hekimatele
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 9,889
- 2,799
Tutajua mwezi ujao nani ni nani kwenye fani hii
Akiongea na MakutanoShow sasa hivi ameongelea kuhusu mgombea urais kupitia CCM baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mbio za urais.
Amesema hata kama mtu akijaza wapambe wake CC na NEC siyo kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa urahisi.
Alitoa mfano mara tatu kuhusu Lowassa kwamba siyo msafi na hata Nyerere alisema hivyo. Alisema kwamba siyo lazima kuwepo ushahidi bali kama watu wanaongea tu na kukuhisi inatosha kuthibitisha kwamba wewe siyo msafi.
lowassa ni chaguo la mungu kwetu sisi watanzania wapenda maendeleo
Magamba wote wachafu ndio maana Lowassa anachanja mbuga kuelekea 2015...Hakuna hata mmoja wa kumnyooshea kidole na kumwambia, "Kwa ufisadi ulioufanya nchi hii kamwe haustahili kupewa ridhaa na Watanzania ili kuwaongoza, hivyo kaa pembeni."
Mkapa mchafu, Mwinyi mchafu, Kikwete mchafu, SAS naye walishamchafua DHAIFU na kundi lake la mtandao, kwa UDHAIFU huo mkubwa uliopo ndani ya magamba Lowassa anajua watasema pembeni tu lakini hadharani wanaogopa kumkemea maana nao pia ni watenda dhambi hivyo ameanza kutoa rushwa mapema sana ili kujisafishia njia ya kwenda Ikulu 2015. Sijui mpaka tunafika October 2015 atakuwa ametumia mabilioni mangapi katika kutoa rushwa ili kununua ULAIS...Siyo siri nchi yetu imeoza!!!
I was right up to the moment I am still right to my comment and it standsthe war for the Presidential post in CCM has just began, who will be the winner? let us wait and see
Nimesikia baadhi ya wasomi wanawakosoa wale 'wanaowachafua' wenzao.
Kwani huu si mwendelezo wa sera za kulindana hata kama mtu ni mchafu asisemwe?
Kama sio sasa atasemwa muda gani?
Au chama vyama vinataka kuwaletea tena wananchi watu wachafu ili wapate kuchaguliwa na hatimaye kuongoza nchi?
Nadhani ni wakati muafaka kuanika mabaya na mazuri yote ya watia nia ili uma uwajue na kisha kuwatendea haki muda ukifika.
Isitoshe ni vyema mamlaka za uteuzi zikayafanyia kazi yote yanayozungumzwa ili watuletee watu safi.
almost wote ni wachafu, ila kwanini amshambulie Lowasa peke yake tena ni mara zote? kuna kitu hapa nyuma ya pazia!
Nape ni sawa na mbwa kibogoyo. Hang'ati. Amejaa unafiki mtupu. Hana uwezo wa kupambana na rais mtarajiwa wa Tanzania, Hon Edward Lowassa. 2015 ataumbuka sana huyo Nape.
almost wote ni wachafu, ila kwani amshambulie Lowasa peke yake tena ni mara zote? kuna kitu hapa nyuma ya pazia!