mbona kijani imetawala hapo? Nadhani lilikuwa kusanyiko la viongozi wote wa magamba .ccm ina wanachama kiduchuu sana hapa SAUT na ukiwachunguza karibu wote ni watoto wa mafisadi na jangili.
aha aha aha aha kweli siasa noma 2012 aliadi mpira jezi gari ajawai kupeleka apo nsumba high school aliposomea leo hii amekuja tena saut atawapromic saut mpaka ndege kazi kwenu
magamba hamjielewi kweli cku ya leo nimesikia watu wanasema pesa tukipewa na ccm tunachukuwa 7bu ni kodi zetu ila kura hawapti hata mimi npo tayar kupokea money but kura ni ndoto 2015.
Njaa haichagui msomi au mbumbumbu, wote matumbo yanahitaji kushiba, wali wanaohongwa wanafunzi wa SAUT hautofautiani na anaohongwa mwanakijiji wa Iselamagazi.
""hatuhitaji ser 3 bali tunahitaji maendeleo""Ni ukweli usiopingika kwamba tunahitaji maendeleo kwa gharama yeyote kama linavonadi bango mojawapo hapo. Kuna watu wakitoa hizi kauli sitoshangaa lkn kuna wengne ambao unategemea wawe ndo kioo na mwanga kwa jamii yetu yenye mauzauza mengi na umaskini uliopitiliza huku nchi ikisheheni rasilimali pasi mfano wa nchi nyingne yeyote africa. Hao wanafunzi walobeba mabango (siwezi waita wasomi coz wengne ndo semister ya 2 tu chuoni na wengne pengne wasihitim) Wameshindwa kujiuliza hiyo miaka 50 ilopita tulikuwa wapi na ser 2 tusipate maendeleo ndo tuje tuyapate leo? Watupe mikakati thabiti na hakika kuwa kwa mpango maendeleo tuloupanga sasa baada ya miaka 50 utaleta tija tofauti na ile ya awali.
Lakini zaidi ya hilo wanashinwa kujua kwamba katiba nzuri ni ile inayojenga mfumo imara ktk kuendesha na kusimamia vema uchumi wa nchi. Kwa mfumo huu ambao kila mmoja "mjasiriamali kifisadi" na hakuna kuwajibishana wala anaeonyesha kujali zaidi ya kutetea wezi na kuwahifadhi tutasubiri sana hicho wanachokiita maendeleo. Msije mkajaribu kuwaita wasomi tafadhali kwa sababu hawaelewi walichokiandika/walichoandikiwa
Hahahhaha! Mabavicha mmehangaika weeee mwisho yametimia niliwaambia hamuwezi zuia mafuriko kwa viganja!!! Rais wa serikali ya wanafunzi SAUT, Saimon Filbert Macheyeki kakabidhi kadi ya CDM kwa Nape na kupewa kadi ya kijani kadi ya CCM.
Huyo macheyeki tulishamfukuza kitambo lakini akakatalia kadi ya cdm na habari zake zilishawahi mwagwa hapa kitambo,kumbe alitaka kuvuna mapesa kutoka ccm?
Huyo macheyeki tulishamfukuza kitambo lakini akakatalia kadi ya cdm na habari zake zilishawahi mwagwa hapa kitambo,kumbe alitaka kuvuna mapesa kutoka ccm?
Hivi kijana wa chuo kikuu na akili timamu unaishabikia ccm.unaacha masomo unamsikiliza mtu kama nape..utakuja kujuta maishani na hakika utakuwa maskini milele
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif]Zaidi ya Watu 420 wajiunga na CCM[/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif]Wanachuo SAUT waahidi kudumisha Umoja wao na Ushirikiano [/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif]Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage na wananchi wa Nyamalango ,wilaya ya Nyamagana Mwanza ambapo aliwaambia kuwa CCM itaendelea kuongoza kwani ndio chama pekee chenye sera inayoeleweka kwa wananchi,mipango na ahadi zake zinatekelezwa kila kona ya nchi.[/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif] Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea kadi ya CHADEMA kutoka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agustine Ndugu Simon Philbert Macheyeki ambaye amejiunga rasmi na CCM,katika mkutano huo zaidi ya wanafunzi 86 wa chuo hiko wamejiunga na CCM na wanachama wapya 420 wamejiunga na CCM.[/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif]Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi kadi ya CCM Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine Ndugu Simon Philbert Macheyeki ambaye amejiunga rasmi na CCM,katika mkutano huo zaidi ya wanafunzi 86 wa chuo hiko wamejiunga na CCM na wanachama wapya 420 wamejiunga na CCM.[/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif] Kadi za wanachama wapya waliojiunga na CCM kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine Mwanza.[/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif]Wanachama wapya 420 wajiunga na CCM kutoka Chuo Kikuu cha SAUT Wilaya ya Nyamagana[/FONT].
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif]Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agustine Ndugu Simon Philbert Macheyeki akila kiapo cha kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamalango wilayani Nyamagana.[/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif] Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wananchi na wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage Mwanza[/FONT].
[FONT=Arial,Helvetica,sans-serif]Wanachama wa Tawi la CCM SAUT wakiburudisha kwa kucheza na kuimba nyimbo mbali mbali.[/FONT]
Janga la kitaifa, Ukiona vijana wanashabikia vyama ambavyo vimeshindwa kuwajali watu wake zaidi ya ubinafsi wakati wengine wametoka kama kwetu Lindi ambako hali ni ngumu kijiji.
Kimsingi kama huu ndio mtizamo wa vijana hawa na hayo yanayoonekana kwenye mabango, basi kama yanatoka nyoyoni mwao. Basi niendelee kuisikitikia Tanzania na hususan wako siku za karibuni hasa pale watakapogundua kuwa ndoto zao hazitmiliziki. By the way ndio mitanzania.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.