Nape, mfukuzeni Dr. Slaa uanachama CCM

Nape, mfukuzeni Dr. Slaa uanachama CCM

kapya

Senior Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
153
Reaction score
54
Bwana nape mjadala wa kadi ya CCM aliyonayo Dr.umechosha masikio ya watu na kutufanya tusahau kufikiria matatizo ya msingi ya taifa letu,badala yake tuijadili kadi.

sasa basi naomba nikushauri kuwa kama una uhakika kuwa Dr. Slaa anamiliki kadi ya M na anailipia,hivyo ni fika kuwa ni mwanachama wa CCM. Na kwa kuwa katiba ya CCM hairusu mwanachama kutumikia vyama viwili.

NAKUSIHI ILI KULINDA HADHI YA KATIBA YA CCM,ANDAENI UTARATIBU NA MUITE PRESS CONFERENCE MUMFUKUZE UANACHAMA KULIKO KUKAA NA KUZUNGUMZIA HOJA ZA KADI WAKATI WATANZANIA TUNA SHIDA KIBAO AMBAZO ZINAPASWA KUJADILIWA.

NAWASILISHA
 
Walikuwa wapi kipindi cha uchaguzi uliopita?

Hivi kama kweli Dr.anamiliki na kuilipia hiyo
kadi kwanini wasilete kielelezo?

Nape unajiaibisha ndugu yangu!!!!
 
Bwana nape mjadala wa kadi ya ccm aliyonayo dr.umechosha masikio ya watu na kutufanya tusahau kufikiria matatizo ya msingi ya taifa letu,badala yake tuijadili kadi.sasa basi naomba nikushauri kuwa kama una uhakika kuwa slaa anamiliki kadi ya ccm na anailipia,hivyo ni fika kuwa ni mwanachama wa ccm.Na kwa kuwa katiba ya CCM hairusu mwanachama kutumikia vyama viwili,NAKUSIHI ILI KULINDA HADHI YA KATIBA YA CCM,ANDAENI UTARATIBU NA MUITE PRESS CONFERENCE MUMFUKUZE UANACHAMA KULIKO KUKAA NA KUZUNGUMZIA HOJA ZA KADI WAKATI WATANZANIA TUNA SHIDA KIBAO AMBAZO ZINAPASWA KUJADILIWA.NAWASILISHA

Napeeeee! Mbona hamkuweka pingamizi wakati wa uchaguzi mkuu 2010? Kwamba kuna mgombea uraisi ana kadi mbili za vyama?????!!!!!!!!!!!!
 
Kwanza nikupongeze kwa busara kubwa uliyotumia na maneno ya kiungwana. Ni kweli nilianzisha mjadala huu,lakini baada ya hapo sijaendelea kujadili hili,mie naendelea na majukumu yangu mengine japokuwa nasikia maneno mengi sana tena ya kipuuzi sana! Nasikitika mjadala huu kutumika kudhalilisha watu akiwemo Dr. Slaa(babu yangu)...HAIKUA KUSUDIO LA MJADALA HUU...nilitaka kumkumbusha babu kuishi anayoyahubiri basi!! So Dr. Sio mwanachama wa ccm kwa mujibu wa katiba ya ccm bali ANAMILIKI KADI YA CCM na hoja yangu hapa wakati yeye ANAHAMASISHA WATU KURUDISHA KADI ZA CCM YEYE YAKE KAKIRI KUITUNZA...kulipia kadi na kuwa na kadi is kipimo cha uanachama wa mtu...
Bwana nape mjadala wa kadi ya ccm aliyonayo dr.umechosha masikio ya watu na kutufanya tusahau kufikiria matatizo ya msingi ya taifa letu,badala yake tuijadili kadi.sasa basi naomba nikushauri kuwa kama una uhakika kuwa slaa anamiliki kadi ya ccm na anailipia,hivyo ni fika kuwa ni mwanachama wa ccm.Na kwa kuwa katiba ya CCM hairusu mwanachama kutumikia vyama viwili,NAKUSIHI ILI KULINDA HADHI YA KATIBA YA CCM,ANDAENI UTARATIBU NA MUITE PRESS CONFERENCE MUMFUKUZE UANACHAMA KULIKO KUKAA NA KUZUNGUMZIA HOJA ZA KADI WAKATI WATANZANIA TUNA SHIDA KIBAO AMBAZO ZINAPASWA KUJADILIWA.NAWASILISHA
 
