Nape amjibu Lowassa kuhusu Ajira...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape amjibu Lowassa kuhusu Ajira...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Mar 23, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 827
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nnauye amjia juu Lowassa

  Waandishi Wetu | Mwananchi | March 22, 2012

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amemtaka Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kueleza jinsi alivyoshughulikia kutatua tatizo la ajira wakati akiwa Waziri Mkuu.

  Kauli hiyo ya Nnauye inakuja siku moja baada ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka kueleza kwamba tatizo hilo haliwezi kufafanishwa na bomu na kufafanua kuwa wanaosambaza uvumi huo hawaitendei haki Serikali.
  "Kila siku wanalalamika Serikali ya CCM inatengeneza bomu katika suala la ajira, lakini hao wanaolalamika si walikuamo madarakani na walifanya nini.

  "Unapofika wakati unazungumzia masuala yanayogusa jamii na Taifa kwa ujumla unapaswa kuwa na uhakikika na unachokisema sio kupita katika makanisa kuongea kitu ambacho huna uhakika. "Amekuwa akitumia njia mbalimbali hususan makanisani kuelezea tatizo la ajira ambalo linaitatiza serikali, lakini mimi nabaki na msimamo ule ule kuwa yeye alipokuwa serikalini (Waziri Mkuu) alifanya nini kutatua tatizo la ajira," alihoji tena.

  Tucta
  Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi (Tucta), Nicolas Mgaya alisema suala la ajira bado ni tatizo kwa serikali na kwamba linapaswa kutatuliwa.

  Mgaya alisema kuna vijana wengi wanahitimu masomo katika kila fani kwamba kupata kazi ni tatizo ambalo kama litasimamiwa ipasavyo litapungua.

  Mgaya alisema serikalini kuna upungufu wa wafanyakazi, lakini inashindwa kuajiri, sasa umefika wakati wa kuziba mapengo hayo na kuwaondoa vijana walioko mitaani bila ajira.

  "Katika shule za msingi na sekondari kuna upungufu wa walimu, lakini majumbani kwetu kuna vijana waliohitimu masomo ya ualimu hawajaajiriwa sasa hapa serikali inataka kutatua ama inaongeza matatizo," alihoji Mgaya.


  MY TAKE:
  Hawa CCM wanataka tuwaelewe vipi kujibizana wenyewe kwa wenyewe?? Hivi majibu haya ya Nape yanaonyesha nini katika ushiriki wa Lowasa kwenye Kampeni Arumeru ikiwa ataamua kwenda????
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,292
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nape ni mnafiki, kesho atasimama kumsifia Lowassa jukwaani Arumeru
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 827
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nakubaliana na wewe, hakawii kula matapishi yake kama alivyofanya wakati wa sakata la kujivua gamba
   
 4. m

  mahoza JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,230
  Likes Received: 398
  Trophy Points: 180
  Hehehehe ndugu wakigombana chukua jembe ukalome wakipatana ( sijui Kama Hawaii watapatana) Lowasa alileta ajira gani kwa vijana? Aache unafiki wakupita makanisani kujikosha. Angeita mkutano wahadhara aseme hayo ndio angeiata. Why can't he shutup his big mouth? He's a disgrace 2 da nation.
   
 5. Matunyengule

  Matunyengule JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 701
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nape ni mbumbumbu wa uongozi kwani kitendo cha kumshambulia Lowassa kuwa alifanya nini wakati akiwa kiongozi ni kukubaliana na Lowassa kuwa ni kweli Kikwete hana maamuzi au maono ya kutatua tatizo la ajira bila Lowassa. Nape uwe na data za kukusapoti si kukurupuka tu msema hovyo wa magamba.
   
 6. H

  Honey K JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilichokurupuka ni kipi? au kwasababu nimepingana na hoja ya kuwaita vijana bomu kila siku? Na kisa kasema flani? Lazima umtukane nape na kumwita mbumbumbu ndio siku yako iende?... Serikali imetoa takwimu za hali halisi ya ajira nchini, nikatakiwa kutoa maoni, nilichojibu kuwa serikali iko sahihi, hali ya ajira nchini kwa takwimu sio maneno ya barabarani, na hasa ukilinganisha na nchi hata za Afrika mashariki tu Tanzania ni bora kuliko zingine, umbumbumbu wa Nape uko wapi?

  Nadhani ni vizuri pamoja na kutakiwa kutukana kila unapokuta jina la Nape, akili za kuambiwa changanya na zako....
   
 7. H

  Honey K JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unafiki wa Nape ni upi?

  Kama kusimamia msimo wangu kuwa rasilimali za nchi lazima zifaidishe watanzania walio wengi ni unafiki, nina furaha kuitwa mnafiki.....

  Kama kwa kusema watu waache ufisadi na ulafi wa madaraka ni unafiki jina hilo linanifaa sana....

  Haya mengine ya Arumeru Mashariki, najua ni hasira za kushindwa kutakakowakuta, na najua itakuwa aibu kubwa kwa magwanda, si vibaya mkitanguliza hasira zenu kwangu maana mie ndo punching bag.....
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu una hakika kwamba wote wanaokushambulia ni wapinzani?
   
