Nape: Kamba Hukatika Pembeni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape: Kamba Hukatika Pembeni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Omutwale, Oct 18, 2011.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Watu hufikiri kuwa, labda jinsi pekee ya kummaliza mwanasiasa ni kwa kumhonga pesa/kumnunua au kumtoa uhai, LA HASHA. Hakuna njia nzuri kabisa, yenye matokeo bora yasiyo na ghalama kubwa katika kummaliza mpinzani wako kisiasa kama:

  KUJUA VEMA udhaifu wake na kuufanya kuwa FAIDA kwako. Kila mwanadamu ANA udhaifu wake. Kanuni hii pia inayofanya kazi katika Nyanja mbalimbali za maisha mfano katika Biashara.


  Wapinzani wa Nape wameujua vema udhaifu wake. Na nampa heko aliyewasaidia kuubaini. Udhaifu wa Nape ni mkubwa katika wepesi wa matamshi/maandishi mazito anayotoa katika hadhi yake kama Katibu Mwenezi. Hapa ndiko wapinzani wake ndani na nje ya CCM wanapojizolea maksi za ushindi vitani. Ukiishagundua huu udhaifu na kubaini kuwa kila tamshi la adui yako ni tata, lisilo na hadhi, lenye kejeli, na kuudhi hadhira, na wakati mwingine ujumbe anaotoa siyo wake kazi unayobaki nayo ni rahisi sana. Utamtengenezea misururu ya waandishi wa habari na kumuandalia matukio na hadhira ili ahutubu. Maana unajua kila baada ya tukio, ujumbe wake ukifika kwa hadhira, heshima na mvuto wa mtoa ujumbe vinashuka.

  Awali watu walipomwita Nape vuvuzela ilinipa taabu kuelewa walimaanisha nini. Wajua wakati mwingine kama huna kamusi na umekutana na neno jipya katikati ya sentensi, inabidi utumie uelewa wa maneno yale mengine kupata maana ya sentensi. Sasa naweza kupata maana yake kama bomba tupu linalopitisha upepo wa mpulizaji na kutokea upande wa pili kwa sauti pana. Vuvuzela halipitishi ujumbe wake lenyewe na wala halichuji kinachopitishwa. Matamshi na maandishi ya Nape yanampa sifa ya kulichukua jina hili.

  Kuna mambo Nape anabolonga kama vuvuzela na kuna mengine mengi anaharibu kutokana udhaifu wake wa kuanzisha ama kuchangia mijadala kwa kutoa hoja nyepesi kwenye masuala mazito. Na mbaya ni kwamba, yeye kila akiletewa MIC anakuwa kama mtoto kaletewa vanilla ice cream, lazima alambe! Akipigiwa simu na mwandishi anahisi yeye ni Encyclopedia Britannica, majibu yote anayo na ni sahihi! Na kwa sababu ya kuwa pitishio la ujumbe asio uasisi, kuendelea kuonyeshaa udhaifu wa Nape pia ni kuanika udhaifu wa anayepitisha ujumbe kwa Nape.

  Angalia hii mifano halisi:
  • Kauli za Nape juu ya msimamo wa kujivua gamba
  • Hotuba ya Nape kwenye Mkutano wa Mwanza juzi - “Nawashukuru Lusinde na Mwigulu kwa utangulizi wenu. …..mmenisaidia kuwabana wagonjwa pua ili mimi niwape dawa”
  • Nape kukana maandishi yake mwenyewe juu ya matokeo ya Igunga kwenye ukuta wake FB na ID yake JF
  • Kutowajua hata wapinzani wake nje ya CCM (Dr. Slaa na Mbowe-hii bado mbishi kabisa)
  • Kauli tata katika midahalo – Ujamaa wa ki-sayansi umepitwa na wakati. Ukiachana na sayansi unashikana na arts (sanaa). Hivyo anamaanisha ccm iko kwenye zama mpya ya ujamaa wa ki-sanii-GOOD! -ccm bado inayaenzi yote aliyoyaanzisha Baba wa Taifa ikiwemo Azimio la Arusha.
  Nape anamalizia pumzi yake ya mwisho ya uhai kisiasa. Namshauri ayapokee maoni yangu kama changamoto na yanaweza kumsaidia. Mimi si wa kwanza kumwambia juu ya suala hili. Radio Producer (member JF) naye amewahi kumshauri. Na tunafanya hivi kwa sababu tunamtaka arudi kwenye mstari kwa manufaa ya anachofikiri anakipigania.
   
 2. Kabwela

  Kabwela Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, sikio la kufa haliskii dawa na asiyejua kuwa hajui ni mgumu kukubali kuliko aneyafahamu kuwa hajui. Sijui Nape atakuwa upande upi, tusubiri tuone iwapo atakusikia
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,823
  Trophy Points: 280

  Ukiamua kumuua mbwa wako unayemfuga huna haja ya kukimbizana naye, waambie majirani kuwa huyu ni mbwa mwizi anakula kuku pia mbwa huyo anakichaa pia waambie majirani kuwa mbwa wako ni koko anakula mpaka kinyesi, baasi majirani wataokota mawe watampiga na kumuua mbwa huyo bila ya wewe mfugaji kumtupia hata jiwe moja Mbwa. Nape amesema yeye ni mbwa na mfuga mbwa ni CCM.
   
