Nape: Mlipuko wa bomu la Arusha yawezekana ulipangwa na CHADEMA wenyewe

mwambojoke

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
1,059
627
Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22) -kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.

Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%.

Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka.


Hata wale 27.28% walioamua kuwajaribu wenzetu, tunawatakia kila lakheri, kwani wametumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wanaodhani watawasaidia kufikia malengo yao ya kimaendeleo. Uchaguzi kwenye kata hizi zote umeisha sasa tuwatumikie wananchi.

Kata nne za jiji la Arusha hazikufanya uchaguzi baada ya kuahirishwa kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuka kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema mjini Arusha tarehe 15/06/2013.

CCM tunalaani tukio hilo la mlipuko wa bomu na matukio yanayofanana na hayo katika nchi yetu. Tunawapa pole wale wote walioathirika na tukio hilo.


Ni vizuri serikali ikalichunguza swala hili kwa kutumia muda mfupi na kuhakikisha waliohusika wanapatikana na kuchukuliwa hatua zinazostahili.

Pamoja na kulaani na kuitaka serikali kukomesha vitendo hivi nchini, ni wakati muafaka kwa vyama vya siasa nchini kujitazama upya kwani kuna kila dalili kuwa tukio hili kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari mhe. Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa ni la kupangwa, inawezekana limepangwa na Chadema wenyewe.

Hali ya kisiasa jijini Arusha kuelekea uchaguzi huo ilikuwa wazi kuwa wana Arusha walishaamua kuzirudisha kata hizo nne kwa CCM, hasa baada ya kuchoshwa na maandamano na vurugu za kila siku jijini Arusha.


Aidha kauli za kukata tamaa za viongozi wa Chadema na vitendo vyao ni dalili tosha kuwa tukio hili lilipangwa na Chadema wenyewe.



CCM tunaendelea kusisitiza na kulaani juhudi za wenzetu kujaribu kujenga umaarufu wa chama chao juu ya damu za Watanzania. Juhudi hizi zinapaswa kulaaniwa na wazalendo wote ndani na nje ya nchi.


Tukumbuke asiyekubali kushindwa, si mshindani. Si busara wala uungwana na ni kinyume na utu kutumia majanga ya kutengeneza kama mtaji wa kisiasa.

Lakini CCM tunalaani pia kitendo cha viongozi wa Chadema kujaribu kutumia baadhi ya misiba na majeruhi wa tukio hili kisiasa na mwisho wa siku kwenda kuwatelekeza hospitali baadhi yao baada ya kuwaahidi kubeba gharama zote za matibabu na mazishi.


Tunaipongeza serikali kwa kuingilia kati na kuwasaidia waathirika hawa na kuhakikisha wanapata huduma inayostahili.

CCM inarudia kueleza masikitiko yake kwa waathirika wa tukio hili la kinyama na kikatili lisilostahili kuvumiliwa hata kidogo.


Kama Chama tumeguswa sana na tukio hili pamoja na kulilaani, tunawasihi watanzania tushindane na kutofautiana bila kupigana na kuvunja tunu ya nchi yetu ya amani na utulivu.

Katika demokrasia ya vyama vingi swala la kuvumiliana ni swala la msingi sana katika kufikia ukomavu wa demokrasia hiyo.

Imetolewa;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi.
17/06/2013

video fupi siku ya tukio.

Mbowe akiitaja serikali kuhusika

Chanzo: CCM Blog: CCM YALAANI TUKIO LA MLIPUKO WA MABOMU ARUSHA
 
Last edited by a moderator:
Lema nae asema wanamjua mlipuaji kwa video waliyonayo.. Wanamjua mpaka jina.. Asema ccm wanahusika... Voa
 
Hilo tulilitegemea kusikia,matamko kama hayo ni ya kawaida kutoka Lumumba.
 
Kama kuna jina nikiliona nasikia kichefu chefu ni huyu jamaa mzandiki, si kila kitu ni siasa na propaganda, nina uhakika kama haya yatakuja kumpata ndugu yake na huyu jamaa mlopokaji ndiyo atajua uchungu wa kupoteza ndugu kwa Uchafu wa chama cha kifisadi, hivi Nape anapata muda wa kukaa na kutafakari angalau kwa dakika tano. mambo yanayo weza kumtunzia heshima yake zaidiya kuwazia kuwa CCM ndiyo maisha yake yote!
 
Bandu bandu humaliza gogo yakhe. Ukifikiri wameshinda kidogo kumbe kapu lenu linapungua na mwisho wa siku, debe tupu halikosi kelele.
 
Hivi can someone put sense in these politicians? Bado watu wanatafakari yaliyotokea mnaanza kurusha siasa zisizo na msingi. Inaingia akilini kweli kuwa mkutano ni wa kwako utupe bomu ambalo linaweza kukuua wewe mwenyewe? Kwahiyo hata Kanisani Olisti walikuwa wakristu wenyewe au hawa hawa CHADEMA, sijui ili kukidhi nini. Kauli zenu zina impact mbaya kwa taifa jamani. Kumbukeni wanaofanya matendo haya wanaweza kuwa watu au kikundi kidogo sana nje au ndani ya vyama vyenu (CCM na CHADEMA) wakiwa na nia mbaya lakini kwa malengo yao. Msitugombanishe Watanzania kwa uchu wenu wa kisiasa.
 
