Nape azungumza Chuo kikuu Cha Waislamu Morogoro: Aisifia Bajeti; aasa CCM

Nadhani sasa Nape atambue kuwa kumbe hata hao wanaovaa magwanda ya kijani hawako pamoja nao. Maana kikao hicho kilikuwa cha wanachama wa CCM na wao ndio wamevujisha taarifa hizi...
 
Kama kawaida zilitumika gari ndogo kadhaa kuwapeleka wafuasi hao kwenye mkutano,kifupi ccm inaendelea kutapatapa
 
Mpaka sasa sijaona Tatizo Kiongozi wa chama chochote kusema kama hatutafanya vizuri wenzetu watachukua nchi..........hapa sio suala la Silaa wala la Mrema.......nani akipewa nchi anauwezo wa kuiongoza? Period...
 
Nape, kwanza pole kwa kuwa misquoted, kwa position yako, kuwa misquoted kwa makusudi au kwa bahati mbaya, ni jambo la kawaida, na lazima ulikubali na kulizoea, ambapo kwa social forums zote uzushi pia upo kutokana na viwango tofauti vya uelewa kati ya mtu na mtu. Dawa ya uzushi sio tuu kuukanusha, bali kuurekebisha, just put things right na straight, kwa kueleza ulichomaanisha ili kuudefeat huo uzushi.

Hili la kuwa blocked mimi limenistua, sio kwa sababu halipo, bali siamini kuna kitu kama hicho jf. Nijuavyo mimi, wanaokuwa blocked ni wale ambao officially wamekuwa banned na sababu za ban zao hutolewa, hili la members kuwa blocked, ndio nalisikia kwako, na kama ni kweli linafanyika, its not fair, na inatubidi siye wengine tuanze kuiangalia jf kwa jicho pembe.

Mkuu umeongea yote!!!
Na naona Mods wameshaunganisha threads...

Kuna haja ya hawa jamaa kuwa na PR, ili kujua wao ni wakina nani na wanatakiwa wajibu vipi??...Nafikiri anahitaji muda wa kukomaa
 
Najua kuna wanasiasas humu ndani ya JF ambao wanafanya siasa tu kama mtoa mada hii. Lakini Nape wala usihofu kuhusu tuhuma kama hizi. Humu Jamvini kuna watu mbalimbali na wenye upeo na tabia mbalimbali. Kuna wengine wanatumia kwa maslahi ya kisiasa kwa kuwachafua wengine kama tulivyoona kwenye uchaguzi wa Bavicha. Pia kuna thread moja ziliwazushia Mh Lema na Zito. Kwa hiyo, wewe jibu kwa upole kwa kukanusha kama hujasema hivyo. Hiyo ndo siasa dungu yangu. Kuhusu kufuta thread, humu threads za kukadia CDM naona hazipiti kwani nilijaribu zikazimwa kweli. Nafikiri wakereketwa wa CDM ni wengi humu kuliko wa CUF, CCM na Taifa.
 
huko ndo saizi yake na ndo kwenye vibaraka wake huko. Chuo chenyewe kinatoa dgree za ajabu sana zinatambulika qatari, omani,saud arabia na afghanistani tu.
Komandoo, haya ulioyasema ni kweli au? Kama ni hivyo chuo cha nini basi? Watazalisha vijana wa namna gani?
 
WANAOTAKA KUJUA nilisema nini chuo cha kiislamu Morogoro,asome post ya Achebe ya mwanzo yenye kichwa cha habari....bajeti imelenga kutatua kero za elimu ya juu... Hata kama si yote ameyaandika Achebe lakini hiyo ni standard..
Kuhusu eti nimetembelea chuo cha kwasababu ni cha kiislamu, nadhani hawakuona nilipokutana na wanafunzi wa Udom na Tumaini Iringa.
 
WANAOTAKA KUJUA nilisema nini chuo cha kiislamu Morogoro,asome post ya Achebe ya mwanzo yenye kichwa cha habari....bajeti imelenga kutatua kero za elimu ya juu... Hata kama si yote ameyaandika Achebe lakini hiyo ni standard..
Kuhusu eti nimetembelea chuo cha kwasababu ni cha kiislamu, nadhani hawakuona nilipokutana na wanafunzi wa Udom na Tumaini Iringa.

Hukuzungumza chochote kuhusu Dr Slaa? Majibu yako yananifanya nitake kuamini kile ulichoita uzushi na huu wako ndio niuone uzushi. Huyo Achebe hajazungumzia hilo, kwa nini usiseme kwa kifupi kwamba sijazungumza lolote kuhusiana na huo ulioita uzushi au niliongea hili na hili kuhusu hilo. Sometimes huwa naona kama unatumia watu kuandika humu kwa niaba yako. Siamini kama ni wewe Nape, kama ni wewe kweli basi naanza kuamini kwamba unapokuwa kiongozi mkubwa ndani ya CCM ndio uwezo wako wa kufikiri na kujenga na kujibu hoja unapungua.
 