 4. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Daudi,
  Umesema vema. Ila nyongeza ya hapo, Nape kama mbwa kwanza wamembatiza jina baya a kisha wamemuharibu pua yake hivi sasa hanusi tena. Anabweka kwa kumkimbia adui anayedai kutomjua huku akiwa anaficha mkia na shingo imepinda kuangalia anakotoka hasijue majaaliwa ya aendako! Kazi ya kumalizia kutoa uhai wa mbwa wa sifa hizi ni nyepesi kama kupuliza sufi.
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,823
  Trophy Points: 280
  Mdahalo na Nape ni easy kama kumpapasa maiti, At the first word u need to shake his credibility na jamaa hana political maturity atapanic kama kawaida yake atatema yale maneno yake machafu alafu mwisho wa siku atajichoresha na kila mtaa atakaopita Mbwa huyu raia watamfukuza kwa mawe coz wamengundua ni Mbwa koko na mwenye Mbwa ambaye ni CCM anapita kando kama sio mliki wa mbwa huyo.
   
 6. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni kweli nape kwa sasa anapoteza credibility yake kama kijana na ya chama kwa ujumla kwa mambo yake na matamshi yasiyo mashiko. jambo moja baya simwoni kama wa kujifunza/kusikiliza lolote toka kwa yeyote lenye maana ya ushauri, nadhani kwa vile ameshazoea kutumwa obvious na JK kumsemea basi anaona hakuna wa kumkanya maana,so hana heshima kwa wana ccm wenyewe wala wapinzani. thats bad, acha tusubiri na kuona!
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hahahaaa, tangu jana nacheka mwenyewe mara nikikumbuka "Ntawashikisha ukuta......."

  Naanza kuamini maneno niliyoyasema mwenyewe baada ya kuona hii picha jinsi anavyochekelea kugawa kanga kwa wanaume.

  Angalia vizuri utaona mama mmoja tu kasimama anasubiri mgawo wa khanga, ila Nnape yeye na WASHIKA UKUTA.

  [​IMG]
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,823
  Trophy Points: 280
   
 11. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  James Millya naye anasema Nape vuvuze

  Ngoma ikilia sana.......
   
 12. m

  mpigilie JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ona alivyokenua meno....angalia body laungage yake...naogopa kumfananisha na shoga ila inaniwia vigumu kutomfananisha na shoga
   
 13. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Hivi TAKUKURU walikuwa wapi hapa? Maana hii inaonyesha kuwa ni rushwa ya KHANGA na KOFIA kwa kwenda mbele.

  Nawasikitikia sana CCM.

  Na saana namskitikia sana huyu jamaa kwa kupewa azi hii ya Ukatibu Mwenezi. Hakika viatu vya ofisi hii vimempwaya na tayari vilishachomoka miguuni na sasa anatembea pekupeku!!!

  CCM watajutia upuuzi wao huu wa kumweka mtu asiye na hekima na busara kwenye nafasi hii. Ni ukweli na uwazi kuwa NAPE anaisambaratisha CCM na kuiandalia mazishi katika kaburi la 6x6.

  Sijajua hasa kama kweli Mwenyekiti wake Kiwete haoni huu UJINGA unaofanywa na NAPE NAUYE. Hata kama M/kiti hajaona Katibu Mkuu naye yuko wapi??? Kweli SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTELEZA.

  CCM kwishneeeeeeeeee!
   
 14. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  naongeza:

  hashauriki pamoja na kupigwa msasa hapa jf.......

  hana tofauti na wana mipasho .......

  ni mhuni na mwenye lugha za matusi...

  hajui anachokifanya....

  kiufupi hana tabia njema na callibre ya uongozi!
   
 15. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
 16. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
   
 17. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #17
  May 31, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Umeandika ukweli mtupu kuhusu huyu jamaa ,pia juzi wakati anajitetea humu javini kuhusu tamko la vijana wa Bukoba ,alijichanganya akaandika "Marehemu nilikuwa namheshimu kama baba yangu mzazi" .Ikashangaza kama mtu alikuwa kama baba yake mzazi (alikuwa rafiki wa baba yake mzazi) iweje alienda kufanya shughuli za chama (kueneza itikadi za chama) kwenye msiba ili hali unajua baba(rafiki mkubwa wa baba yake) yake anazikwa kipindi hicho!!!?
   
 18. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  kamba hukatika pembamba.
   
 19. i

  isotope JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nasikitika yanayomkuda huyu dogo. Nepi ni sawa na mchwa aliyeoteshwa mabawa kuwa kumbikumbi. yeye alipoona mabawa akafurahi kuwa sasa anaweza kuruka. akaruka kutoka ndani ya kichuguu, matokeo yake anaanza kuliwa na ndege; binadamu wanamuokota wakamkaange. Kwisha kazi!
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii picha inadhalilisha utu wa mtanzania. Hakuna namna ya kueleza lakini ni jambo la kusikitisha.
   
Loading...