Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,554
Waziri Nape - Clouds TV
Trh 20. 08. 2022
Serikali ilifanya tathimini ya mwisho ya gharama za data mwaka 2018 ambayo ndiyo inatumika hadi sasa.
Tathimini hii ilionesha kuwa gharama ya kusafirisha unit ya data ipo kati ya tsh 2.09-9.35
Tathimini mpya kwa sasa inafanyika ambayo itaanza kutumika tena mwaka kesho. Hii ina maanisha kuwa mapitio haya hufanyika kila baada ya miaka 4.
Hali ya sasa inaonesha kuwa kuna line milioni 58 za simu nchini. Jambo hili lilifanya tuwe na wateja wengi kuliko watoa huduma.
Kwenye data, wingi huu wa watu uliathiri ubora wa huduma. Hatupaswi kuwa wapiga kelele wakati wa kuongea na simu, hatupaswi kumpigia mtu simu afu asipatikane.
Baada ya kuona ongezeko kubwa sana la bei, Serikali iliamua kuwavuta watoa huduma kutoka tsh 40.41 hadi 9.35, kazi hii imefanywa na Serikali ya awamu ya 6.
Hivi sasa tunavyozungumza bei ya kununua data Tanzania imeshuka hadi kufikia wastani wa tsh 1.71-9.35 na watoa huduma hawapaswi kuzidisha hapo.
Hata hapa tulipo, tunabanana kuuza data chini ya kiwango inachozalishwa.
Kwa takwimu za sasa, Tanzania ni nchi ya 6 Afrika kwa unafuu wa gharama za data, ya 50 duniani kwa unafuu huu. Tafiti hizo zimefanywa na mataifa tofauti, hazijafanywa na Serikali.
Hii bei ni ya chini sana kwa kuangalia, sisi watu wetu bado maskini. Purchasing power yao ni ndogo ndiyo maana Serikali inadhibiti ili isipande sana.
Sasa tunafanya tathimini upya ili kuja na mapitio mapya ya maeneo yanayo toa mwongozo wa bei. Maeneo hasa ya usafirishaji wa data ndiyo tunashughulikia kwa sasa. Lengo ni kupunguza gharama hizi.
Mwanzoni gharama ilikuwa ndogo kwa sababu baadhi ya watoa huduma wali compromise ili kuiweka chini zaidi lakini huduma zao zikawa mbovu.
Serikali haipuuzi na haitakuja kupuuza malalamiko ya watu wake. Tunasikia na tunashughulikia.
KUHUSU VIFURUSHI
Hizi ni huduma za ziada, siyo huduma za msingi. Kuna ambavyo vimeshuka na vingine vimepanda. Hili nalo tunapitia
Mtoa huduma hawezi tu kupandisha bei pasipo kuleta mapendekezo kwa mamlaka (TCRA) . Hii nayo hufanyika kila baada ya miezi 3.
Kazi ya makampuni siyo kuomba ridhaa kwa wananchi, isipokuwa ni kuwapa tu taarifa juu ya biadhaa mpya wanazotoa. Lakini, bidhaa hizo hupitia kwanza TCRA
MASWALI NA MAJIBU
MDAU 1: Unapewa MB 550 tu kwa siku, na kabla ya masaa 24 kimeisha hata haujatumia sana. Hii imekaaje?
Nape: Kwenye kuchagua unapewa muongozo, ni mitambo wameseti ambayo watoa huduma na mamlaka wanapitia kuhakiki usahihi wa mitambo hii.
Hii nime address sana, na nilisema tangu mwanzo. Kama kuna mtu kaibiwa aje atoe ushahidi wa kuibiwa bando. Wengi wamekuja na baada ya uchunguzi wanaelewa.
Ni vizuri kuwa makini na matumizi ya smart devices tunazotumia. Kuna mambo mengi yanaendelea nyuma ya pazia ambayo unaweza ukawa hujui.
Unaweza tu kuwa unapakua WhatsApp. Kitendo cha kubonyeza sehemu ya kukubali kikaja na mambo mengine ambayo pia yanakula data yako. Tuwe makini.
Leo pia narudia, kama kuna mtu hajatendewa haki aje. Mimi pia natamani nipate kesi moja ya wizi ithibitishwe ili iondoe yote haya.
==
MDAU 2: Tunapewa tu taarifa na makampuni kuwa vifurushi vimepanda, lakini hatuna nafasi ya kutoa maoni. Tufanye nini?
Nape: Unaweza kutoa maoni yako TCRA, wanasikiliza. Tena kuna desk moja pale kwa ajili ya watu wa aina hii.
==
MDAU 3: Bei zitashuka?
Nape: Tunashughulikia
==
MDAU 4: (Alitoa lugha ya matusi)
Nape: Niulize vizuri, nitakujibu vizuri. Matusi hayawezi kusaidia. Tuwe na utaratibu wa kuzungumza kwa staha.
==
MDAU 5: Kwanini gharama za kusajili line zisipande ili kuzuia watu wengi kuwa na line nyingi ambazo zinaelemea makampuni?
Nape: Haya ni maoni, nimeyapokea.
==
MDAU 6: Mimi natumia kiswaswadu. Nikiunga kifurushi cha dakika na data, internet yangu huenda wapi na sijaitumia?
Nape: Nunua kifurushi kisicho na internet ili kuondokana na kadhia hii.
==
MDAU 7: Kwanini mnatumia US dollar kwenye comparison na siyo Tsh ambayo ndiyo uhalisia wa maisha ya mtanzania?
Nape: US dollar ni swala la kidunia. Ndiyo kiasi kinachotumika kulinganisha gharama zetu na huko duniani.
Tunapozungumza kwa lugha ya ndani tunatumia Tsh, tukiweka mizani nje ya mipaka ya nchi tunatumia dollar.
==
MDAU 8: Kwanini bando lina expire hata kama sijatumia?
Nape: Weka salio la kawaida, masharti ya bado yapo hivyo.
Ni kama tiketi ya mwezi (kwenye basi), mwezi ukiisha hata kama haujatumia ina expire.
==
AGIZO
Kila kampuni ya simu na TCRA waendelee kuelimisha watu, nataka kuona TCRA wakijibu maswali ya watu na makampuni ya simu yakiendelea kutoa elimu.
Wito wangu ni watu wapunguze hasira, watoe maoni kwa lugha ya staha kwani lengo letu ni moja tu, kujenga.