Nape kanusha na hili.

Mr.Busta

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
672
99
ITV katika taarifa ya habari jana saa 2 usiku.wameonyesha wenyeviti wa kijiji wa ccm akikiri kwamba M4C inawapa wakati mguu na kushindwa kuongozo.NAPE KANUSHA AU UNASEMAJE KWA HII?
 
Wapi huko mkuu? Hata kama ni kweli, huyo Nape hawezi kukanusha kuhusu hao wenyeviti ila atakanusha huu uzi wako!
 
vijijini huko kilosa.akikaa kimya anakubaliana na hali halisi.tunataka kauli yake mbna wanawategemea sana hawa wenyeviti wa vijiji katika kush4nda uchaguzi
 
Nini significance ya kauli yake ikiwa kweli hao wenyeviti wameona bora waseme kweli ya hali halisi inayowakabili?
 
Nyiye hammjui Nape huwa hana msimamo, ana damu na akili za kinyonga.
Akija humu atakwambia kuwa hao ni maji taka, au sio wenyevit wa CCM bali ni CDM wanajifanya CCM.
 
ITV katika taarifa ya habari jana saa 2 usiku.wameonyesha wenyeviti wa kijiji wa ccm akikiri kwamba M4C inawapa wakati mguu na kushindwa kuongozo.NAPE KANUSHA AU UNASEMAJE KWA HII?

Baada ya kupinga kumalizika wabunge wa magamba wameagizwa waende kukanusha yote yaliyokuwa yanasemwa kwenye M4C.kwasasa Nape yupo busy kuona ni jinsi gani wataratibu mikutano katika maeneo ambayo m4c wamepita ikiwa ni kujaribu kuweka mambo sawa.
 
Narudia kusema tena, sisi tuliopo Lumumba tunafuatilia kila kitu kinachoendelea kuhusu M4C kuanzia kule Lindi, Mtwara, London, USA, Dar, Mara, Morogoro, Arusha nk.

Kifupi tupo kwenye wakati mgumu sana kuliko wakati mwingine wowote toka mfumo wa vyama vingi umeingia tena nchini.

Taarifa za makada wetu kutoka sehemu mbalimbali ni za kukatisha tamaa tu kila siku.

Hii ni baadhi ya mikakati tulioianza na ambayo tunairatibu siku kwa siku.

*Mpango wa NAPE;
kupiga propaganda na kuiga operation za M4C (Propaganda ni rahisi kufanya na ndio msingi wa siasa za chama chetu lakini kwa sasa hazina nguvu kwa sababu ya utandawazi na kukua kwa uelewa kwa watu,
kufanya zile operation ulikuwa mpango mzuri lakini shida ni:
1/Unakigawa chama
2/Ni gharama kubwa (chama kina ukata na haukutengewa fungu maalum)
3/Ungehalalisha harakati za M 4C.
4/Hatuna uzoefu wowote wa siasa za kiharakati kwa sababu hatukuwahi kuwa chama cha upinzani toka tumepata uhuru)

*Mpango wa PINDA;
kutumia Dola ie Polisi, DC, RC, Tendwa (Lakini pia anaogopaogopa kwa sababu aliratibu mpango wa polisi kule Arusha na suala la Ulimboka halafu mambo yakamtokea puani, hivyo ni bora awatumie Tendwa,DC,RC zaidi kuliko polisi)

*Mpango wa WASIRA: kupandikiza mamluki ili wawavuruge(hili linahitaji usiri na pesa, ni kama kucheza kamari)

*Mpango wa MWIGULU; Kutumia pesa na ahadi za kuwapa vyeo ili kuwanunua makamanda wao ili wahamie CCM (Mchezo wa kitoto sana, bahati mbaya hata Mukama anauunga mkono, Makamba Senior alifanyaga hivyo na ukazaa matatizo makubwa sana ndani ya chama)

*Mpango wa JK;
Kutumia mahakama na Bunge kuzima harakati zao(Ni mkakati wa hila tu, matokeo mazuri yanadumu kwa muda mfupi sana, lakini unazaa athari mbaya kwetu kwa muda mrefu)

*Mkakati maalum wa IKULU; kutumia usalama wa taifa na vyombo vya habari kuwasambaratisha kwa gharama yoyote (Tatizo ya mbinu hii inahitaji usiri mkubwa sana, na kwa sasa hakuna siri tena!)
 
Ngoja niondoke ukumbini- manake kipigo kingine huwezi kutarajia mtu kuamka labda kama atakuwa Uli.
 
haiwezi kukanusha maana hii ni live na atakachokuja nacho ni kubwabwaja tu wala hatakuja na point bali pumba
 
nina uhakika nafasi ya Nape kama wangekuwa watu wanaanyiwa interview basi isingeweza kupita hata kidogo
 
Narudia kusema tena, sisi tuliopo Lumumba tunafuatilia kila kitu kinachoendelea kuhusu M4C kuanzia kule Lindi, Mtwara, London, USA, Dar, Mara, Morogoro, Arusha nk.

Kifupi tupo kwenye wakati mgumu sana kuliko wakati mwingine wowote toka mfumo wa vyama vingi umeingia tena nchini.

Taarifa za makada wetu kutoka sehemu mbalimbali ni za kukatisha tamaa tu kila siku.

Hii ni baadhi ya mikakati tulioianza na ambayo tunairatibu siku kwa siku.

*Mpango wa NAPE;
kupiga propaganda na kuiga operation za M4C (Propaganda ni rahisi kufanya na ndio msingi wa siasa za chama chetu lakini kwa sasa hazina nguvu kwa sababu ya utandawazi na kukua kwa uelewa kwa watu,
kufanya zile operation ulikuwa mpango mzuri lakini shida ni:
1/Unakigawa chama
2/Ni gharama kubwa (chama kina ukata na haukutengewa fungu maalum)
3/Ungehalalisha harakati za M 4C.
4/Hatuna uzoefu wowote wa siasa za kiharakati kwa sababu hatukuwahi kuwa chama cha upinzani toka tumepata uhuru)

*Mpango wa PINDA;
kutumia Dola ie Polisi, DC, RC, Tendwa (Lakini pia anaogopaogopa kwa sababu aliratibu mpango wa polisi kule Arusha na suala la Ulimboka halafu mambo yakamtokea puani, hivyo ni bora awatumie Tendwa,DC,RC zaidi kuliko polisi)

*Mpango wa WASIRA: kupandikiza mamluki ili wawavuruge(hili linahitaji usiri na pesa, ni kama kucheza kamari)

*Mpango wa MWIGULU; Kutumia pesa na ahadi za kuwapa vyeo ili kuwanunua makamanda wao ili wahamie CCM (Mchezo wa kitoto sana, bahati mbaya hata Mukama anauunga mkono, Makamba Senior alifanyaga hivyo na ukazaa matatizo makubwa sana ndani ya chama)

*Mpango wa JK;
Kutumia mahakama na Bunge kuzima harakati zao(Ni mkakati wa hila tu, matokeo mazuri yanadumu kwa muda mfupi sana, lakini unazaa athari mbaya kwetu kwa muda mrefu)

*Mkakati maalum wa IKULU; kutumia usalama wa taifa na vyombo vya habari kuwasambaratisha kwa gharama yoyote (Tatizo ya mbinu hii inahitaji usiri mkubwa sana, na kwa sasa hakuna siri tena!)

namba 4 nimeipenda sana, hii ni mtaji wa mfumo wa vyma vingi nchini. upinzani kuchukua nchi ni lazima, hata ikiwa miaka50 ijayo
 
Back
Top Bottom