Kapya,
Kwahiyo huwezi kumfukuza mtu ambaye simwananchama wako! Kama mjadala wa viongozi wetu kuishi maisha wanayoyahubiri unachosha is ajabu ipo siku utadai tumechoshwa na mjadala juu ya vita dhidi ya ufisadi na rushwa!
 
Kwanza nikupongeze kwa busara kubwa uliyotumia na maneno ya kiungwana. Ni kweli nilianzisha mjadala huu,lakini baada ya hapo sijaendelea kujadili hili,mie naendelea na majukumu yangu mengine japokuwa nasikia maneno mengi sana tena ya kipuuzi sana! Nasikitika mjadala huu kutumika kudhalilisha watu akiwemo Dr. Slaa(babu yangu)...HAIKUA KUSUDIO LA MJADALA HUU...nilitaka kumkumbusha babu kuishi anayoyahubiri basi!! So Dr. Sio mwanachama wa ccm kwa mujibu wa katiba ya ccm bali ANAMILIKI KADI YA CCM na hoja yangu hapa wakati yeye ANAHAMASISHA WATU KURUDISHA KADI ZA CCM YEYE YAKE KAKIRI KUITUNZA...kulipia kadi na kuwa na kadi is kipimo cha uanachama wa mtu...
we mbona mnafiki hivi?si ulisema utatoa ushahidi wa yeye kuilipia hiyo kadi?halafu kumwita babu wakati baba yako anafariki 2001 alikuwa na umri sawa na slaa kwa umri wake wa leo inaonyesha usivyokuwa nakumbukumbu
 
Kapya,
Kwahiyo huwezi kumfukuza mtu ambaye simwananchama wako! Kama mjadala wa viongozi wetu kuishi maisha wanayoyahubiri unachosha is ajabu ipo siku utadai tumechoshwa na mjadala juu ya vita dhidi ya ufisadi na rushwa!
hii vita ishakushinda na umesalimu kwa lowassa,sasa hivi unajikomba kwa lowassa,mseme tena akuondolee ulaji wa kifisadi ulionao sasa..chezea mamvi we
 
Kapya,
Kwahiyo huwezi kumfukuza mtu ambaye simwananchama wako! Kama mjadala wa viongozi wetu kuishi maisha wanayoyahubiri unachosha is ajabu ipo siku utadai tumechoshwa na mjadala juu ya vita dhidi ya ufisadi na rushwa!

Vipi magamba lini yatatoka!!!!
 
Hahaha magwanda mnalo! Mnaanzishiwa ngoma mnacheza kama mazuzu! Mkiambiwa hicho sio chama ni NGO mnanuna!! Akhhaaaa!

childish is not far away !!!!

ninauhakika hata maana na sheria inayotunga na kuelezea NGO huijui
 
Kwanza nikupongeze kwa busara kubwa uliyotumia na maneno ya kiungwana. Ni kweli nilianzisha mjadala huu,lakini baada ya hapo sijaendelea kujadili hili,mie naendelea na majukumu yangu mengine japokuwa nasikia maneno mengi sana tena ya kipuuzi sana! Nasikitika mjadala huu kutumika kudhalilisha watu akiwemo Dr. Slaa(babu yangu)...HAIKUA KUSUDIO LA MJADALA HUU...nilitaka kumkumbusha babu kuishi anayoyahubiri basi!! So Dr. Sio mwanachama wa ccm kwa mujibu wa katiba ya ccm bali ANAMILIKI KADI YA CCM na hoja yangu hapa wakati yeye ANAHAMASISHA WATU KURUDISHA KADI ZA CCM YEYE YAKE KAKIRI KUITUNZA...kulipia kadi na kuwa na kadi is kipimo cha uanachama wa mtu...

