Nape: Mlipuko wa bomu la Arusha yawezekana ulipangwa na CHADEMA wenyewe

NEPI ya Nnauye...soma hapa kutoka kwenye gazeti la Mwananchi utajuwa ni nani mwenye uwezo wa kutekeleza hili jambo na wala si kuropoka......"
Mtoto aeleza kupigwa risasi


Adam alisema jana kuwa alipigwa risasi na mtu aliyekuwa amevalia sare za polisi, wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu yake, Fahdi katika eneo la Soweto.


Alisema akiwa njiani, aliona watu wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa kupigwa risasi na kuanguka chini.


“Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa amevaa sare za polisi,” alisema Adam mwanafunzi katika Shule ya Msingi Levolosi huku akitokwa machozi.
 
Ukijumlisha total number of Voters

CCM wamepata kura 14,258

CHADEMA wamepata 16,117
kimahesabu rahisi ya darasa la tatu kuna tofauti ya kura 1859 sasa hapo weka na kata zetu nne A town.
 
Siku moja Mungu atawaaibisha kwa maovu wayatendayo, kwa nini ung'ang'ania kitu ambacho kimekushinda kukiongoza, kwa nn umentain status yako kwa kutumia damu ya watu wengine? Shame on you! Mliowezesha janga hili kutokea.
 
Jitu zima akili za mtoto wa darasa la 2, ambae pia ana uwezo wa kutambua na kujua sio vzr kufurahia kifo cha mwenzio
 
Tusiwe watumwa wa siasa, huyu jamaa anatakiwa apelekwe shule kwanza, manake hajielewi kabisa
 
Tunahitaji kuwa na Tanzania moja,tunaomba wanasiasa msitugawe.Bwana Nape kumbuka busara zababa yako,kumbuka busara za wazee wetu.Tanzania ni moja tunawaomba viongozi wa vyama vya Siasa msitupeleke Somalia.Ndugu yangu Nape mtu akifiwa hata kama unamchukia kiasi gan mpe pole mfarij huo ndo Utu.Mfano mtu akikutuumu kuwa wewe ni mchawi umeua mtoto wake,huwezi kwenda kwenye msiba huo ukitamba nakumzodoa.Utatafuta wazee baada ta siku nying umtafute mpatanishwe.Watu waliyokufa Arusha nao ni watu,wanahitaj kufarijiwa.Uliyoyasema wewe na Lukuvi inaelekea hujaguswa na msiba huo,angalau ungesubir watu walokufa wakazikwa.Mtu kuwa chama cha upinzani haina maana kuwa amepoteza U-tanzania wake.Kama CCM hamkuwa tayari na Mfumo wa vyama ving mgevifuta mwaka 2000 baada ya mwalimu kufa,mkatutawala mnavyotaka,mkatuibia manavyotaka,mkasafirisha Twiga kwenye briefcase mnavyotaka.Rudisha moyo wako,kumbuka busara za baba yako aliyelipenda Taifa hili na watu wake. Soma Mithali 13.1-2
 
Mungu yupo ya CHADEMA ila ukweli na dhambi kubwa sana ambayo ccm inachuma na siku zao zinakaribia
 
Kuna watu nawaheshimu sana hapa nchini kwetu lakini uvumilivu unanishinda kuendelea kuwaheshimu kutoka na kutoa maneno midomoni mwao bila kuushirikisha ubongo.Toka nizaliwe ndo nasikia hii.eti mtu anaweza kuchukua bomu na kulipiga nyumbani mwake mwenyewe na huku anajua sifa za bomu likilipuka linafanya nini,NI KWELI HII JAMANI?.Jamani wakati mwingne mapojijua kuwa mmeumiza watu wasio kuwa na hatia ishieni tu kuwapa hizo pole zenu za kinafiki.msiongee na maneni yasiyo kuwa na maana kwani mnatia watu hasira.
 