Nape ameamua kujihami mapema..lakini Lema amesema wana ushahidi usio na mashaka kuhusu mlipuaji, amesema wanamjua mpaka jina.. Tusubiri tuone..alisema Nape hana akili sawawa kwa kitendo cha kuwahusisha cdm
 
naona wameamua kulopoka kama kawaida yao, dunia imeshajua udhalimu wa ccm, na ipo siku wataumbuka tu, mungu atawalaani wale wote wanaomwaga damu za wenzao. hili jambo halina muda mrefu tutapata ukweli maana najua mtageukana tu.
 
Katika hali isiyo ya kawaida au ya kawaida kwake, nikiwa nasililiza taarifa ya habari ya bbc Nape alisema "Bomu lililorushwa kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha lilipangwa na CHADEMA wenyewe kwa sababu waazi wa Arusha wamechoka siasa za CHADEMA"
1. Nilisikia miguno kwa watu wote waliokuwa karibu, watoto,vijana na wazee waliguna.
2. Mimi binafsi nilipatwa na hasira kwani hii ndo sura halisi ya ccm inayotuongoza na kutudanganya waziwazi

my take
Kama wananchi wameichoka chadema je wanakikubali chama gani?

Wananchi wanahudhuria kwa wingi sana mikutano ya ccm na cuf kuliko chadema?

Apimwe akili kwa nguvu hyu hajitambui
 
Wahusika ni hawa
Nape Nauye
Mwigulu Nchemba
Juliana Shonza
Mtera Mwampamba,, FBI wakija waanzie na hao, baada ya kuhakikisha mpango umeenda sawa wakatimkia Dodoma!
 
Akizungumza na sauti ya America Nape amesema wanaohusika na bom hilo ni cdm..
Amesema chadema ndiyo waliolipua hilo bom na wala sio ccm!

Ni lini mara ya mwisho Nape aliongea jambo la maana. Naamini hata JMK anafahamu Nape is a problem ila anamvumilia tu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Jamani ee huyu nape inawezekana anachongea ni pumba hakuna haja ya kushindana na mjinga wakati bado tuna majonzi ya kupoteza ndugu zetu!
 
Hivi can someone put sense in these politicians? Bado watu wanatafakari yaliyotokea mnaanza kurusha siasa zisizo na msingi. Inaingia akilini kweli kuwa mkutano ni wa kwako utupe bomu ambalo linaweza kukuua wewe mwenyewe? Kwahiyo hata Kanisani Olisti walikuwa wakristu wenyewe au hawa hawa CHADEMA, sijui ili kukidhi nini. Kauli zenu zina impact mbaya kwa taifa jamani. Kumbukeni wanaofanya matendo haya wanaweza kuwa watu au kikundi kidogo sana nje au ndani ya vyama vyenu (CCM na CHADEMA) wakiwa na nia mbaya lakini kwa malengo yao. Msitugombanishe Watanzania kwa uchu wenu wa kisiasa.

Haha, Unauliza Embe Kibada.
Rejea Mshtakiwa hilo tukio ambaye polisi wanamshikilia, Anaitwa nani Vile?
Sito shangaa na hili la soweto wakitafuta Mkenya na akajifanya ni Mfuasi wa Chadema.
 
Huu unaoongelewa hapa ndiyo unafiki, hili si sawl alakusikitikia ni serikali kulishughurikia na kutoka na jibu. ninauhakika kwa Asilimia 100 kama bomu hili lingetupwa katika mkutano wa CCM mpaka sasa watu kibao wangekuwa ndani, hiii si siri. Lakini haya yana mwisho. mnapoteza roho za ndugu zetu kisha mnakuja kupiga propaganda.
Na kusema mnashughurikia hili jambo ni upuuzi, mambo mangapi yamepita hivi hivi au mnadhani sisi ni wajinga au mpaka auwawe kiongozi wa serikali au wa jeshi.Najiuliza kama kweli nyie mna dini? kweli mtuunaweza kuongea uongo bila kujali kama kuna Mungu
 
Akizungumza na sauti ya America Nape amesema wanaohusika na bom hilo ni cdm..
Amesema chadema ndiyo waliolipua hilo bom na wala sio ccm!
Nami nimemsikia,nimesikitika mno!!!
Kiongozi wa Chama tawala unazungumza kitu ambacho ukiwekwa kati ya mawakili utajikanyaga.
Palikuwa na haraka gani,je akiitwa auelezee mpango mzima ataeleza kitu kweli?
So sad!!!!!!!!!!!!!!
Nimesikitika mno na nimekata tamaa na CCM,kweli wamefilisika kiasi hiki,inasikitisha!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom