Nape atoa msaada kujenga shule Mara

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
[h=3]NAPE AUKABIDHI MIFUKO 700 YA SARUJI MKOA WA MARA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARASA[/h]


NA BASHIR NKOROMO, MUSOMA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeukabidhi mkoa wa Mara tani za saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mkoani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimnisho ya miaka 35 ya CCM.

Saruji hiyo itatumika kujenga madarasa kwa ajili ya wanafunzi ambao wameshindwa kuanza kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa madarasa licha ya kufaulu mwaka huu.

Akikabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa mkoa huo, John Tupa, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema saruji hiyo imetolewa na makada wa CCM ambao wameamua kutoa mchango huo kwa kupitia CCM ikiwa ni kuunga mkono maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM.

Nape alisema makada hao ni Zulfikar Nanji wa Kampuni ya Mwanza Huduma Ltd (mifuko 400) Joseph 'Msukuma' Kasheku mfanyabiashara ambaye pia Diwani wa Kata ya Nzela, Geita na Mjumbe wa NEC, Vedastus Mathayo ambao wote wametoa mifuko 100 kila mmoja.

Alisema kada mwingine ni Dk. Isack Chacha Ng'ariba ambaye aliahidi kutoa tani 200 za saruji ahadi ambayo aliitoa papo hapo wakati wa makabidhiano hayo.

Nape aliwashukuru wafanyabiashara makada hao wa CCM kwa kuiunga mkono CCM katika kuhakikisha kwamba sherehe za miaka 35 ya CCM inakuwa na mafanikio makubwa kwa kutekeleza azma ya kuchangia shughuli za maendeleo.

Alisema, wafanyabiashara na makada hao wanaichangia CCM pia kama kuonyesha shukurani yao kwa kuweza kufanya biashara zao kwa miaka mingi katika mazingira ya amani na utulivu chini ya uongozi wa serikali ya CCM.

"Mkiona vinaelea vimeundwa, amani na utulivu huu uliopo ni mazingira yaliyojngwa na kuendelea kutunzwa na CCM tangu ilipoanza kutawala nchi hii baada ya kurithi uongozi kutoka vyama vya TANU NA ASP miaka 35 iliyopita", alisema Nape.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa alisema, jumla ya watoto 6486 kati ya asilimia 50.3 ya watoto waliofaulu, wameshindwa kuanza kidato cha kwanza mkoani mwake kutokana uhaba wa vyumba vya madarasa licha ya kufaulu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa unahitaji madarasa 718 wakati yaliyopo ni 479 na hiyo kuwa na upungufu wa madawati 239 na kwamba wilaya ya Bunda ndiyo inayoongoza kuwa upungufu wa madarasa.

Alisema licha ya kupata msaada huo wa saruji bado mkoa unahitaji mabati, mbao na madawati kwa ajili ya madarasa yatakayojengwa.
 
Naurumia sana huyu dogo
Wanamchambia na unapotea
Vijana tunakosa imani naye maana hana msimamo anatumiwa kama msalani
 

Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa unahitaji madarasa 718 wakati yaliyopo ni 479 na hiyo kuwa na upungufu wa madawati 239 na kwamba wilaya ya Bunda ndiyo inayoongoza kuwa upungufu wa madarasa.


jamani wilaya ya Bunda si ni jimbo la Steven Wassira?
 
Kawaida yao! Wanajitokeza wafanyabiashara wakubwa wanatoa hivyo vi misaada then wanajiambatanisha na mtu mkubwa wa chama eti yeye/chama ndo wametoa/kusaidia.Tushawazoea sana tu.
 
Naurumia sana huyu dogo
Wanamchambia na unapotea
Vijana tunakosa imani naye maana hana msimamo anatumiwa kama msalani
niwewe kweli au naota??
umekuwa msema kweli siku hizi hongera sana bibie!
 
Mimi nilidhani yeye Nape katoa zake mfukoni au mimi sielewi maana ya maneno hayo hapo juu ?
 
Heading inachanganya. Nape hajatoa msaada, amepokea msaada uliotolewa na makada wa chama chake kusaidia ujenzi wa madarasa mkoani Mara.
 
Sasa ni nini haja ya kuleta mavideo kamera kibao kama ni msaada wa kawaida?...
Hapo ujue msaada huo unaaandamana na mkono wa chuma uliofichama!
 
Namuona kama mbunge wa zamani wa Musoma Mjini bwana Manyinyi.
You're wrong, umuonaye ni mdogo wake Manyinyi aitwaye Vedastus - mjumbe wa NEC Mara. Manyinyi sasa hivi yuko busy na uwekezaji wilayani Serengeti. Mungu akipenda, anaweza kupambana na Dr Kebwe 2015 jimbo la Serengeti.
 
You're wrong, umuonaye ni mdogo wake Manyinyi aitwaye Vedastus - mjumbe wa NEC Mara. Manyinyi sasa hivi yuko busy na uwekezaji wilayani Serengeti. Mungu akipenda, anaweza kupambana na Dr Kebwe 2015 jimbo la Serengeti.

Mara kuna vituuuuko! Chambiri alishindwa Tarime akakimbilia Babati akawekeza akashinda; Manyinyi naye baada ya kushindwa Musoma Mjini amekimbilia Serengeti anawekeza huenda naye akashinda.

Hi Dr. Kebwe yupo kweli? si afadhali Dr. Wanyancha huwa namsikia kwenye mfuko wa barabara.
 
Back
Top Bottom