kutokana na matendo yao."
Porokwa ambaye amejitambulisha kwa maneno na vitendo kuwa ni kutoka kundi la Edward Lowassa anasema, mbali na kusukumwa na mapenzi ya chama chake katika kutoa ushuhuda huo, ushahidi anaoutoa unalenga kuonyesha kuwa Sitta, Dk. Mwakyembe na Nape, ni wasaliti.
"Hawa ninaowataja, si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe…," anaeleza.
Anasema, "Na hili la Mpendazoe ambaye alikuwa mbunge, akaacha mishahara kadhaa na mafao yake kwa makubaliano ya kazi ya pamoja ambayo nilishirikishwa katika hatua za awali na mwisho wake wakamtosa na sasa wanamkana hadharani, ni moja ya sababu iliyonisukuma sana kutoa ushuhuda huu."
Naye mjumbe wa NEC na mwenyekiti wa baraza la wadhamini la CCM, Peter Kisumo pamoja na kutoingia kwa undani kuzungumzia suala hilo amesema, "Wanaotajwa kuanzisha CCJ, zamu yao ikifika watashughulikiwa."
Hata hivyo, Kisumo amesema suala la kuanzishwa kwa CCJ linaweza kuonekana halina maana yoyote kwa sasa, lakini sharti uchunguzi ufanyike na wanaohusika wachukuliwe hatua.
Mchambuzi maalum wa gazeti hili, Kondo Tutindaga ananukuu Nyerere akishupalia baadhi ya wana-CCM waliounga mkono hoja ya kuunda Tanganyika pale walipochukua fomu kugombea urais mwaka 1995.
Anamnukuu Nyerere akisema mwaka 1995 walikuwa wanatafuta rais wa Tanzania na siyo Tanganyika; na kwamba wanaotaka urais wa Tanganyika wasubiri.
"Ni kwa msingi uleule…Kikwete aweza kuwaambia waanzilishi wa CCJ walio ndani ya CCM, kuwa waondoke wakaunde CCJ ili iwe rahisi kwao kutekeleza madhumuni yao. Hata kama chama si mama, lakini pia chama si koti la kuvaa na kuvua kila unapohisi kero ya joto au baridi," anaeleza mchambuzi huyo.
Kwa kuwa sasa ni dhahiri CCJ ilianzishwa na wana-CCM waliokerwa na sera za CCM, pamoja na kiongozi wake, yaani Rais Kikwete, sisi tulio wana-CCM msimamo, tuna mashaka na viongozi wa namna hii.
Walioanzisha CCJ, mwandishi anasema, "…si wanachama wa kawaida, bali viongozi waandamizi ndani ya CCM. Usaliti wa namna hii, siku moja utazaa uhaini."
 
Nape sasa ndio atakayekisukuma chama cha Magamba makaburini, watanzania sasa ndio wakati muafaka wa kukizika. tusmsubirie Nape atuletea Makaburini sisi tumalize kazi.

Ccm ni chama kilichojengeka kitaasisi zaidi,kwa hiyo haitaweza kusambaratika kirahisi kama hivi vyama ovyo,kumbukeni kuwa mtanzania yoyote anaetaka huduma huanzia kwa balozi na asilimia tisini ya mabozi w shima ni ccm so swala la ccm kusambaratika ni hadithi za kufikirika
 
Ccm ni chama kilichojengeka kitaasisi zaidi,kwa hiyo haitaweza kusambaratika kirahisi kama hivi vyama ovyo,kumbukeni kuwa mtanzania yoyote anaetaka huduma huanzia kwa balozi na asilimia tisini ya mabozi w shima ni ccm so swala la ccm kusambaratika ni hadithi za kufikirika

Ukianza kunywa damu za watu (kuua) ujue huo ndio mwanzo wa kusambaratika. CCM tutakuja kuisahau sio kusambaratika tu.
 
Ccm ni chama kilichojengeka kitaasisi zaidi,kwa hiyo haitaweza kusambaratika kirahisi kama hivi vyama ovyo,kumbukeni kuwa mtanzania yoyote anaetaka huduma huanzia kwa balozi na asilimia tisini ya mabozi w shima ni ccm so swala la ccm kusambaratika ni hadithi za kufikirika

Inaelekea hujui historia au hutaki kuikumbuka. Awali Tanganyika ilikuwa nchi ya vyama vingi. Mwaka 1965 baada ya Muungano na nchi kuitwa Tanzania serikali ya Mwalimu Nyerere ilivifunga vyama vya siasa vyote vingine na kutangaza kuwa Tanzania ni nchi ya chama kimoja. Baada ya hapo ndipo chama kilipoanzisha mashina ya nyumba kumi kumi na kuwa na wajumbe wa nyumba kumi au wenyeviti wa mashina ambao walikuwa ni viongozi wa chama cha TANU. Baadaye TANU ilipoungana na ASP na kuzaa CCM wale wajumbe wa mashina wakawa viongozi wa mashina ya CCM ya Nyerere.