bajeti imelenga kutatua kero za elimu ya juu:nape

katibu wa halmashauri kuu ya taifa ya ccm itikadi na uenezi nape nnauye amesema bajeti ya mwaka 2011/2012 imelenga kutatua kero zilizojitokeza kwenye elimu ya juu .
Aliyasema hayo mjini morogoro wakati akizungumza na wanafunzi wa elimu ya juu wa vyuo vikuu vya morogoro kwenye mahafali ya kuwaaga makada wa ccm waliokuwa wakisoma kwenye chuo kikuu cha kiisilamu cha mjini morogoro.
Akitolea mfano uamuzi wa serikali kutoza kodi ya kukuza ujuzi(skills development levy), ambayo kwa bajeti ya 2011/2012 mgawanyo wake umelenga kupeleka asilimia 4% kati ya 6% ya kodi hiyo kwenye bodi ya mikopo na hivyo kuongeza uwezo wa bodi kuhudumia wanafunzi.
“mwaka jana kodi hii ilikusanya karibu bilioni 200, na huwa inaongezeka kadri uchumi unavyokua, mategemeo kwa mwaka huu wa fedha pesa hii itaongezeka hivyo kutenga aslilimia hiyo itasaidia sana kwenye kutatua tatizo la mikopo kwa elimu ya juu”alisema nape
akawataka wanafunzi wawapuuze wanaopita na kusema hakuna kilichofanyika huku wakijua wazi kuwa kila mwaka hatua kubwa tu inapigwa katika kushughulikia kero mbalimbali za wananchi.

“kumekuwa na maneno mengi juu utaratibu wa kutoa mikopo na uendeshaji wa bodi yake, lakini rais kwa kulitambua hili ameunda tume ya kuangalia namna bora ya kushughulika na hili la bodi, tume ikikamilisha, na hili ongezeko la pesa bila shaka changamoto nyingi zitapungua” alisema nape.
Nape aligawa vyeti vya kuhitimu kwa makada 65 wa chuo hicho na kupewa taarifa ya chama ya tawi hilo. Alipokelewa mkoani morogoro na viongozi wa ccm mkoa huo wakiongozwa na mwenyekiti wa ccm mkoa huo ndg. Petro kingu.



pengine angejiuliza ni wanafunzi wangapi wanajiunga na vyuo vikuu kila mwaka na wangapi wanamaliza darasa la 7 na kidato cha 4 ambao hawapati nafasi ya kuendelea na masomo. Angejiuliza pia kuwa ukiondoa msingi wa kuwawezesha vijana hawa ambao kwa kiwango kikubwa wanapaswa kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kujiajiri utakuwa na taifa la aina gani. Chukua mfano tu; hivi tunao uwezo wa kuanzisha garage kila kijiji kwa ajili ya kufanyia matengenezo zana za kilimo(power tillers) zinazonunuliwa na wakulima? Ufundi ungekuwa base ya kutatua tatizo hili. Tungempongeza kama serikali ingetenga asilimia 10 kwa ajili ya elimu ya juu na asilia 10 kwa ajili ya elimu ya ufundi. Vinginevyo; kwa rate ya vijana wanaofeli kidato cha nne kila mwaka na wakakosa hata nafasi za ufundi tunatayarisha bomu la hatari.
 
''Aliyasema hayo mjini Morogoro wakati akizungumza na wanafunzi wa elimu ya juu wa vyuo vikuu vya Morogoro kwenye mahafali ya kuwaaga makada wa CCM waliokuwa wakisoma kwenye chuo kikuu cha Kiisilamu cha mjini Morogoro.''

Makada wanapelekwa kusomea uislamu?
 
huko ndo saizi yake na ndo kwenye vibaraka wake huko. Chuo chenyewe kinatoa dgree za ajabu sana zinatambulika qatari, omani,saud arabia na afghanistani tu.

Wewe unaonekana huna akili na umetawaliwa na udini.... huna hoja, Kukaa kimya ni bora kuliko kuongea ujinga na watu wote wakajua ni mjinga... :crazy:
 
Muslim University iNATOA DEGREEN za ukweli tatizo lenu mshazoea degree za CHUPI nyinyi mziki wa MUM hamuuwezi
 
huko ndo saizi yake na ndo kwenye vibaraka wake huko. Chuo chenyewe kinatoa dgree za ajabu sana zinatambulika qatari, omani,saud arabia na afghanistani tu.

Mhhh ushabiki mwingine hata hauna maana. Ina maana shahada za ualimu zinazotolewa hapo hazitambuliwi hata na nchi kama Kenya, Tanzania, Uganda??? bali Qatar, Omani, Saudi Arabia na Afghanistani tu???? Acha chuki za kitoto hizo!!!
 
sasa ndungu huo ni udini sio siasa aja udinii jibu hoja za nape sio mambo ya chou.
 
digrii ni digrii tu hata kama inatambulika samunge peke yake.chuki zako za kisiasa zimekupofusha,angalia usianguke.aah vipi wewe kwa hiyo kiongozi akizungumza na wanafunzi wa Tumaini, sawa.Lakini akifika morogoro...............hii nchi yetu sote jamani.acha mawazo ya kale .watu wamesoma sana siku hizi na wanajua kinachoendelea.acha chuki.au kafiri nini?
baki kwenye mada ..mambo ya ukafiri yametoka wapi? nadhani inferiority complex inakusumbua ndiyo maana unaita wenzako makafiri ili ujifariji kidogo!! hizi dini zinazotuchanganya mbona tumeletewa na wageni tu!
 
Back
Top Bottom