Nape: Kamba Hukatika Pembeni!

Nape: Kamba Hukatika Pembeni!

Hahahaaa, tangu jana nacheka mwenyewe mara nikikumbuka "Ntawashikisha ukuta......."

Naanza kuamini maneno niliyoyasema mwenyewe baada ya kuona hii picha jinsi anavyochekelea kugawa kanga kwa wanaume.

Angalia vizuri utaona mama mmoja tu kasimama anasubiri mgawo wa khanga, ila Nnape yeye na WASHIKA UKUTA.

attachment.php
Dah hao wote nawaangalia wana maisha duni sana, wanapewa hongo ya khanga.
 
Huu ujumbe ni mzuri sana kwa Nape,ila kwa sababu anajifanya mjuaji wakati hajui kitu tunamuacha kama alivyo,
Nape ni mlopokaji na ni mtu asiye na msimamo,
mimi namfananisha na kinyonga kwa sababu yuko tayari kuikana hata rangi yake harisi,
nadhani wengi tumemshuhudia kwa maandishi na kauli zake za mipasho,
huyu jamaa ni sikio la kufa hata tufanyeje haliwezi pona.
 
hapo nadhani anaimba kale ka wimbo: sandakalawe apate...kipapatio, cha kuku...kuku gani...!
 
Kuna wakati 1+1="(moja ndefuuu)" na kuna wakati "mtoto wa nyoka si nyoka"
 
Nasikitika yanayomkuda huyu dogo. Nepi ni sawa na mchwa aliyeoteshwa mabawa kuwa kumbikumbi. yeye alipoona mabawa akafurahi kuwa sasa anaweza kuruka. akaruka kutoka ndani ya kichuguu, matokeo yake anaanza kuliwa na ndege; binadamu wanamuokota wakamkaange. Kwisha kazi!

Nimeipenda hii! Well done.
 
Watu hufikiri kuwa, labda jinsi pekee ya kummaliza mwanasiasa ni kwa kumhonga pesa/kumnunua au kumtoa uhai, LA HASHA. Hakuna njia nzuri kabisa, yenye matokeo bora yasiyo na ghalama kubwa katika kummaliza mpinzani wako kisiasa kama:

KUJUA VEMA udhaifu wake na kuufanya kuwa FAIDA kwako. Kila mwanadamu ANA udhaifu wake. Kanuni hii pia inayofanya kazi katika Nyanja mbalimbali za maisha mfano katika Biashara.


Wapinzani wa Nape wameujua vema udhaifu wake. Na nampa heko aliyewasaidia kuubaini. Udhaifu wa Nape ni mkubwa katika wepesi wa matamshi/maandishi mazito anayotoa katika hadhi yake kama Katibu Mwenezi. Hapa ndiko wapinzani wake ndani na nje ya CCM wanapojizolea maksi za ushindi vitani. Ukiishagundua huu udhaifu na kubaini kuwa kila tamshi la adui yako ni tata, lisilo na hadhi, lenye kejeli, na kuudhi hadhira, na wakati mwingine ujumbe anaotoa siyo wake kazi unayobaki nayo ni rahisi sana. Utamtengenezea misururu ya waandishi wa habari na kumuandalia matukio na hadhira ili ahutubu. Maana unajua kila baada ya tukio, ujumbe wake ukifika kwa hadhira, heshima na mvuto wa mtoa ujumbe vinashuka.

Awali watu walipomwita Nape vuvuzela ilinipa taabu kuelewa walimaanisha nini. Wajua wakati mwingine kama huna kamusi na umekutana na neno jipya katikati ya sentensi, inabidi utumie uelewa wa maneno yale mengine kupata maana ya sentensi. Sasa naweza kupata maana yake kama bomba tupu linalopitisha upepo wa mpulizaji na kutokea upande wa pili kwa sauti pana. Vuvuzela halipitishi ujumbe wake lenyewe na wala halichuji kinachopitishwa. Matamshi na maandishi ya Nape yanampa sifa ya kulichukua jina hili.

Kuna mambo Nape anabolonga kama vuvuzela na kuna mengine mengi anaharibu kutokana udhaifu wake wa kuanzisha ama kuchangia mijadala kwa kutoa hoja nyepesi kwenye masuala mazito. Na mbaya ni kwamba, yeye kila akiletewa MIC anakuwa kama mtoto kaletewa vanilla ice cream, lazima alambe! Akipigiwa simu na mwandishi anahisi yeye ni Encyclopedia Britannica, majibu yote anayo na ni sahihi! Na kwa sababu ya kuwa pitishio la ujumbe asio uasisi, kuendelea kuonyeshaa udhaifu wa Nape pia ni kuanika udhaifu wa anayepitisha ujumbe kwa Nape.