 9. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Ww Nape ni mbumbumbu kuliko nilivyodhania.. Hebu soma Signature yangu chini hapo. Bora unyamaze ili tudhanie unajua. Yaan mama Kabaka analeta hadithi za 2006 kurudi nyuma halafu tumwamini. Hey give us a break kabisa.
  Haya tuambie toka Feb 2008 ni mradi gani mkubwa mmeleta nyinyi? Lowassa was everything 4 u guys coz he got plans na anaweza thubutu kuliko Mkwe...re anaiba bila hata mipango. Miradi mikubwa yote alisimamia Lowassa na yy ndio alikuwa mzee mikakati japo only 2 years.
  Narudia kusema na nitasema serikali ya JK ni janga la kitaifa na hii CCM yenye sekretariet mbovu kiasi hiki ndio janga bab kubwa kwa watanganyika. Makamba anaonekana alivyo smart hata akiongea lakin Huyu Nape na katib mkuu ni janga la kitaifa +++
   
 10. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 20,130
  Likes Received: 10,046
  Trophy Points: 280
  Lowasa alisema ataendeleza mapambano, je ueamua kumwekea kigingi?lakini Nae achana na statistics zenu za kupika, je sio kweli kwamba vijana ni bomu, ivi kuna hiaji lolote kubwa la vijana kwa sasa tofauti na ajira?au kwa kuwa kasema Lowassa ndio imekuwa ishu. Majibu unayotoa ndio suluhishi la tatizo kwa kuwa moyo wanko unakiri kuwepo kwa tataizo. Nape mheshimu sana Lowasa, amekuumiza mara chungu mzima, unapenda akumalizie kabisa, hata ushawishi wako mdogo usiwepo tena, yaani akutie kwenye mfuko wa shati badala ya mfuko wa nyuma kama iivyo sasa
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 135
  kukurupuka jadi yao wanabishana mpaka na ukweli.
   
 12. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 135
  nyie akina Nape mnadhani si tunakula hayo matakwimu? Sijui unachopinga kitu gani? Kama mtu hakufanya lolote bas asiseme lolote na nyie muendelee kutofanya lolote? Endeleeni kugawana tu ajira kindugu, ipo siku mtajutia mnayoyafanya..
   
 13. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi Nape, umeona wapi Mafisadi wakaacha Ufisadi kwasababu tu mtu kama wewe umekwenda kuongea kwenye Chombo cha habari na kuwataka waache Ufisadi!

  Kumbuka unavyomuuliza "hesabu" yake Lowasa, hata wewe utakuja kuulizwa "hesabu" yako ya kuwaadaa wananchi. Unajua fika kuna vyombo vya kushughulikia ufisadi na mafisadi, hutaki kuvitumia, unapiga domo kwenye vyombo vya habari ili kuwahadaa wananchi wakuone kwamba unachukizwa na Ufisadi!
   
 14. M

  Makupa JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Nape nakubaliana na wewe kabisa si vizuri hata kidogo ukawaita vijana kuwa wao ni bomi, ili mradi tu anaeneza hii sumu aweze kupata sapoti ya vijana kwa ajili ya malengo yake binafsi.Ndugu yangu Nape kuhusu tatizo la ajira sidhani kama ni kweli kuwa kenya wana matatizo kuliko tanzania, usisahau kuwa kenya ina viwanda vingi kuliko tanzania kwa msingi huo vyanzo vya ajira kenya ni vingi kuliko tanzania
   
 15. TETILE

  TETILE Member

  #15
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nape Nnauye!

  Wewe mwenyewe uko hapo kwa sababu baba yako alikuwa mwanasiasa kwa Tanzania tumezoea kurithishana uongozi kama wafalme.
  Sasa basi na hili mtalishuhudia Arumeru Mashariki.

  Lowasa kaondoka madarakana feb 28 2008, kipi kipya kilichobuniwa na kufanyiwa kazi na CCM au ni migomo ya kila siku ya vijana Vyuoni,mgomo wa madaktari,mgao wa umeme usio na kikomo.

  Hakika Lowasa angekuwa madarakani angekuwajibisha wewe kwanza halafu wafuate wengini wasiotimiza wajibu wao.

  Kama huamini endelea kupiga domo kama hatamwambia BOSS wako (JK) Akubwage.

  Soma alama za nyakati JK na ED wako pamoja na wana maamuzi yoyote juu yako!
   
 16. A

  Ahakiz Member

  #16
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha uongo serikali hii ya tz haina takwimu za vijana ambao hawana ajira ila wana takwimu za wazee ambao wamesitafu halafu wanawapa ajira za vijana kama unabisha kuna majina ya wakuu wa mikoa na wilaya yanaanza na kanali mstaafu,ruteni mstaafu na bodi mbalimbali kuongozwa na akina mzee mzindakaya,akina pius msekwa na wengine zile zote ni ajira za vijana na mie nikiwemo
  hiyo serikali acha iendereze mipasho kwenye maisha ya watu.
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 11,832
  Likes Received: 1,287
  Trophy Points: 280
  Wewe nape ni gamba la kufa mtu au kwavile wewe unakazi hapo ccm unafikiri na sisi tunatembelea v8 Kama wewe
   
 18. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,773
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Hapa ndio umbumbu wake wewe bwana mdogo nape unajidhihirisha.kujiringanisha na kenya. Mtwara wana msemo kwamba umenifirisi sina la kuongeza.
   
 19. V

  Visionmark Senior Member

  #19
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maisha yamebadilika sana Nape, si kwa Tz tu bali ni kwa nchi zote duniani. Watznia wa miaka hii sio wale wa enzi hizo, hapana! Watznia wa leo ni watu ambao wanataka kuona kile walichoahidiwa na viongozi wao kinafanyika, kinatekelezwa na kionekane kiuhalisia sio tu kuja na takwimu ambazo ziko tofauti kabisa na hali halisi ilivyo na ukategemea kwamba wa2 watakuamini kiurahisi, hakuna! Viongozi we2 wanapaswa kubadilika kwa kiasi kikubwa sana! Watznia tunataka vitendo na sio maneno ama takwimu za kupika!
   
 20. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #20
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,531
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  anaweza kukana kuwa Hajasema na atalipandisha mwananchi mahakamani! Magamba ni zaidi ya kinyonga!
   
Loading...