Nape amjibu Lowassa kuhusu Ajira...!

Lowasa ni mnafiki mkubwa sana. Analiona tatizo hili baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu?. Amekuwa madarakani muda mrefu sana kwanini alizungumzie leo hili suala?. Kwa hadhi na heshima anayopewa Lowasa ana sababu gani ya kwenda kuongelea hili suala makanisani ili hali anaweza kuwasiliana na viongozi husika na kuwaeleza?. Amekuwa Mbunge na waziri wa wizara tofauti muda mrefu sana, huyu kiumbe ni hatari kuliko mchawi. Hivi kwanini serikali haimkamati na kumweka rumande mnafiki huyu?.
 
Lowasa ni mnafiki mkubwa sana. Analiona tatizo hili baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu?. Amekuwa madarakani muda mrefu sana kwanini alizungumzie leo hili suala?. Kwa hadhi na heshima anayopewa Lowasa ana sababu gani ya kwenda kuongelea hili suala makanisani ili hali anaweza kuwasiliana na viongozi husika na kuwaeleza?. Amekuwa Mbunge na waziri wa wizara tofauti muda mrefu sana, huyu kiumbe ni hatari kuliko mchawi. Hivi kwanini serikali haimkamati na kumweka rumande mnafiki huyu?.
Serikali imkamate na kumweka lumande kwa jambo lipi!!! Mawazo yako yamepinda sana. After all, hata kama alikuwa kiongozi na hakushughulikia hilo jambo, hiyo haimwondolei uhuru wa kusema na kuishauri serikali kushughulikia jambo analoliona kuwa ni muhimu kwa ustawi wa nchi. Tatizo la nchi hii, kila kitu kikiongelewa lazima kihusishwe na uhasama wa kisiasa hata kama ni kitu chema. Ptuuuuuu, ujinga gani huuuuuu!!!!
 
Nape,
Nakubaliana na hoja hii kwamba Lowassa alikuwa wapi siku zote hasa alipokuwa waziri mkuu?nilitegemea angetoa data kwamba ni kwa kiasi gani alichangia katika ongezeko la ajira kwa kusimamia project A,B,C,D na nyinginezo na jinsi ambavyo serikali ilishindwa kusimamia.

Kama hakuliona hili akiwa waziri ni kosa.....lakini kama katambua sasa na kulinyamazia ni ADUI WA TAIFA



Kashfa zinazomuandama Lowassa za RICHMOND,zilichangia kukwamisha ujenzi wa viwanda ambavyo vingetoa Ajira

Mwatex.Urafiki,Kiltex,UFI nk.... JE?..Vimekufa kwa sababu ya Richmond? Tujadili hoja hata kama huyu mtu hatumtaki.
 
Nape is just making a fool out of himself. First of all, Lowassa didn't call the youth bomu but he used a figurative language to depict the severity of the problem. Nape is well known for his insatiable appetite of taking one's words out of context. The issue here is not what Lowassa did when he was a prime minister but rather what he asserted about youth unemployment in our country. Nape et al. should shift their focus on curbing unemployment instead of attacking the messenger. Everyone knows that Lowassa has been involved in a lot of shady deals but that can not be used to belitle what he has asserted. As the old saying goes, " to wrongs don't make a right."
 
Kimsingi hali ya ajira sio njema, ila ninaona kama jambo hili linapelekwa kisiasa zaidi kuliko vile ilivyotaiwa kufanywa.
Jambo la hatari kabisa ni kwa EL kulifanya hili kama karata yake ya kukubalika na vijana hii nayo haijakaa vyema.
 
Si maneno ya Lowassa kusema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni (kama) bomu.
Si maneno ya Nape kumlaumu Lowassa kuwa "yeye alifanya nini akiwa Waziri Mkuu.
Si maneno ya kukurupuka ya Gaudensia Kabaka ya kusema Tutajenga vituo vya ajira nchi nzima.

Cha kushangaza, Lowasaa, Nape na Kabaka wote ni wa CCM, kwa hivyo tatizo la ajira halitatatuliwa kwa wao kulengeana madongo, na wala halitataliwa kwa kukurupuka kwa Bi Kabaka na kuja na ahadi za uongo kwa sababu tu anataka kuzima kauli ya Lowassa. Kikwete yupo madarakani miaka mingapi mpaka leo baada ya Lowassa kusema ndio wanakumbuka shuka wakati kumeshakucha?

Vijana wasio na ajira asilima 21, wanataka kazi, hawataki bla bla bla. Kwa hivyo Nape, Lowassa, Kabaka, wacheni hizo na mtimize wajibu wenu wa ajira kwa vijana. Maneno ya Lowassa, iwe alifanya chochote, iwe hakufanya kitu, ukweli ni kuwa hivi sasa kuna vijana hawana ajira na kama lisipotatuliwa, linaweza kuwa zaidi ya bomu.
 
Ndivyo uongozi wa serikali legelege ya JK/CCM unovyofanya siku hizi, hawana hoja ya namna ya kuondoa hilo BOMU la vijana wasio na ajira kwa kutumia rasilimali (natural resources na man power) lukuki tulizojaliwa na kudhibiti ufisadi, wanachoweza ni MIPASHO
Itapigwa mipasho weeeeeeee (Kabaka/Nape/soon watajoin Pinda na JK mwenyewe vs fisadi EL) hakuna lolote litakalofanywa na serikali yetu hii huku BOMU likizidi kukua. Likilipuka (soon) wataanza mipasho tena weeeeee (vs EL) badala ya kudhibiti madhara yake. Namna hii 2015 mbali sana!
 
Nilichokurupuka ni kipi? au kwasababu nimepingana na hoja ya kuwaita vijana bomu kila siku? Na kisa kasema flani? Lazima umtukane nape na kumwita mbumbumbu ndio siku yako iende?... Serikali imetoa takwimu za hali halisi ya ajira nchini, nikatakiwa kutoa maoni, nilichojibu kuwa serikali iko sahihi, hali ya ajira nchini kwa takwimu sio maneno ya barabarani, na hasa ukilinganisha na nchi hata za Afrika mashariki tu Tanzania ni bora kuliko zingine, umbumbumbu wa Nape uko wapi?

Nadhani ni vizuri pamoja na kutakiwa kutukana kila unapokuta jina la Nape, akili za kuambiwa changanya na zako....

Kijana punguza speed...your are oblivious wa mambo mengi. Kuwa msemaji (Mwenezi) wa chama hakumaanishi kuwa unaweza kuisemea serikali.
 
Back
Top Bottom