Nimeona nije na hili tena maana kila nikiwaza nakosa jibu sahihi. Hivi baada ya Baba wa taifa kufariki hakukubaki mtu mwenye akili ndani ya CCM? Hivi mwenyekiti wetu huoni hali ya chama inavyokuwa? Kama kweli yumo mwenye akili naomba niwaulize hivi hamwoni kuwa Nape na Mwigulu waichimbia Kaburi CCM au hamuoni.
Nilishangazwa na matamshi ya Katibu mwenezi wa CCM ndugu Nape Mnauye kuwa CHADEMA ndiyo waliojirushia mabomu, hivi kuna mtu yeyote aliye na akili angalau kidogo anayeweza kukubaliana na hayo? Ushauri kwa Nape, si kila jambo ujiweke kimbelembele kunena, wakati mwingine sema hivi tunavihachia vyombo vya dola kufanya kazi yake maana suala hili linahitaji uchunguzi. Hakika kauli ya Nape imenitia kichefuchefu. Namwomba Mwenyekiti afanye utaratibu wa kumwondoa katika nafasi hiyo, kuwa msemaji wa chama kunahitaji mtu mwenye busara zaidi ya Nape. Chama kimekuwa cha wapiga kelele tu wasio na busara. Alipotolewa Makamba nilidhani kuna mabadiliko ya maana yatakayotokea maana kama ni ubovu Makamba alikuwa wa ovyo kabisa. Hebu papasa mpate watu kama Philip Mangula wawe wasemaji wa Chama, NAPE HAWEZI KABISA. Tusisubiri Lowassa Kuja mumwondoa mwondoe sasa.
 
kwa kauli hii, inamaanisha yule balozi wa Vatican au watu wake ndio walio rusha Bomu Kanisani
 
Bwana Mdogo Nape, hata kama umeajiriwa kwa ajili ya kusemasema, jifunze kuchagua na kupanga cha kusema. bado una safari ndefu sana maishani na kisiasa, unaanza kuwa kichefuchefu mapema mno.
 
kwangu mimi naweza kuitupia lawama serikali sababu ndiyo ina jukumu la kulinda uhai wa raia wake na ccm ndo chama kinachoongoza serikali sasa kama imeshindwa kuchukua hatua za kulinda raia basi hawatufai kwa maana hili bomu sio la kwanza tena mkoa mmoja hii inaonyesha vyombo vyetu vya usalama vinatumia kodi yetu kunywa pombe si kufanya kazi inayotakiwa
 
[h=2]Ukweli kuhusu mlipuko wa Arusha na Mwigulu Nchemba,kwa manufaa ya Watanzania na Wana Arusha ni huu![/h]
Naibu Katibu mkuu(CCM)bara na Mbunge wa Iramba magharibi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba,ambae alikua mmoja Kati ya viongozi wa CCM wa kitaifa,walioshiriki katika kampeni zilizohusisha kata 4 ndani ya manispaa ya Arusha na moja Monduli,ambayo CCM wameichukua tena,amekua mstari wa mbele kunadi wagombea wa chama chake katika chaguzi ndogo zilizohitimishwa mapema tar 18.7.2013. Kumekua na mengi yaliyo na yanayosemwa dhidi yake,nikiwa mmoja Kati ya wakazi waliofatilia karibu siasa za Arusha na kwa maoni tofauti nikaona ni vema nishiriki nanyi katika habari hii ju ya kweli na yasiyo ya kweli,mwenye ushahidi tofauti awasilishe huo na si matusi.

Ni kweli alidhihirisha mbele za umma wa wana Arusha wa kata zote ju ya ukomavu wake wa kisiasa alionao,kwa kujenga hoja za chama chake,na kueleza wapiga kura na wengineo Yale ambayo chama chake kimefanya na kwa vielelezo.

Wakati akifanya hivyo pia hakuacha ku-refer ju ya upande wa wengine ambao pia walipata fursa ya kujinadi mwaka 2010,kupitia kwenye uchaguzi mkuu,kuaminika kwa wapiga kura kutokana na ahadi zao lukuki kisha kupata fursa za uongozi kwenye jumla ya kata 8 Kati ya 19,pamoja na jimbo la Arusha.alijaribu kuhoji endapo viongozi hao waliwahi hata kutekeleza moja Kati ya ahadi lukuki zilizoelezwa kua zingetekelezeka ndani ya mwezi mmoja! Majibu kwa wapiga kura wa Arusha yalikua HAPANA! Alikua akiendelea kuwakumbusha kua sasa wamekwisha jua chama chenye asili ya utekelezaji na chenye asili ya kutoa ahadi lukuki hewa na kisha kutotimiza.

Ni kweli pia,aliambatana na Yule kijana Musa wa Igunga,ambaye alifanyiwa kitendo cha kinyama na kisicho hata na tone la hofu ya Mwenyezi Mungu,kwa kumwagiwa na tindikali na kisha kutupiwa kwenye miiba,ambapo alifanikiwa kukimbizwa KCMC na baadae Nchini India. Kabla ya kumsimamisha ili naye awasalimu Kama ilivyohaki kwa mwanachama wa chama chochote kupewa nafasi na chama chake kusalimu wapiga kura,hakukua na dhambi katu kwa Mwigulu, kuwaeleza Wananchi maswahibu yaliyomkuta kijana mwenzao na huku akilaani kitendo hiko na kusema kua Tanzania hatupaswi kufika hapo.