Angalia hii mifano halisi:
  • Kauli za Nape juu ya msimamo wa kujivua gamba
  • Hotuba ya Nape kwenye Mkutano wa Mwanza juzi - "Nawashukuru Lusinde na Mwigulu kwa utangulizi wenu. …..mmenisaidia kuwabana wagonjwa pua ili mimi niwape dawa"
  • Nape kukana maandishi yake mwenyewe juu ya matokeo ya Igunga kwenye ukuta wake FB na ID yake JF
  • Kutowajua hata wapinzani wake nje ya CCM (Dr. Slaa na Mbowe-hii bado mbishi kabisa)
  • Kauli tata katika midahalo – Ujamaa wa ki-sayansi umepitwa na wakati. Ukiachana na sayansi unashikana na arts (sanaa). Hivyo anamaanisha ccm iko kwenye zama mpya ya ujamaa wa ki-sanii-GOOD! -ccm bado inayaenzi yote aliyoyaanzisha Baba wa Taifa ikiwemo Azimio la Arusha.
Nape anamalizia pumzi yake ya mwisho ya uhai kisiasa. Namshauri ayapokee maoni yangu kama changamoto na yanaweza kumsaidia. Mimi si wa kwanza kumwambia juu ya suala hili. Radio Producer (member JF) naye amewahi kumshauri. Na tunafanya hivi kwa sababu tunamtaka arudi kwenye mstari kwa manufaa ya anachofikiri anakipigania.

[h=3]Nape Anasema: " Inanipa Faraja Kusemwa Na Waovu"- Kutoka Facebook[/h]
[h=6]"INANIPA FARAJA KUCHUKIWA NA KUSEMWA VIBAYA NA WAOVU( wezi na watumiaji vibaya wa rasilimali na dhamana za uongozi walizopewa). HII INANIFANYA NISONGE MBELE KUWATETEA WANYONGE NA MASIKINI WA NCHI YANGU DHIDI YA UNYANG'AU WA MAFISADI HAWA!"- Nape Nnauye[/h]We call it Nape versus Maige. Angekua amesoma ushauri huu leo asingeandika haya.
 
Here we go again,

Personalities over policies, puppeteering over philosophizing, pubertal palavering over pointed punditry, putrid pugilism over potent pragmatism , philistine partisanship over poised pondering, pretentious pregnant populism over practical and pursuable productivity...

And that's just in the p's...
 
Huwa najiuliza, hivi Nnauye Jr angekosa ule Ukuu wa Wilaya wa Masasi ambao ulimpelekea kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikiadi na Uenezi hivi leo hii angekuwa wapi?

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Last edited by a moderator:
thitakii....bwaana.yaone.basi nampa huyuuu........haha. Thats is the power of proffessional photographers.They have heart and addditional eye on the lens.
 
Nape Anasema: " Inanipa Faraja Kusemwa Na Waovu"- Kutoka Facebook


"INANIPA FARAJA KUCHUKIWA NA KUSEMWA VIBAYA NA WAOVU( wezi na watumiaji vibaya wa rasilimali na dhamana za uongozi walizopewa). HII INANIFANYA NISONGE MBELE KUWATETEA WANYONGE NA MASIKINI WA NCHI YANGU DHIDI YA UNYANG'AU WA MAFISADI HAWA!"- Nape Nnauye

We call it Nape versus Maige. Angekua amesoma ushauri huu leo asingeandika haya.

The guy is naive here...anajikuta ktk hali ambayo hata osama alimini kuwa anaua kwa ajili ya bigger course ..kuwa wanafanya ktk kumsujudia Mungu...na kukomboa mataifa ya kiislam na Yerusalem..

Kwa siasa za kijinga za ccm za kuwaita wachina true friends ktk soko huria, tena wakati wachina wananegotiate serious deal atmosphere ina mparalyse km vile amekwenda ktk shrine toa sadak.


-Nape anaweza kuwa hajui masikini ni nani ndio maana anaongea vitu vinavyoshangaza watu wote hadi hao masikini.Does it mean lazima ongee, hata kama kazi yake ni kuongea, kwaniakichelewa kidogo tuu si watawahi akina wassira, na wengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom