Nape ataja sababu madeni ya TTCL

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,032
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametaja sababu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupata hati chafu mfululizo kuwa ni urithi wa matatizo ya hesabu za kifedha yaliyoanza wakiwa na mbia wao kabla Serikali haijarudishiwa umiliki wa shirika hilo.

Nape alisema hayo jana jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika wilaya 23 nchini, ikiwa ni takribani wiki moja imepita tangu Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 kuwasilishwa bungeni na kuonyesha dosari kadhaa kwa T'TCL.

Miongoni mwa kasoro alizozibaini CAG, Charles Kichere ni TTCL lilikuwa na madeni ya Sh21 bilioni ambayo uongozi haukuweza kutambua wadaiwa husika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, TTCL ni kati ya mashirika yaliyo na deni kubwa kuliko mtaji walionao, kwani ripotibilieleza shirika lina jumla ya deni la Sh349.9 bilioni huku likiwa na mtaji wa Sh227.8.

Katika hafla hiyo,Waziri Nape alisema hoja ya madeni vasiyo na vielelezo iliyoibuka ilianza katika ukaguzi wa mwaka 2017/18 ikiwa na deni la Sh91.43 bilioni.

Alisema shirika hilo lilirithi kutoka kwa iliyokuwa kampuni ya simu Tanzania
iliyoanzishwa mwaka 1994 na mwaka 2016 mbia alitolewa kwenye kampuni hiyo na kuwa shirika la simu Tanzania mwaka 2017 kisha shirika la mawasiliano Tanzania.

"Shirika limepitia mambo mengi ambayo yamekuwa na matokeo hasi na chanya, limekumbana na changamoto zinazotokana na historia.

Mfano wakati wa ukaguzi 2017/18 kuna tofauti kubwa kati ya hesabu zilizoonekana kwenye mfuko wa anka-ra na mfumo wa hesabu.

Awali, akizungumza utiaji saini mkataba wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa kilomita 1520 katika wilaya 23 kati ya shirika hilo na Kampuni ya Huawei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la mawasiliano Tanzania, Peter Ulanga alisema mradi huo utakamilika kipindi cha miezi sita.

Alisema mradi huo utakaogharimu Sh37.4 bilioni, utakwenda kumaliza changamoto katika maeneo yaliyokuwa hayana mawasiliano, ili kuongeza matumizi ya Tehama, mitandao na kuboresha uchumi. "Kupitia upanuzi huu, kampuni za mawasiliano zitapata fursa za kibiashara ukizingatia tunaelekea katika mkakati wa kuunganisha mkongo na nchi jirani na hii itatusaidia kukuza uchumi na biashara nchini" alisema Ulanga. Ulanga alizitaja wilaya hizo

Kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mbogwe, (Shinyanga), Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Muheza, Kilindi, Mombo, Lushoto (Tanga), Ngara (Kagera), Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na Hai (Kilimanjaro), Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Longido, Mbulu (Arusha).

Pia Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti (Pwani), Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Ruangwa, Nachingwea (Lindi), Halmashauri ya Wilaya ya Newala (Mtwara), Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga (Ruvuma), Wilaya ya Ludewa (Njombe) na Halmashauri ya Wilaya ya Vwawa, Ileje mkoani Mbeya.
 
Pamoja na hasara hizo na wakaamua kujiandalia futari kwenye hoteli ya kitalii ya Johari Rotana.
Embu waache dharau zao za waziwazi
 
Nape akiwa kama waziri mwenye dhamana anapaswa kujikita zaidi katika kuzungumzia suluhu ya tatizo, zaidi ya kutumia muda mwingi kuelezea historia ya tatizo.

Tena anatilia mkazo tatizo hilo lilizidi kuwa baya katika kipindi cha utawala wa JPM. Hajui kuwa kwa kufanya hivyo anazidi kuamsha hisia mbaya sana dhidi yake. Afanye yale apaswayo kuyafanya kwa sasa ili shirika litengamae, na aachane na hizo ngonjera zake..
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametaja sababu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupata hati chafu mfululizo kuwa ni urithi wa matatizo ya hesabu za kifedha yaliyoanza wakiwa na mbia wao kabla Serikali haijarudishiwa umiliki wa shirika hilo.

Nape alisema hayo jana jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika wilaya 23 nchini, ikiwa ni takribani wiki moja imepita tangu Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 kuwasilishwa bungeni na kuonyesha dosari kadhaa kwa T'TCL.

Miongoni mwa kasoro alizozibaini CAG, Charles Kichere ni TTCL lilikuwa na madeni ya Sh21 bilioni ambayo uongozi haukuweza kutambua wadaiwa husika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, TTCL ni kati ya mashirika yaliyo na deni kubwa kuliko mtaji walionao, kwani ripotibilieleza shirika lina jumla ya deni la Sh349.9 bilioni huku likiwa na mtaji wa Sh227.8.

Katika hafla hiyo,Waziri Nape alisema hoja ya madeni vasiyo na vielelezo iliyoibuka ilianza katika ukaguzi wa mwaka 2017/18 ikiwa na deni la Sh91.43 bilioni.

Alisema shirika hilo lilirithi kutoka kwa iliyokuwa kampuni ya simu Tanzania
iliyoanzishwa mwaka 1994 na mwaka 2016 mbia alitolewa kwenye kampuni hiyo na kuwa shirika la simu Tanzania mwaka 2017 kisha shirika la mawasiliano Tanzania.

"Shirika limepitia mambo mengi ambayo yamekuwa na matokeo hasi na chanya, limekumbana na changamoto zinazotokana na historia.

Mfano wakati wa ukaguzi 2017/18 kuna tofauti kubwa kati ya hesabu zilizoonekana kwenye mfuko wa anka-ra na mfumo wa hesabu.

