Ni aibu kuwa na kijana msaliti kama Nape Nnauye
-Kwanza nilitegenea Nape
katika kujitokeza kwake kwenye media aongelee kashfa ya rushwa kwenye chaguzi ndani ya chama hasa ndani ya UVCCM mbayo ni jumuiya aliyotaka kuiongoza na ndiyo iliyomfikisha hapo kwa kujifanya na kuaminisha watu kuwa yeye ni mpambanaji dhidi ya ufisadi.Sikutegemea kwa mpambanaji kama huyu aongelee hili kabla ya hilo suala la rushwa
-Degree yake ya Journalism kule chuo cha Acharya,Bangalore ndiyo amekuja kuitumia vibaya kisiasa?Nape hajawahi kuwa makini katika uongozi tangu akiwa Acharya.Ni attention seeker
-Kwa kuwa huyu ni Muoga wa hesabu na takwimu(uwezo wake mdogo darasani tunaujua kule Acharya na tunaheahimu mapungufu yake) ameshindwa kujua M4C imezinduliwa miezi 4 tu iliyopita na kule Morogoro matokeo ya Udiwani yanajulikana,kule Iringa Dola ilipotumika hali ya kisiasa inajlikana na kule Lindi ambako M4C ilikoeneza uhamasishaji kwa kubeba bendera ya upinzani hata kuunga mkono jitihada za Mbunge wa CUF kwa maslahi ya Taifa matokeo yanajulikana
-Hapa hafanyi kazi ya uenezi bali ana kiu ya kujibiwa na Dr.Slaa au Mnyika tu.Hana majibu ya kuhusika kwake kuchochea vijana UVCCM kupigana ngumi hadharani na kudhalilisha chama chake wakishirikiana na kijana wa mwenyekiti ambaye anamtetea katika upuuzi waliofanya.
-Vijana kama Nape wanatakiwa kuacha siasa na kuwaachia wazee makini kwani vijana wa sampuli yake ndani ya CCM wameendelea kuwa sehemu ya siasa za kutumika na wazee kwa rushwa ili kupitisha matakwa ya wazee hao.Anachofanya Nape ni kukwepa aibu ya wazee wake kuzidiwa dau katika Rushwa kwenye chaguzi na wazee wengine waliokubuhu kwa kashfa za ufisadi hasa katika kampuni tata ya RICHMOND.
-Nani asiyejua CHADEMA imeshinda kata nyingi nje ya zile iliyokua ikishikilia?
-Katika uchaguzi huu CHADEMA imewanyang'anya CCM kata na kulinda kata zake
-Nape anamaanisha kuwa CCM ikiwa na uchaguzi shughuli nyingine ndani ya chama zinasimama?Wasira alikua akifanya nini Arusha?Wasira ni waziri na ni sehemu ya dola kwa mujibu wa kanuni za ovyo za uchaguzi Tanzania.Nape Mwenyewe alikua Shinyanga na Waziri wa zamani Maige
-Watu wenye legacy kama ya Dr.Slaa hawastahili kuacha siasa kwani kufanya hivyo vijana wa aina ya Nape hawatalipeleka taifa pazuri.Wanahitaji kufundwa hata kama wamenogewa ufisadi huko CCM
-Wakati Nape akijifanya CCM ilikua kwenye uchaguzi wake wa ndani,badala yake walitumia Dola na wahalifu sugu kutishia watu kujitokeza kupiga kura pamoja na Green Guard.Ni wakati sasa wa kuhuisha daftari la kudumu la wapiga kura na tufuate kanuni hai za demokrasia.Tuwe na mfumo ambao kila kijana anayefikisha miaka 18 moja kwa moja qjumuishwe kwenye daftari la wapiga kura
Pia sasa nitatoa wito kwa chama changu tuimarushe Red Brigade zaidi kulinda wafuasi wetu