Nape CCJ ulihusika nayo? Ungwana ni kipimo cha busara ni vyema pia na wewe ukaishi unavyohubiri
 
Kapya,
Kwahiyo huwezi kumfukuza mtu ambaye simwananchama wako! Kama mjadala wa viongozi wetu kuishi maisha wanayoyahubiri unachosha is ajabu ipo siku utadai tumechoshwa na mjadala juu ya vita dhidi ya ufisadi na rushwa!

Maneno ya Nnauye Jr yamejaa masihara na utani mwingi, bila shaka anatuaminisha kuwa yeye binafsi anaiona Chadema kama mtani wa jadi na wala sio mpinzani anayetishia kutwaa dola toka mikononi mwa CCM. Ninayo maswali, lakini sitakuuliza leo, acha nifaidi kwanza hizi sherehe zilizopo mbele yetu,
 
Walikuwa wapi kipindi cha uchaguzi uliopita?

Hivi kama kweli Dr.anamiliki na kuilipia hiyo
kadi kwanini wasilete kielelezo?

Nape unajiaibisha ndugu yangu!!!!

Mkuu wangu naomba badilisha comment yako hapo,huna ndugu mwenye akili kama za Nape huyu jamaa ni too chaldish, akili zake za kitoto sana ndio maana huwa namuignore,hebu soma comment zake hapo juu....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kakazania wamfukuze nasikia hata kumtukana huyu jamaa,usiwafanye watu watoto Nape,utoto wako peleka huko kama unaona anawaangaisha akili CCM then usituletee utoto humu ndani....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Nape nimeipenda attitude yako leo: Ila kwa kuwa kuna miaka mitatu kabla CDM hakijashika dola, napendekeza jamani vijana mliopo ndani ya CCM kemeeni ufisadi kama afanyavyo Filikunjombe. Maana hakuna namna nyingine ni lazima tuendelee kutawaliwa na CCM hadi October 2015, basi jitahidini kuiokoa nchi kutoka makucha ya MAFISADI ndani ya CCM. Please!!!!
 
Kwanza nikupongeze kwa busara kubwa uliyotumia na maneno ya kiungwana. Ni kweli nilianzisha mjadala huu,lakini baada ya hapo sijaendelea kujadili hili,mie naendelea na majukumu yangu mengine japokuwa nasikia maneno mengi sana tena ya kipuuzi sana! Nasikitika mjadala huu kutumika kudhalilisha watu akiwemo Dr. Slaa(babu yangu)...HAIKUA KUSUDIO LA MJADALA HUU...nilitaka kumkumbusha babu kuishi anayoyahubiri basi!! So Dr. Sio mwanachama wa ccm kwa mujibu wa katiba ya ccm bali ANAMILIKI KADI YA CCM na hoja yangu hapa wakati yeye ANAHAMASISHA WATU KURUDISHA KADI ZA CCM YEYE YAKE KAKIRI KUITUNZA...kulipia kadi na kuwa na kadi is kipimo cha uanachama wa mtu...

Nikusahihishe hapo kwenye red kuwa yeye hajahamasisha watu kurudisha kadi za ccm.Yeye anahamasisha watanzania wanyonge (ambao wapo ccm, chama ambacho hakipo tena kwa maslahi ya wanyonge baada ya kukiuka misingi yake) wajiunge na chama kombozi CHADEMA.

Wananchi wanajiunga na chadema na kuwa wanachama wake na wengine kwa ridhaa yao wenyewe huamua kurudisha kabisa kadi zao za chama cha zamani.Kitendo cha wao kurudisha hizo kadi sio moja ya protocal ya kujiunga na chadema asilani.Kanuni na masharti ya kujiunga na chadema yapo wazi kwenye katiba yake na hilo la kurudisha kadi ya chama utokacho halipo ila hufanywa kwa utashi na wanaopenda kufanya hivyo.

Chadema sio kama ccm ambayo mtu anaweza kujiunga na chama kingine na kuwa mbunge kwa miaka 15 na kugombea mpaka uraisi na kushinda(sizungumzii kutangazwa mshindi na NEC) lakini bado kikaendelea kumtambua na kumlazimisha kuwa yeye bado ni wa kwao!Hii inaonyesha kumiliki karatasi ya ccm isiyo active hata kwa miaka 15 bado mmiliki anaendelea kuwa mwanaccm kwa mujibu wa katiba yenu nadhani.Kwahiyo hilo ni kwa katiba yenu tu,lakini sisi chadema uanachama wetu haupo kihayawani kama wa kwenu.

Pili nikuase kuwa siasa unazofanya zinakushushia sana heshima yako ndogo iliyokuwa imebaki.Kumuita Dr.Slaa majina unayopenda kwa lengo la kumdhailisha sio kitu cha kiungwana na ni kumkosea heshima mzee wetu.Ni kweli Dr. ni mtu mzima na anafaa kupewa heshima yake kama ambavyo mtu mzima mzee Kikwete anavyopewa heshima yake.Kumuita babu Dr.Slaa na kutomuita babu Kikwete ni kuonyesha jinsi uivyo na kejeli na sio heshima.

Ina maana humuheshimu mzee Kikwete?Sasa mbona humuiti babu kama kweli unamuita Slaa kwa heshima?By the way Dr.Slaa ni mdogo kwa baba yako mzee Nnauye(RIP) ambaye alizaliwa 5/7/1937.Dr.Slaa alizaliwa 29/10/1948!Sasa uhalali wa kumuita babu mdogo wake baba yako kwa miaka 11 unautoa wapi?Mzee Nnauye ulikuwa unamuita babu?
Acha siasa za kijinga kwani kila mtu akiamua kumdhalilisha mwingine kwa maneno kama yako hakuna atakayebaki.

Mwisho nakuomba utoe ushahidi kuwa Dr.Slaa anaendelea kulipia kipande cha karatasi ya ccm alichonacho ama sivyo huna sababu ya kuendelea kuliongelea tena hilo suala.Umeshaliongelea hilo suala sana sasa ni wakati wa kuthibitisha.
 
Hahaha magwanda mnalo! Mnaanzishiwa ngoma mnacheza kama mazuzu! Mkiambiwa hicho sio chama ni NGO mnanuna!! Akhhaaaa!

kauli hii kwel ya kwako nape? au kuna mtu anatumia id yako siamini ninachokisoma
 
[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow]
Mithali sura 26
3 Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,
[/FONT]
[/FONT]
[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][/FONT][/FONT] [FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow]nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu!
[/FONT]
[/FONT]
[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow] 4 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu [/FONT][/FONT]
[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][/FONT][/FONT][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow]wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.
[/FONT]
[/FONT][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][/FONT][/FONT]Bwana Nape Nafasi uliyo nayo ni kubwa sana, nahisi huitendei haki, unaponena kauli yako inahesabiwa kuwa ni kauli ya wana CCM zaidi ya Milioni Tano, achana na mambo ya kitoto, acha mabishano ya kipumbavu na wewe utaonekana kama wao. Maneno hayo juu kama ni msomaji wa Biblia naomba yakusaidie achana nao, wao wanafanya nini wana haki ya kufanya wanayofanya wewe waambie tunafanya nini, wewe waweke mijeredi tu mbona mbinu nyingi tu!! na kama wanachokipigia kelele kina manufaa kwa chama chetu wewe copy na kifanye kabla yao waache wabaki na maandamano tena wala usiwazuie, weye wazuie kwa vitendo watajikuta wako peke yao.

[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][/FONT][/FONT]

Back
Top Bottom