Awali, akizungumza utiaji saini mkataba wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa kilomita 1520 katika wilaya 23 kati ya shirika hilo na Kampuni ya Huawei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la mawasiliano Tanzania, Peter Ulanga alisema mradi huo utakamilika kipindi cha miezi sita.

Alisema mradi huo utakaogharimu Sh37.4 bilioni, utakwenda kumaliza changamoto katika maeneo yaliyokuwa hayana mawasiliano, ili kuongeza matumizi ya Tehama, mitandao na kuboresha uchumi. "Kupitia upanuzi huu, kampuni za mawasiliano zitapata fursa za kibiashara ukizingatia tunaelekea katika mkakati wa kuunganisha mkongo na nchi jirani na hii itatusaidia kukuza uchumi na biashara nchini" alisema Ulanga. Ulanga alizitaja wilaya hizo

Kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mbogwe, (Shinyanga), Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Muheza, Kilindi, Mombo, Lushoto (Tanga), Ngara (Kagera), Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na Hai (Kilimanjaro), Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Longido, Mbulu (Arusha).

Pia Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti (Pwani), Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Ruangwa, Nachingwea (Lindi), Halmashauri ya Wilaya ya Newala (Mtwara), Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga (Ruvuma), Wilaya ya Ludewa (Njombe) na Halmashauri ya Wilaya ya Vwawa, Ileje mkoani Mbeya.
sidhani kama nape anajua lolote kuhusu mambo ya finance.kwani ukirithi hesabu za nyuma ambazo tayari zilikaguliwa ndo inapelekea kuleta hayo madudu?inawezekanaje kuwe na deni halafu usimjue anayekudai.hiki ni kichekesho cha mwaka. hapa ni issue ya debit na credi tu kitu ambacho hata book keeper anajua sasa iweje watu wenye CPT (T) washinde kuikamilisha hiyo transactin ndogo tu?hapa napata shida na inawezekana ndo matatizo ya kuajiri vyeti na si ujuzi.haya mabodi sijui ya uhasibu,ugavi,ufamasia nk ni miradi tu si chochote wala lolote.tukubali kurudi tulikotoka.si vibaya kupiga U- Turn.
 
Hili shirika linatia kichefuchefu sio Siri huduma mbovu sijawahi kuona ukitaka wakuunganishe na fiber internet watakujazisha form wakikwambia watakuja kukufanyia survey, kitu ambacho cha dakika kadhaa kwa kutumia google map ila wao watakuweka miezi 3 na huduma hutapata. Nimeshatembelea mara kadhaa duka lao la Tegeta (Kibo Complex) wadada na mama mmoja wanaona ufahari kukaa ofisini pasipo wateja kupata huduma wenyewe wanakwambia vifaa hakuna mara maombi ni mengi visingizio vya kijinga kabsa kutoka kwa watu wasiojua majukumu yao ya msingi waliozoea uvivu pasipo kujali uhai wa shirika na mali zake, fikiria mdada ananiambia eti kama unaona unachelewa kwanini usiende kupata huduma kampuni nyingine nilisikitika majibu yake shirika limejaa watu wasio sahihi hawafai kulitumikia. Wito kwa waziri Nape hao watu sio wa kuchekea hebu wabane koo shirika linao uwezo wa kutengeneza pesa nyingi kupitia huduma za fiber internet kama wakiacha uzembe na kuwa na uchungu na mali ya umma hawana lolote zaidi ya kukuongopea na uvivu usio na mfano
 
Bao la mkono tu? Hili ni vurumai unayokuta shambani baada ya tembo kupita, kwanza unabaki na mshangao! halafu unapiga mayowe wooooi halafu unakaa chini na unakaa kimyaaaa yaani hizi jazba zote within 1min....na baada ya kutafakari unaona ni kana picha: mkono mithili ya mkonga wa tembo, pasua miti, vunja mizizi ili ale karanga aisee Inatia huzuni kwa uharibifu unaofanyika ukizingatia hasara kubwa itokekanayo na vijikaranga Yaani Aisee, duh dah ntiiii yaani aaaah ntiii

Chagua kwa Uangalifu 2025 hii tosha kwa sasa. Duh
 
Ndio maana watu wanataka TAKUKURU, Polisi na Bi Tozo kuchukua maamuzi yaliyo yao baada ya report ya CAG. Sio kusubiri ngonjera za wabunge kukaa, maana sampuli yenyewe ya wabunge ndio hao hakina Nape

Kwenye kichwa cha Nape shughuli za CAG zinahitaji majibu ya porojo kama siasa alizo-zoea. Kuna taratibu za kihasibu baada ya muda kukubali hilo sasa ni bad debt futa hiyo hela aipatikani tena ndio CAG anachoangalia. Yeye analeta porojo za siasa.

Unapata picha hizi ndio sababu miaka nenda-rudi kwanini mambo yale yale yanajirudia; mtaalamu anafanya kazi yake anakwambia tatizo A badala ya wahusika kuchukua hatua. Wanawapa nafasi watu kama kina Kibabaj kuangalia anachosema mtaalamu sawa kweli.

Sasa kuna ugumu gani wa kumuongea mtu kama huyo, ndio maana hakuna kinachobadilika. Ni sawa na bank kumdai marehemu ambae dhamana yake ilikuwa ajira kwa mtaji huo kungekuwa hakuna kutoa ‘non performing loans’ kwenye vitabu vyao ipo siku marehemu atafufuka na kulipa madeni yake.

Hovyo kweli
 
Dah!

Badala ya kusema wamejipanga namna gani, yeye lawama tu za awamu ya tano.

Zero kabisa
 
Back
Top Bottom