Katibu wa itikadi n uenezi wa chama cha mpinduzi (ccm) Nape Nnauye amemtaka katibu kuu wa chadema dr. Wilboard Slaa kuwaeleza Watanzania fedha ambazo amepewa na nchi za Ulaya kwa ajili ya uchaguzi mkuu na masharti yake ni yapi na asipoeleza CCM itayaweka bayana.
Nape alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyikakijiji cha Biharamulo mkoani Kagera amabapo alisema wanaushahidi wa masharti aliyopewa Dr. Sla kwa niaba ya chama chake na lengo za nchi hizo la kufanikisha uchaguzi mkuu
Alisema kabla ya kuanza kutumia fedha hizo ni vemaDr. Slaa akawaambia watanzania masharti gani amepewa ili wapime na kuona dhamira ya chama hicho kinyume CCM itaeleza kila kitu hatua kwa hatua na kutaja masharti yote amabayo Dr. Slaa amepewa na waliotoa fedha hizo
Akifafanua, Dr. Slaa yupo nchi za Ulaya na kilichompelek ni kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu na tayari nchi kadhaa zimempa fedha tayari kwa kwa masharti ambayo lazima wayatekeleze na ccm tayari imepata masharti hayo, hivyo kabla ya kuwaambia Watanzania, Dr. Slaa aseme akishindwa hawatakaa kimya.
Alisem kwa sehemu kubwa fedha amabazo zimetolewa na baadhi ya nchi za ulaya kwa chadema hazina nia njema kwa Watanzania ndio maana wanataka Dr. Slaa awe mkweli kwa kueleza masharti gani aliyopewa.
Chanzo: jamboleo
June 16, 2015