Nape: Mlipuko wa bomu la Arusha yawezekana ulipangwa na CHADEMA wenyewe

Nape na Mwigulu, hivi nyie ni binadamu? au ukute tunaongea na maroboti, hivi hata kama kukipenda chama, au pesa ua ukubwa kiasi hicho cha kushinwa kuhurumia roho za watanzania, kamwe hatuta wasahau, hamtafutika kwenye roho za watu wema wa nchi hii
 
Kwa kweli CCM walipaswa kuwepo kwenye maajabu 8 ya dunia.Sasa kama Kiongozi wa juu wa ccm anasema Chadema ndo wahusika wa mlipuko wa bomu kwenye mkutano wao wenyewe,kwa nini serikali yake hiyohiyo inatangaza dau la tsh.100ml kwa atakaewajua wahusika,hii si hadaa ya wazi kwa wananchi?
 
hv inakuaje mtu mzima unaamua kusema uongo wa waz? Yan hata ukimtazama nape uson wakat anayasema hayo,utagundua kuwa dhamira inamsuta yan..MUNGU yupo.
 
Kauli ya ccm hiyo. Kwani unawezaje kutenganisha kauli yake na chama cha magaidi (ccm?)
 
Nimesikia maneno aliyotamka NAPE,Eti wananchi wa Arusha wamechoka na siasa za chadema walipanga kuichagua CCM ,hivyo CHADEMA walilipua bomu ili kuvuruga uchaguzi....inatia hasira,kweli unawafanya watanzania wote hawajui ukweli,ni wajinga mabumbu wasiojua lolote,wakazi wa arusha wanastaili hayo matusi pamoja na msiba mkubwa walioupata?

Nape huna mungu wewe? hujui kufa? utaishi milele wewe?.....NAPE NAPE NAPE mungu si athumani na hukumu yake ipo hapahapa duniani...tusubili tutaona.


Huyo jamaa atakufa kifo kibaya sana!! Tena alaaniwe
 
Nape hajielewi. Tatizo huwa anakurupuka sana kutoa matamko yasiyo na kichwa wala miguu.
 
naona wameamua kulopoka kama kawaida yao, dunia imeshajua udhalimu wa ccm, na ipo siku wataumbuka tu, mungu atawalaani wale wote wanaomwaga damu za wenzao. hili jambo halina muda mrefu tutapata ukweli maana najua mtageukana tu.
Ninakuunga mkono 100% Yaani huyu Nape hadi mdomo wake unanuka. Mbona asijikalie tu kimywa? Haya ni maisha ya binadamu hata kama anawaona wanyama kwa kuwa walikuwa kwenye mkutano wa CDM. Hiyo CCM haiwezi kuchagua viongozi wenye utu? Nape watanzania wameshaelimika. Kuendelea kufikiria kuwa mtatugandamiza forever sii kweli. Itafika siku mtajikuta hoi kuliko KANU ilivyo sasa hivi huko Kenya. Ninakusihi sana Nape sometimes kaa tu kimywa kutunza utu na heshima ya taifa letu. Mungu awalaze pema waliouawa na kuendelea kuwafariji ndugu na jamaa zao. Mungu awaimarishe na kuwalinda viongozi wa CDM wanaendelea kupigania uhuru wa nchi yetu ili iweze kurudisha heshima na utu wake. Baba yetu wa taifa Nyerere tuombee huko kwa Mungu ulipo tusilipoteze kabisa jina la taifa letu ulilolitumikia kwa moyo mweupe.
 
Leo nape amekuwa FBI!!! Yaanu mtu asiyejali maisha ya binadamu mwingine namchukia kama shetani. Shame on you angekuwa amekufa mama yako ungetoa kauli kama hii??!! Lakini yote tunamwachia Mungu ipo siku yatawarudia wenyewe.

Siasa ni nini mbele ya uhai? Mnawaza kuiba tu maana hao watu mnaojidai mnawatetea kumbe mnapanga mipango ya kuwaua!!!!! Kumbe ibilisi anawafuasi wengi hivi
 
wakati mwingine ukimsikiliza nape anayo yaongea unaweza ukafikiri hayupo seriouz..yaani cdm walijipangia wao wenyewe lile shambulizi mmh! hii ni zaidi ya huo upinzani
 
Naombeni mnisaidie,

Hivi Nape anapotoa kauli kama katibu mwenezi anakuwa amediscuss na kukubaliana na viongozi wengine wa chama au anakurupuka tu na kutoa tamko?

Seriously?!!!
Mtu na akili zake unaweza ukaita waandishi wa habari na kutoa kauli kama hiyo kweli tena at this time?!

NIMEMDHARAU sana huyu JUHA!!!kichwa kubwa halina kitu kichwani!!

Sitaki kuamini CCM wametafuta wakaona huyu ndie mtu anaewafaa!!kama ndio hivyo basi hapo chama chote ni mazero

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Nashawishika kuamini Nape haamini katika uwepo wa Mungu wala maisha baada ya kifo, vinginevyo asingeishi maisha anayoishi sasa. Kwake ccm ni zaidi ya Tanzania, na maisha ya watanzania wenzake. Hivi huyu mtu ana chembe ya conscience kweli? Hoja zake zina matobo hata mtoto mdogo anadoubt alichoongea!
NAPE, maisha wa mtu yeyote yana thamani kuliko siasa na uongo unaoendekeza. Na Mungu ninayemwamini atawaweka uchi muda si mrefu. Inauma sana!
 
Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22) -kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.

Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%.

Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka.
2.jpg


Hata wale 27.28% walioamua kuwajaribu wenzetu, tunawatakia kila lakheri, kwani wametumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wanaodhani watawasaidia kufikia malengo yao ya kimaendeleo. Uchaguzi kwenye kata hizi zote umeisha sasa tuwatumikie wananchi.

Kata nne za jiji la Arusha hazikufanya uchaguzi baada ya kuahirishwa kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuka kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema mjini Arusha tarehe 15/06/2013.

CCM tunalaani tukio hilo la mlipuko wa bomu na matukio yanayofanana na hayo katika nchi yetu. Tunawapa pole wale wote walioathirika na tukio hilo.


Ni vizuri serikali ikalichunguza swala hili kwa kutumia muda mfupi na kuhakikisha waliohusika wanapatikana na kuchukuliwa hatua zinazostahili.

Pamoja na kulaani na kuitaka serikali kukomesha vitendo hivi nchini, ni wakati muafaka kwa vyama vya siasa nchini kujitazama upya kwani kuna kila dalili kuwa tukio hili kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari mhe. Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa ni la kupangwa, inawezekana limepangwa na Chadema wenyewe.

Hali ya kisiasa jijini Arusha kuelekea uchaguzi huo ilikuwa wazi kuwa wana Arusha walishaamua kuzirudisha kata hizo nne kwa CCM, hasa baada ya kuchoshwa na maandamano na vurugu za kila siku jijini Arusha.


Aidha kauli za kukata tamaa za viongozi wa Chadema na vitendo vyao ni dalili tosha kuwa tukio hili lilipangwa na Chadema wenyewe.

CCM tunaendelea kusisitiza na kulaani juhudi za wenzetu kujaribu kujenga umaarufu wa chama chao juu ya damu za Watanzania. Juhudi hizi zinapaswa kulaaniwa na wazalendo wote ndani na nje ya nchi.



Tukumbuke asiyekubali kushindwa, si mshindani. Si busara wala uungwana na ni kinyume na utu kutumia majanga ya kutengeneza kama mtaji wa kisiasa.

Lakini CCM tunalaani pia kitendo cha viongozi wa Chadema kujaribu kutumia baadhi ya misiba na majeruhi wa tukio hili kisiasa na mwisho wa siku kwenda kuwatelekeza hospitali baadhi yao baada ya kuwaahidi kubeba gharama zote za matibabu na mazishi.


Tunaipongeza serikali kwa kuingilia kati na kuwasaidia waathirika hawa na kuhakikisha wanapata huduma inayostahili.

CCM inarudia kueleza masikitiko yake kwa waathirika wa tukio hili la kinyama na kikatili lisilostahili kuvumiliwa hata kidogo.


Kama Chama tumeguswa sana na tukio hili pamoja na kulilaani, tunawasihi watanzania tushindane na kutofautiana bila kupigana na kuvunja tunu ya nchi yetu ya amani na utulivu.

Katika demokrasia ya vyama vingi swala la kuvumiliana ni swala la msingi sana katika kufikia ukomavu wa demokrasia hiyo.

Imetolewa;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi.
17/06/2013



CCM tutawatoa madarakani kwa mtutu wa bunduki. That's all I can say. We only need time and space. Tukiamua tunaweza pata ufadhili napotelea mbali acha tuingie msituni coz hii ndiyo njia pekee ya kuikomboa nchi hii kutoka kwa hawa manyang'au ccm. We will eventually take them to justice.
 
Huwa sio kawaida yangu kuzungumzia jina la mtu,hasa wakati ambao sie tunatafakari ni wapi Tanzania aliyotuachia baba wa Taifa hili inapoelekea kwa sasa unaposikia siasa za Guilty politics zinazotolewa na wanaojiita viongozi wa ccm unashindwa kujiuliza hata kama ni siasa huwezi kufikia hatua ya kukosa hata akili ya darasa la pili naamini kauli za watu kuwa ccm are tired,wako tayari kwa lolote katika nchi hii ili kumentain status yao naamini hakika kuwa Nape ni VUVUZELA,anashindwa hata kusoma alama za nyakati kuliko kutumia nguvu nyingi ni bora angejua kuwa hizi ni zama nyingine tunajua,tunaona,na tunaelewa wanachofanya,Their days are numbered.
 
Back
Top Bottom