Nape amtaka Zitto kujenga upinzani wa kweli

Nape amtaka Zitto kujenga upinzani wa kweli

zinyalulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
420
Reaction score
224
Salaam,

Nimesoma gazeti la Nipashe, Nape akimtaka Zitto kuanzisha upinzani wa ukweli sio kama wa CHADEMA.Kwa mujibu wa Nape amesema CHADEMA siasa zao zinaligawa taifa.

Mimi najiuliza ni upinzani gani anaoongelea Nape kwa Zitto? Maana ili taifa lisigawanyike lazima wote tuwe CCM na ni upinzani gani anaomtaka Zitto kuanzisha nakuifurahisha CCM?

Nawasilisha
.

Siku chache baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kutangaza kujiunga na chama cha ACT-Tanzania, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amemtaka kujenga upinzani wa kweli kwa ajili ya kujenga nchi na si kubomoa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro, Nape alisema anamkaribisha mwanasiasa huyo upya katika ulingo wa siasa.

Alisema kinachotakiwa ni upinzani wenye lengo la kujenga na Zitto akitaka heshima aachane na siasa za Chadema zenye lengo la kuvuruga.

Hata hivyo, alisema hawawezi kuwa na mfumo wa vyama vingi vyenye lengo la kubomoa, hivyo ajenge upinzani wa kweli wa kuijenga nchi.


CHANZO:
NIPASHE
 
Nape anaamini kuwa upinzani wa kweli ni kuwa mpinzani wa kweli wa upinzani.

Anamkumbusha jamaa yao.
 
Hahahahaha maccm kwa maccm yanapeana mbinu za kuangamiza upinzani nchini
 
CCM wanataka kuwapumbaza ACT kuwa ni partners sasa ACT chukua wafuasi huko CCM ,cdm,cuf kadiri uwezavyo na wao watachukua ACT Kadiri wawezavyo hizo ndizo siasa
 
Nape ukitoa matumbo yenu, hakuna kitu mnachosimamia na kusaidia nchi, je tutateseka mpaka matumbo yenu aache kuwasumbua au la???
 
Nape asipoitaja Chadema kwenye mikutano ya ccm bas choon hataenda siku hiyo..
 
ACT na CCM ni washirika , Zitto atalipwa mafao yake yote - Makinda .
 
Salaam,nimesoma kwenye nipashe nape akimtaka kuanzisha upinzani wa ukweli sio kama wa chadema.kwa mujibu wa nape amesema chadema siasa zao zinaligawa taifa.mimi najiuliza ni upinzani gani anaoongelea nape kwa zitto?maana ili taifa lisigawanyike lazima wote tuwe ccm na ni upinzani gani anaomtaka zitto kuanzisha nakuifurahisha ccm?nawasilisha

mkuu kwa kauli hyo bac ACT ni dhahiri tawi la ccm....
 
vuvuzela limeshindwa kuficha mahaba yake kwa Zitto
 
Last edited by a moderator:
Taifa wanaligawa wao na makundi yao ya kusaka urais, wapumbavu kabisa hawa
 
Zito ni mwanaccm lazima nape amkumbushe kazi waliyotuma zito kuubomoa upinzani haijaisha.
 
Nape anaposema kugawa Taifa chadema wanasiasa za ukabila na ukanda ndiyo maana wanagawa taifa.
 
Nape ana zuga,wakati ACT na CCM ni familia moja.
 
Back
Top Bottom