Ni kweli,ameeleza bayana kupitia kampeni alizoziongoza kua hawezi kuwapenda "chadema/wana siasa wanaoratibu migogoro kwa vijana/Kada yoyote ile, badala ya kuratibu namna ya kuwasaidia vijana hao/wananchi",alisisitiza mara kwa mara hathari ya kiongozi alieaminika na kupata dhamana ya kuongoza ni vema akajaribu kusimamia namna ya kukabiliana na kero za Wananchi badala ya kuwaongezea kero nyingine kwa kupandikiza chuki ungali unaboresha maisha yako na familia yako na hao waliokufikisha hapo wakiambulia kubaki na fujo pamoja na kuharibiwa watoto wao na biashara zao kuyumba.

Ni kweli,alisema kwa kua chadema wameshindwa kutekeleza waliyoahidi hata kutunza tu yaliyofanyika Arusha,wakati madiwani wao hawaingii bado manispaa!je wana Arusha mtawezaje kupata uwakilishi ju ya kero zilizopo endapo mtawachagua!which is very true!

Ni kweli pia alisema,kuna kila sababu wana siasa kua na utu,uzalendo na nia ya dhati ya kusaidia Wananchi hususan kwenye Yale unayoyasema,akitolea mifano hai mingi ya changamoto zilizopo Arusha mjini bila ya kusemewa.

Si kweli,kua alisema Arusha watakoma wasipoichagua CCM,sababu tukumbuke hata kabla ya uchaguzi huu mdogo kata hizo zilikua kwa CDM,na CCM haikua na cha kupoteza bali Wananchi wa kata hizo na Jimbo la Arusha kwa ujumla,kwa kukosa uwakilishi ndani ya manispaa na bungeni,Tanzania nzima inajua kua hata mbunge Lema hajawai toa mchango wa aina yoyote Kama uwakilishi kwa wapiga kura wake zaidi ya kuendelea kujenga uchumi wake na familia huku Wananchi wakiachwa wakielemewa na matatizo.

Si kweli kua,alichochea kwa maneno kwenye jukwaa lolote,mahali popote,pale ju ya fujo kwa aina yoyote,isipokua kwa wapinzani wa maendeleo Kwao yaliokuwa yakisemwa na Mwigulu na ambayo hua anayasema siku zote,ndani ya bunge na penginepo kwenye ulingo wa kisiasa,yamekua kama miiba ya moto ya inchi 7! Bali kwa wapinzani wa kisiasa Imekua changamoto inayohitaji kujipanga tena kwa ajili ya maboresho.

Nahitimisha kwa kushauri yafuatayo;
1. Ni vema tukawa wana siasa na si wapinzani wa siasa,kwa kuwa wa kweli kwenye ukweli na kusimamia haki palipo na haki.
2.Ni vema Kama GT,Mzalendo wa Nchi ukachukua hatua ya kupigania Nchi badala ya ushabiki.

3.Chama/Viongozi makini ni wale tu wanaoweza kukusanya na si kutawanya watu wake.

4.Si vema hata kidogo,kupotosha wengine kwa maslahi ya siasa za ushabiki,Mahusiano ya aina yoyote,udini,ukabila,ujinsia ama matarajio ya baadae yasioyojulikana hata hatma yake.

5.Hatma ya Tanzania ya Leo ipo ju yako na mimi,tukae tutafakari yapi yatakua matunda ya kutumika kwa uongo!nini hatma ya WATOTO zetu,WADOGO zetu,WAZAZI wetu hata BABU na BIBI zetu baada ya kushiriki kuvuruga amani yetu,kupitia kauli za udini,ukabila na siasa chafu za wana siasa WAROHO! Wanaotuchochea leo!


Ndugu Mtanzania"chukua hatua ya kusimamia ukweli na kupinga uongo hadharani maana laana ya aina yoyote itakayotokana na upotoshwaji wowote ule,hautokuacha,wakati watu wakianza kuchinjana na kubaguana kwa dini AMA makabila yao hakika yote hayo yataandikwa upande wako. Natambua wapo watakaoleta ushabiki katika hili,ila muombe Mungu akusaidie kuchangia kwa hekima.
Idumu Tanzania,Idumu amani yetu na undugu wetu.​
 
Chadema kushinda kata zote nne arusha tena kwakishindo kikubwa,,,ni jibu tosha kuwa haiusiki hata kidogo katika mlipuko uliotokea viwanja vya soweto tena ukizingatia ushindi uliopata katika kata husika ya kaloleni,, CHADEMA kwa kura 1,470 dhidi ya CCM kura 530 na CUF kura 275,,demokrasia makini 2.
 
Back
Top Bottom