Mchambuzi,
..hivi kwa haya madubwana yote tuliyonayo nchi hii kuanzia uranium,iron ore,natural gas, gold, ardhi, na rasilimali watu, wewe unadhani ni kitu gani kinawezekana within 5,10,and 15 yrs??
..labda tunachotofautiana is on how radical the changes that we want have to take place.
..mimi ninachoogopa ni attitude ya wa-Tanzania kuona kama umasikini ni halali yao. we r not that demanding kwa viongozi wetu.
..kuna fikra imejengeka nchi hii kwamba wananchi tuko kwa ajili ya kuwatumikia viongozi.
..quite frankly I would b happy kama CDM/CUF/CCM/CCJ etc etc watawafanya wananchi wawe na over expectations. hata kama kitendo hicho kitapelekea kuwaondoa madarakani.
You have raised an interesting point ambayo ningependa kuijadili kidogo.
Miaka 50 iliyopita, Venezuelans, kama sisi leo hii, walikuwa wanazungumzia about
"sowing the oil" – kwa maana ya kwamba kutumia mapato ya mafuta na gesi kuwekeza kwenye sekta ya kilimo hence transform the sector; Lakini matokeo yake, kilimo kikaendelea kuwa neglected as leaders were mesmerized by oil, including kujenga sky scrapers mijini, kutorosha fedha nje na kuweka kwenye mabenki uswisi n.k; Matokeo yake ni kwamba leo hii, Venezuela imports karibia nusu ya chakula chake;
wananchi consume imported wheat kuliko wanayoizalisha ndani ya nchi; Wakati huo huo, politicians na washirika wao na pia wajanja wachache ndio wamekuwa the new middle class wakiishi Americanized life styles on Oil money huku majority ya wananchi wanaendelea kuwa katika hali duni; ni wananchi hawa ambao ndio waliomuunga mkono Hugo Chavez katika harakazi zake za mapinduzi, hasa kutokana na ahadi zake kwamba he will
"Sow the oil" kwa faida ya wengi;
Leo hii, watanzania wanaimbiwa nyimbo na ngonjera zile zile za Hugo Chavez - kwamba nchi imejaa kila aina ya neema in terms of rasilimali na ni moja ya nchi zinazo zalisha Dhahabu kwa wingi sana duniani lakini utajiri huu unanufaisha wachache huku wananchi walio wengi wanazidi kuwa maskini. Sina maana kwamba Chadema watafanya ya Hugo Chavez bali natoa angalizo tu kwani tumeona jinsi gani CCM (Nape) na Chadema wameanza kuvutana juu ya fedha za vyama vyao huku suala la rasilimali zetu (oil, gas, minerals..) liki dominate sana kwenye mvutano huu. Ni muhimu kwa wananchi kuelewa kwa kina kuhusu suala hili, hasa given the experience kama ya Venezuela na kwingineko;
Mimi ni muumini wa economic development inayoendana sambamba na ukuaji wa demokrasia; kwa mfano, Iam against Maendeleo katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi na zinazo experience economic growth and development kutokana na mafuta, lakini huku wananchi wake wakibanwa kwenye suala zima la demokrasia; Ndio maana nadhani nitakuwa sahihi kusema kwamba kama hatutakuwa careful, mapato yatayotokana na Resources za mafuta, gesi, madini…zinaweza kuja vuruga democratization Tanzania kwani utawala husika utakuwa katika nafasi nzuri ya kuchuma fedha kutoka sekta hizi na kuwekeza just the minium kwa manufaa ya wananchi huku nyingine nyingi zikienda mifukoni mwa watawala na wakubwa zao huko nje; Na katika mazingira yetu ya high illiteracy etc,wananchi wanaweza kuridhika na Maendeleo japo kidogo na kutoona tena umuhimu wa kubadilisha vyama vya siasa katika chaguzi kuu; hii inaweza kuua demokrasia nchi kwetu;
Chama ambacho kipo kwenye loosing end on this ni CCM na vyama vingine ambavyo havitafanikiwa kuwa part of the coalition government iwapo Chadema itashinda 2015;
Pamoja na umuhimu wote wa rasilimali hizi (mafuta, gesi, madini..), bado nadhani kwamba income generated from accumulation of Human and Physical Capital ina manufaa zaidi kwa demokrasia yetu; CCM ipo katika hali mbaya sana kwani Chadema wakifanikiwa kuingia ikulu 2015 and sow just the minimum (oil, gas, uranium etc), kuna uwezekano wakakaa ikulu for the next foreseeable future kama ilivyo kwa vyama tawala Botswana, Angola etc ambako hali za maisha ya watu zinaboreshwa, lakini there is less pressure on democratization;
CCM had an opportunity to utilize resources za nchi in the context of what I have discussed lakini kuna kila dalili kwamba kimechelewa;