Leo tuko kwenye mfumo wa vyama vingi tangu 1992. Suala la wakuu wa mashina kuwa ni viongozi wa ccm ni sababu ya historia tu, walikuwepo na bado wapo, kwa kuwa katiba haijabadilishwa na sehemu yao haijapatiwa ufumbuzi wa kisheria tofauti na uliokuwepo. Hiyo siyo sababu ya kufikiri kuwa leo hii chama cha magamba bado kina nguvu. Kumbuka kuwa CCM ilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na ilikubalika na nchi nzima kwa kuwa ilikuwa inatetea maslahi ya wafanyakazi. Nyerere aliwahi kusema bei ya mahindi itapanda ili mkulima apate pesa zaidi, lakini bei ya unga unaotokana na mahindi hayo hayo ambayo yamenunuliwa kwa wakulima yakakobolewa na kusagwa na National Milling Corporation haitapanda asilani. Hii ni kumfanya mfanyakazi aweze kumudu hali ya maisha. Bei ya mahindi, sukari, maharage, nafikiri hata mafuta ya taa enzi za Mwalimu ilikuwa inahakikishwa kuwa haitapanda, ili mfanyakazi ambaye ndiye mtaji wa CCM ya Nyerere aweze kumudu gharama za maisha. Lakini ili mjulima aweze kumudu gharama za maisha, bei za mazao yake zilikuwa zinaongezwa kila mwaka. Huo ulikuwa mtaji wa chama.

Leo hii sio CCM bali ni ccm. Sio Chama cha wakulima na wafanyakazi bali ni chama cha mafisadi. Mkulima gani leo hii au mfanyakazi gani leo hii analindwa na ccm? Usihesabu kuna mashina mangapi ya ccm, jiulize kuna watu wangapi wanaofaidika na chama cha mafisadi? ccm ya JK sio CCM ya Nyerere. Chama kimegeuka kutoka kuwa chama cha kutetea maslahi ya wanyonge na kuwa chama cha kuwatajirisha watu wachache hususan mafisadi na familia zao. Chama hakina mtaji, kimekwisha, haya yote ni mateke ya mfa maji!!!
 
"Nitampiga mchungaji wa kondoo na kondoo wa kundi lake watatawanyika".
Ni mitandao makundi mitandao makundi mpaka 2015.
 
Ccm ni chama kilichojengeka kitaasisi zaidi,kwa hiyo haitaweza kusambaratika kirahisi kama hivi vyama ovyo,kumbukeni kuwa mtanzania yoyote anaetaka huduma huanzia kwa balozi na asilimia tisini ya mabozi w shima ni ccm so swala la ccm kusambaratika ni hadithi za kufikirika

Nakushauri usome kidogo historia kuhusu sehemu zote yalikofanyika mapinduzi. Usitiwe upovu na mtandao wa chama nchi nzima.
 
Na bado mpaka 2015 yatabaki majivu hapo Lumumba, sisi kwetu ni kicheko tu Mungu wetu anatupigania vita ya kuitokomeza CCM.
 
Saturday, 15 October 2011


Kauli ya Nangole
Nangole katika mkutano wake na waandishi wa habari jana alimtaka Nape aachane na malumbano yasiyo na tija ndani ya chama na badala yake asisitize utekelezaji wa Ilani ya CCM kwani malumbano hayo yanaashiria dalili mbaya za anguko la chama hicho siku zijazo.

Alimtaka Nape ajikite kutangaza mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na chama hicho badala ya kuendeleza malumbano kila kukicha.

“Tufanye shughuli za kukijenga chama. Mimi nilidhani Nape atakuwa akisisitiza utekelezaji wa Ilani za chama lakini yeye kila siku ni 'gamba, gamba tu.' Haya yatatufikisha wapi? Watu wanataka maendeleo,” alisema Ole Nangole. Alisema ndani ya CCM kwa sasa kumekuwa na makundi mbalimbali ambayo yanasigana bila tija huku akionya kuwa dalili hizo za makundi zitaifikisha pabaya.

Akizungumzia kauli ya Nape kwamba kuna uasi ndani ya CCM, Mwenyekiti huyo wa Mkoa alisema ikiwa ni kweli, basi uasi wa kwanza ulifanywa na Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM, kwani aliwahi kutajwa kuwa mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ).

