Nape awasilisha Muswada wa Sheria wa Huduma za Habari

Habari ya Mujini

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
2,517
1,043
MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WA MWAKA 2016 WAWASILISHWA BUNGENI NA KUANZA KUJADILIWA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewasilisha bungeni muswada wa sheria ya huduma za habari wa mwaka 2016, mjini Dodoma, leo.

"Muswada huu pamoja na manufaa mengine mengi utairasimisha Tasnia ya Habari hapa Nchini" amesema Nape.

74202970cd699683fb3ffaaee965ae47.jpg
 
hakika nguvu iliyotumika ni kubwa mno.

Mtukufu anajua yote yaliyomo humo ndio maana kaahidi kuusaini mara tu utakapotua mezani kwake,, naona kamu attack mleta hoja badala ya ku attack hoja, hii ni njia za watawala kukudhoofisha usiendelee kuhoji..

kwa maoni yangu. sioni haja ya kuendelea kuwa na bunge.. itangazwe kuwa kwa awamu hii bunge limekuwa dissolved kwenye serikali.
 
Kuna mtu mmoja kasema hii press conference imefanyika kwa ile principle ya 'miluzi mingi.....' Hapa baadae leo na kesho focus itakuwa kwenye yatokanayo na press conference na baada ya hapo utasikia waandishi hawa hawa wanaanza kulalamika, hata yeye mwenyewe ni kama nimesikia akiwaponda!
Kinachosikitisha ni kuwa wahariri kama wa TBC, Daily News na Uhuru wanaona kama hii sheria 'haiwahusu' lakini wanachosahau ni kuwa Tido Mhando alikuwa TBC na sasa yuko chombo binafsi. Poor us!
 
Haya matukio mawili yawahusuyo wanahabari kutokea katika siku moja, je ni kitu ambacho kimepangwa au ni coincidence? Habari kubwa itakuwa maongezi ya wanahabari na Mh. wakija kustuka muswada umeshapita zamaaaniiii. Kweli siasa nia Sanaa na Sayansi pia
 
ikumbukwe kuwa ukimziba paka mdomo ujiandae kuparuliwa,hakuna nchi yoyote iliyofanikiwa kuminya uhuru wa habari ,ikatawala salama
 
Back
Top Bottom