Alisema mara kwa mara Nape amekuwa akituhumiwa na baadhi ya makada wa chama hicho akiwamo aliyewahi kuwa Mbunge wa Kishapu, Shinyanga, Fred Mpendazoe kuwa ni miongoni waanzilishi wa CCJ na hivyo kutamka kuwa kama ni suala la uasi basi Nape huenda akawa wa kwanza kuasi CCM.



Habari hii imeandikwa na Moses Mashalla, Arusha na waandishi wetu Dar (Mwananchi)

Namheshimu Nnape lakini kwa kweli maneno ya huyu Mzee ni Mazito mno. Wananchi wanataka waone serikali ya CCM imewafanyia nini na inatekelezaje ahadi zilizokuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya 2010 na zile za papo kwa papo!! Haya malumbano hayana tija kwa CCM hata kidogo. Hii ni mbinu ya upinzani kuifarakanisha CCM na wao kuendele na maandamano na kutangazia wananchi "sumu ya ubaya wa CCM"

Kwa kutumia ujanja wa hali ya juu Upinzani ulianza kwa kuwafarakanisha CCM kwa kuwataja baadhi ya viongozi wake eti mafisadi (The Mwembe yanga List of shame)!! Na CCM ikaingia kichwa kichwa na kuanza kuitana mafisadi, moto ukawaka wakasema mafisadi wavuliwe gamba na tangia hapo hakuna cha kutangaza mafanikio ya CCM katika utekelezaji wa Ilani ya 2010! Katibu Mwenezi badala ya Kueneza Sera za CCM amekuwa akieneza habari za magamba. Hivi kuvuana magamba kulikuwa ni sehemu ya ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010? Au Katibu mwenezi hana la kueneza kwa kuwa Serikali ya Chama chake haijatekeleza hata sehemu moja ya ilani ya 2010? Siamini hilo.

Nadhani kuna watu ndani ya CCM wanataka Chama kifilie mbali na wao wana vyama vyao wanataka viibuke. Malumbano kati ya viongozi wa CCM yana tija kubwa sana kwa Upinzani. Kwa mwendo huu CCM kama itakuwepo hadi 2015 inabidi ijiandae tu kuwa kwenye kundi la vyama vya siasa (Siyo chama cha upinzani) kwa kuwa kitakuwa hoi kama UNIP au KANU! Masikini CCM
 
Nape is very BOGUS. Digrii yake ya India ndiyo imemfikisha hapo alipofika.
 
[QUOTE

=fmpiganaji;2649094]Nape asipokuwa makini kundi la wapinzani wake litamuondoa kwenye nafasi yake.
hawezi kuondoka ila cha moto anakiona,bila kumungunya maneno ukweli nape anajitahdi na ana moyo wa kufanya kazi aliyopewa.,penye ukweli tuseme ANAJITAHIDI na daima MWENYEZI MUNGU YU PAMOJA NAYE[/QUOTE]

HUYO MUNGU ALIYE NA CCM NI MUNGU GANI HAPO NAOMBA UTUJUZE ZAIDI MKUU,MI NAJUA CCM WAPO NA DRAGON AU SATAN
 
nashindwa kuwaelewa washabiki wa ccm kama hawamtaki Nape waandamane 2waone kuwa wapo serious?
 
Ccm ni chama kilichojengeka kitaasisi zaidi,kwa hiyo haitaweza kusambaratika kirahisi kama hivi vyama ovyo,kumbukeni kuwa mtanzania yoyote anaetaka huduma huanzia kwa balozi na asilimia tisini ya mabozi w shima ni ccm so swala la ccm kusambaratika ni hadithi za kufikirika


Haya Bwana kama uelewa wako ni huo basi wewe ni hatari kuliko ukimwi,Hivi hujui kuna vyama vingi duniani ambavyo vilijijenga sana lakini hivi leo vimebakia hoi bin taabani.FIKIRIA KWA KINA
 
Wakati Nape anaingia madarakani na Makamba kuondoka nilidhani tutakosa mtu wa kukimaliza hiki chama CCM,Mungu si athumani kamleta kijana Nape Moses Nnauye...anafanya kazi nzuri ya kuimaliza CCM well done Nape.....
 
Naloona mimi ni kuwa nape anatumikia watu 2 na si chama,kwanza anamtumikia jk kwa maelekezo binafsi ya kutukana watu na pili anatumikia kundi la watu ambalo hajui kati yao nani atakuwa rais 2015,binafsi sioni analofanya kama ni JK kwa uwezo wake na mda uliobaki kufanya kitu ni miujiza karne,ndo mana hata nape na viongozi wengine ndani ya ccm wanatumia mda mwingi kuwatukana wale ambao wanajua wanakubalika zaidi kwa wananchi
 
Back
Top Bottom